Nitumie dawa gani macho yangu kila siku jioni yanawasha sana (najikuna mpaka yanakuwa mekundu)

Nyanda lunduma

Senior Member
Apr 10, 2015
187
68
Habari wa jf,

Kama mada ilivyo hapo juu mimi kila ikifika jioni macho yangu huwa yanawasha sana yani najikuna sana mpaka macho yanakuwa mekundu, naombe msaada wenu nimetumia sana dawa mpaka Hospitali nimefika wakaniambia huenda nina aleji na kitu furani kila dawa wanayonipa haifanyi kazi.

Msaada kwenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii dawa ndo natumia
IMG_20200423_224425_1.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole. Kwanza nenda kwa eyes clinician akushauri uvae miwani mbayo ni transparent tu. Pili, zingatia kila macho yanapoanza kuwasha nawa maji mengi baridi safi na salama.

Jizuie sana kuyapikicha pale yanapowasha. Maana ukiyapikicha (blinking) yanapata michubuko ambapo yana attract enfections. Ukizingatia kunawa maji hata dawa hautatumia mkuu
 
Tafuta dawa yenye Mchanganyiko wa Antibiotic na Steroid.. Kama dexaneomycin then uone itakuwaje inaweza kuwa n8 infection sio allergy tu..
 
Usikae gizani.

Nina tatizo kama hilo nikiwa sehemu yenye mwanga mdogo. sometimes naendesha gari nikiwa nimewasha taa ya ndani
 
pole sana mkuu, kwa mawazo yangu nikushauri ufike hospitali wakakuchunguze waweze kujua unashida gani baada ya hapo utapata dawa stahiki japo dawa za macho na masikio zimekuwa ka aina moja na unaweza tumia ukawa sawa ila ni vema ukaenda chunguzwa zaidi kwaajili ya ustawi vema wa macho yako
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom