Uchaguzi 2020 Nitawashangaa CHADEMA kama watampitisha Tundu Lissu kuwa mgombea

Tambukareli

Member
May 8, 2020
26
75
Nitawashangaa CHADEMA kama watampitisha Tundu Lissu kuwa mgombea wao wa Urais

Sababu ni hizi;

Mosi, Tundu Lissu ni mgonjwa. Baada ya matatizo yaliyompata huyu ndugu yetu kule dodoma, uwezo wake wa kujenga hoja umeporomoka kwa kiasi kikubwa. I mean, Tundu lissu wa sasa ni tofauti kabisa na Tundu lissu wa kabla ya shambulio. Hii ni ishara kwamba Tundu hayuko sawa kiafya hasa afya ya akili, hivyo anahitaji matibabu zaidi ya kisaikolojia ili kumrudisha katika hali yake ya kawaida na siyo kumpa ridhaa ya kuwa mgombea Urais.

Kama CHADEMA wanataka Lisu kuwa mgombea wao, basi mwaka huu wampumzishe apatiwe matibabu na kumaliza msongo wa mawazo alionao aje ajipime ifikapo mwaka 2025.

Pili, Tundu lissu ni dikiteta. Baadhi ya watu wachache hudhania kuwa Rais magufuri ni dikiteta. Kiukweli hudhania hivyo kimakosa au labda kwakuwa hawajawahi kukaa na Tundu lissu wakajua tabia zake.

In fact, nchi hii hakuna dikiteta kama Tundu Lissu.

Lissu ni mtu wa mabavu, asiyekubali kushindwa na mwenye kujiona bora kuliko wengine. Kielelezo kizuri ni kipindi hiki cha mchakato wa uchaguzi ndani ya chama, yeye ata kabla ya kupitishwa na chama chake tayari ameanza kuitisha harambee ya kuchangiwa pesa za kampeni kana kwamba ameshajua kuwa yeye ndie bora na atakae pitishwa. Yote haya anafanya kinyume kabisa na taratibu za chama chake na ni mwendelezo wa matumizi ya mabavu na kujiona bora kuliko wengine.

Tatu, Tundu Lissu siyo mzalendo. Lissu ni muumini mkubwa wa siasa za unyang'au na utegemezi wa mabeberu badala ya siasa za ujamaa na kujitegemea. Katika hili, Lisu anakosa sifa za uzalendo na kukubali kuwa kibaraka wa mabeberu. Kielelezo kizuri ni pale alipojitokeza hadharani bila aibu na kuanza kuwatetea mabeberu Accacia katika mikataba mibovu ya kutuibia madini yetu.

Nne, Tundu lissu hana sifa za kuwa Rais. Lissu hawezi kuwa kiongozi bora kwa sababu hana busara, hekima na staha. Mara nyingi hufanya maamuzi kwa kukurupuka na kuhemka, vile vile ni msema hovyo.

Tano, Tundu Lissu ni mtu mwenye jazba na visasi. Ukisoma kwa umakini hotuba yake ya kuomba kuteuliwa kuwania Urais ndani ya chama chake, Lisu amejipambanua kuja kupambana na mtu (JPM) na siyo kutatua kero za wanachi watanzania. Katika hili, Lissu kwenye fikra zake anaamini waliomshambulia walitumwa na serikali hivyo anataka kugombea Urais kama njia ya kulipiza kisasi. Mtu kama huyu hafai kuwa Rais

CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani naamini ninyi mna hazina ya viongozi wazuri, Chagueni mtu sahihi, mzalendo mwenye kulipenda taifa lake apeperushe bendera yenu kwenye uchaguzi huu dhidi ya Rais mtetezi, kipenzi cha wanyonge Dr. Jonh pombe Magufuri

Asalaam aleykum
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
34,977
2,000
Yanga; Hii timu ya Simba kama inataka ushindi dhidi yetu sidhani kama inastahili kumpanga Meddie Kagere pale mbele. Kwanza huwa hajui kufunga, na uwezo wa kupiga Mpira vichwa hana kabisa. Yaani itakuwa hasara kubwa kumuweka hata benchi la akiba.

Simba; Pelekeni ujinga wenu huko, ebo!
 

Leonardo Harold

Senior Member
May 13, 2019
140
250
Hahahhaha nimekuelewa aisee. ..
Yanga; Hii timu ya Simba kama inataka ushindi dhidi yetu sidhani kama inastahili kumpanga Meddie Kagere pale mbele. Kwanza huwa hajui kufunga, na uwezo wa kupiga Mpira vichwa hana kabisa. Yaani itakuwa hasara kubwa kumuweka hata benchi la akiba.

Simba; Pelekeni ujinga wenu huko, ebo!
 

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
1,519
2,000
Lissu ni mtu wa mabavu, asiyekubali kushindwa na mwenye kujiona bora kuliko wengine. Kielelezo kizuri ni kipindi hiki cha mchakato wa uchaguzi ndani ya chama, yeye ata kabla ya kupitishwa na chama chake tayari ameanza kuitisha harambee ya kuchangiwa pesa za kampeni kana kwamba ameshajua kuwa yeye ndie bora na atakae pitishwa. Yote haya anafanya kinyume kabisa na taratibu za chama chake na ni mwendelezo wa matumizi ya mabavu na kujiona bora kuliko wengine.
Pointi

Lakini kuhuu kugombea na kupitishwa, waachie Tu wenyewe
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
5,602
2,000
Mbona mna mgwaya sana Lissu? Yaani hata akisimama diwani wa Chadema asimame na JPM tume ikiwa huru, Ccm wasipo saidiwa na wabeba mbeleko yenu. Dola, Ccm inaondoka madarakani.

Nimempenda sana Rais mpya wa Malawi kumuondolea Mutharika kinga. Tanzania tujifunze kitu hapo. Maana kuna makaburi mengine yana takiwa kuwekewa alama ili ukombozi wa kweli utakapo patikana Tanzania hao watu kama wamekufa washitakiwa wakiwa kuzimu.

Hamuwezi kumtandika mtu rissi za kutosha halafu mna leta utani, watu wana potea mnasema wame safiri.. Iko siku yaja..
 

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
4,549
2,000
CCM mnamwogopa Lissu sana naona hata policcm tayari wanamsubiri wamkamate uwanjani. Wataibuka wengine kujaza nafasi na CHADEMA ndio itakuwa maarufu zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom