Nitumie maneno gani kuwatahadharisha watoto wangu wa kike dhidi ya ukatili wa kijinsia?

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,372
Wakuu,

Kila kukicha tunashuhudia kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto wa kike na kiume hapa nchini.

Yale maeneo ambayo tulidhani ni salama zaidi kwao, nako tayari pameonesha kwamba kunaweza kujitokeza pia mambo haya ya ukatili. Sasa hivi si Kanisani/Msikitini, shuleni wala nyumbani pana usalama wa asilimia zote.

Tumeshuhudia Wachungaji, Masheikh, madereva wa mabasi ya shule (ma anko), walimu na hata baadhi ndugu wa karibu kabisa wakihusishwa na vitendo hivi viovu.

Kwahiyo kama mzazi huwezi kuwa maeneo hayo yote kumlinda mtoto wako, ni lazima atakuwa mikoni mwa hao niliowataja na hata ambao sijawataja kwa namna moja au nyingine hilo halikwepeki.

Kwa maneno mengine ni kwamba hapa lazima mtoto mwenyewe ajengwe au awezeshwe kujilinda yeye mwenyewe anapokuwa peke yake.

Hivyo kwa wale wazazi au wataalamu wa saikolojia za watoto naomba ushauri, nitumie maneno gani yanayofaa kuwatahadharisha watoto wa kike darasa la tatu na chekechea namna ya kujilinda na ukatili wa kijinsia maeneo mbalimbali kwa kadri ya uelewa wao ili wawe salama?

Ni muhimu kuchukua tahadhari kabla ya hatari, tusiache kuwaombea kwa Mungu awaepushe na maovu haya, lakini acha tufanye kadri ya uwezo wetu na Mungu atafanya yaliyobaki.

Karibuni kwa ushauri.

IMG_20221018_134429.jpg
 
Wafundishe watoto wako upendo, wafundishe watoto wako wasiongee na kuuugopa uongo, build friendship now ili wasikufiche chochote, wakuone kuwa ndiye mtu wa kushare chochote na wao, na very important wafundishe neno NO linamaana ni NO,na wanaposema NO hata body language yao ionyeshe ni NO, monitor marafiki wao(including parents wao),mkuu hili linawezekana wekeza kwa watoto wako...TRUST TRUST
 
Asante hilo ni muhimu sana,kujenga trust ili awe muwazi kukueleza chochote,hii nadhani itasaidia kwamba kama kuna ukatili anafanyiwa asikae kimya lakini bado hujasema sasa unawaambiaje ili wakikutana na hawa wahalifu wajue wanafanya nini?
 
Wajengee watoto wako mazoea yaani wawe free kukwambia jambo lolote wasikuogope, wajengee kujiamini, pendelea kuwasifia mara kwa mara "wewe ni mzuri sana, ukisoma kwa bidii utafika mbali na kua mtu makini".... waambie neno " Nakupenda Binti yangu/I love you kid/daughter"

Hiyo itawafanya hiko neno wasilione ni geni kwao kwa maana hiyo wasihadaike,

Waambie wakae mbali na Jinsia ya Kiume, ikitokea mwanaume kamuita peke yake akimbie na aripoti haraka, asikubali kuitwa Mchumba na mtu yoyote aripoti, ikitokea mwanaume kamshika sehemu yoyote ya mwili apige kelele na aripoti haraka sana,

Kama wana miaka 8+ waambie kuhusu Ukimwi waambie unaambukizwa kwa kushikwa hata mkono tu na mwanaume ambaye sio Baba ake au Kaka ake kwa hiyo asikubali kushikwa na aripoti haraka sana,

Usiwaache wacheze mitaani au wacheze na Watoto waliowazidi Umri, usiwawekee movies zinazoonyesha mapenzi angalia sana kwenye TV yako,

Zaidi uwe makini sana kuwalinda sio na Wanaume tu hadi Wanawake.
 
Asante kwa ushauri,nimekulewa vizuri hasa hilo la kuwaweka free kuniambia lolote najitahidi sana,wanapokuwa katika hali ya kawaida wanakuwa huru tu,japo kama baba si unajua kuna muda wakifanya kosa lazima uwe mkali kidogo katika kujengana.

Hilo la kuitwa mchumba hata mimi sikubaliani nalo nimelichukua nitalifanyia kazi,maana ndipo mazoea yanajengeka taratibu hapo.

Pia nakubaliana kwamba ikitokea ameshikwa mwilini na mvulana na mwanaume akimbie au aripoti haraka

Kuna sehemu,Umezungumzia kwamba wakae mbali na jinsia ya kiume,hapa ndio sijaelewa maana unamaanisha kwamba wajitenge na wavulana au vipi?kumbuka wapo shule je inawezekana?

Pili umesena kama ana 8+ nimwambie kwamba hata kushikwa mkono na wanaume ambae si kaka au ndugu hapa naona kama nitamchanganya kumbuka shuleni wanakuwa wamefundishwa jinsi Ukimwi unavyoambukizwa.

Kwa mara nyingine nashukuru sana kwa ushauri wako na mawazo yako,zaidi nisadie kufafanua hapo nilipoonyesha mashaka
 
Asante hilo ni muhimu sana,kujenga trust ili awe muwazi kukueleza chochote,hii nadhani itasaidia kwamba kama kuna ukatili anafanyiwa asikae kimya lakini bado hujasema sasa unawaambiaje ili wakikutana na hawa wahalifu wajue wanafanya nini?
NO..NO..NO.,nimekuandikia hapo juu, ni lazima watoto wajue kusema NO, huu ni mwili wangu you have NO right to touch, mkuu soma to understand
 
Mtoto wa kike anfanyiwa ukatili hata na mlezi wake(baba wa jambo au mdogo wako wa dam kabisa). Suluhu la hapo ni kutoa elimu Kwa wanaume kupunguza masculinity. Pia wawe na adabu ya kukushirikisha kila mazingira hatarishi sio kukuogopa. Hilo litasaidia mno kuwajenga kujiamini.
 
Nimekuelewa mkuu ila mwanzo hukuelezea kwa undani,umesema tu wajue tu kusema NO
 
Mtoto wa kike anfanyiwa ukatili hata na mlezi wake(baba wa jambo au mdogo wako wa dam kabisa). Suluhu la hapo ni kutoa elimu Kwa wanaume kupunguza masculinity. Pia wawe na adabu ya kukushirikisha kila mazingira hatarishi sio kukuogopa. Hilo litasaidia mno kuwajenga kujiamini.
Ni kweli ila hapo umezungunzia wanaume waache masculinity ili watoto wawe huru kuwaeleza mazingira hatarishi.

Sasa hujaeleza je unamjengaje kwamba akitaka kufanyiwa ukatili afanye nini?
 
Watoto Kama una kipato make sure hawasomi Dumu fagio maana juzi NILIKUWA Temeke secondary .jamani watoto wanagegedana sijawai kuona Ni hatari Sana na wote wapo 14/15 yrs above!

Nadhani michezo michafu watoto wanaianziaga shule mainly katika hizi shule za dumu fagio
 
Ni kweli ila hapo umezungunzia wanaume waache masculinity ili watoto wawe huru kuwaeleza mazingira hatarishi.

Sasa hujaeleza je unamjengaje kwamba akitaka kufanyiwa ukatili afanye nini?
Mwambie Aina za mazingira hatarishi, sio kama anapendwa Sana Kwa kuambiwa anapendwa. Na asifikirie kuwa ni kweli akiambiwa ataolewa. Mwambie akiwa na mahitaj ya hela akwambie umpe, pia kuwa na tabia hii hata Kam hujaombwa.
Watoto wa kike wa umri wa binti yko vitu vyao vidogo vidogo tu chipsi na elf 5 tu. Mwambie apende kusoma na msimamie Hilo, akiwa na akili iliyoshiba ndo ataweza kufanya akuelewe vizur zaidi.
 
Asante hilo ni muhimu sana,kujenga trust ili awe muwazi kukueleza chochote,hii nadhani itasaidia kwamba kama kuna ukatili anafanyiwa asikae kimya lakini bado hujasema sasa unawaambiaje ili wakikutana na hawa wahalifu wajue wanafanya nini?
Kuna video moja Polisi anawafundisha watoto unyanyasaji wa kijinsia. Ameshika huku mbele alafu anasema Don't touch, alafu anshika nyuma anasema don't touch. Miye nimetumia ile video kuwaambia .tu asukuguse sehemu hizo wala kifuani sema Nooo. Na hizo sehemu nyingine don't touch. Umekuwa km wimbo hasa huyo mdogo ukimgusa tuu don't touch me.
 
Asante mkuu hio video naweza nikapata wapi?naona kama ni nzuri kupeleka ujumbe
 
Mwambie Aina za mazingira hatarishi, sio kama anapendwa Sana Kwa kuambiwa anapendwa. Na asifikirie kuwa ni kweli akiambiwa ataolewa. Mwambie akiwa na mahitaj ya hela akwambie umpe, pia kuwa na tabia hii hata Kam hujaombwa.
Watoto wa kike wa umri wa binti yko vitu vyao vidogo vidogo tu chipsi na elf 5 tu. Mwambie apende kusoma na msimamie Hilo, akiwa na akili iliyoshiba ndo ataweza kufanya akuelewe vizur zaidi.
Sawa mkuu umeeleweka,ushauri mzuri nitaufanyia kazi
 
Watoto Kama una kipato make sure hawasomi Dumu fagio maana juzi NILIKUWA Temeke secondary .jamani watoto sijawai kuona Ni hatari Sana na wote wapo 14/15 yrs above!
Mkuu wewe ulishuhudia wakifanya hayo kwa macho?hata hivyo Mkuu jamii wanakotoka hao wa shule za dumu fagio na hizi shule za Mabasi ni ileile tu tofauti ni kipato tu,ndio maana nikasema ukatili wa watoto hata walimu,madereva wa mabasi wanaweza wakafanya tu.

Halafu ni bora hata hao wako rika moja kuliko mtoto mdogo kufanyiwa uovu na mtu mzima.

Ndio maana nikasema tahadhari/elimu kwa mtoto ndio muhimu
 
Hivyo kwa wale wazazi au wataalamu wa saikolojia za watoto naomba ushauri, nitumie maneno gani yanayofaa kuwatahadharisha watoto wa kike darasa la tatu na chekechea namna ya kujilinda na ukatili wa kijinsia maeneo mbalimbali kwa kadri ya uelewa wao ili wawe salama?
Mtumie mama yao, mama mdogo au shangazi yao. Hao watatu ni wanawake wenzao hivyo haitakuwa na ukakasi sana kama ukiongea nao directly wewe kama mwanaume ambapo kwa desturi za Kiafrika lazima utahisi aibu/kigugumizi.
 
Back
Top Bottom