Uchaguzi 2020 Nitatia nia Morogoro 2020

May 3, 2019
53
144
MOROGORO NYUMBANI.

Leo 08:30pm,19/09/2019.

Morogoro,Mji kasoro bahari,wenye mito inayotiririka masaa 24 na mabwawa makubwa lakini maji ni changamoto,umeme nao mita kadhaa kutoka mjini bado ni shida mfano Kasanga,kata ya Mindu.

Naamini onyo la Mh Waziri Mkuu kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro liende pia kwa watendaji wa Mkoa wa Morogoro,wanapaswa kuondolewa mara moja ili kuenda na kasi ya Rais Magufuli,

-Morogoro inapaswa kwenda inakopaswa kwenda Kiuchumi.

Toka enzi za Mbaraka Mwishehe wageni walifika toka kila kona kuja kusikiliza bendi ya Cuban Malimba iliyoongozwa vyema na nguli wa Muziki Tanzania,Mbaraka,Juma Kilaza na wengine wengi.

Kwa jiografia ya Mkoa wa Morogoro, wageni toka Zambia,Malawi,Msumbiji,Zimbabwe,Congo,Rwanda na Burundi wanapita katika Mkoa huo,palipaswa kuwa na shughuli za kibiashara,hata bandari kavu ilipaswa kuwepo hapo,na mzunguko wa pesa ulipaswa uwe mkubwa mahali hapo.

Mara baada tu ya Uhuru wa Tanzania mnamo mwaka 1962 Tanzania ilijipambanua kama nguli wa burudani Afrika Mashariki kutokana na harakati za kisiasa na mageuzi ya kitamaduni, kuzungumzia hayo Morogoro ndiyo mji uliokuwa kitovu cha burudani, wanamuziki nguli walikita kambi hapo na watu walikuwa wakitoka miji mikuu ijumaa kwenda kufuata burudani Morogoro na kurejea kazini jumatatu.

Umaarufu,uwepo wa viwanda vya kutosha kama tumbaku,Dimoni hapo miaka ya 1980 vilikuwepo zaidi ya 20,Morogoro ilipaswa iwe jiji kitambo sana.

-Mikumi,Udizungwa na Selous zipo ndani ya Mkoa wa Morogoro.

Eneo la Mkoa wa Morogoro liko katikati ya mikoa ya pwani ya Bahari Hindi na Nyanda za Juu.

Kuna tambarare za chini kama vile Ifakara / Kilombero, pia milima ya juu kama Uluguru penye mlima wa Kimhandu wenye 2646 m juu ya UB.

Mito mikubwa ni Wami na Ruvu inayoanza kwenye milima ya Uluguru. Ruvu ndiyo mto wa kutoa maji ya Daressalaam.

Karibu nusu ya eneo la Mkoa wa Morogoro ni hifadhi za wanyama za Mikumi na Udzungwa na sehemu ya eneo la kuwinda wanyama la Selous.

-Upendo na Ukarimu wa Wakazi wa Morogoro.

Kabila kubwa ni la Waluguru waliotoa jina kwa mji wa Morogoro pamoja na milima ya Uluguru.

Makabila mengine makubwa zaidi ni Wangulu, Wakagulu, Wasagala, Wapogolo, Wandamba, Wabena, Wambungu, Wakutu na Wavidunda.

Upande wa dini, karibu nusu ni Waislamu na nusu ni Wakristo.

-Morogoro kitovu cha Mawasiliano

Barabara Kuu za lami za Dar es Salaam - Morogoro - Mbeya - Zambia/Malawi na Daressalaam - Morogoro - Dodoma hupita eneo la mkoa pamoja na reli ya kati Dar es Salaam - Morogoro - Dodoma - Kigoma / Mwanza. Reli ya TAZARA hupita wilaya ya Kilombero.

-Nusu ya Uchumi wa Tanzania ungetokana na Kilimo Mkoani Morogoro.

Ardhi ya Morogoro ina takribani rutuba ya kufaa kwa mazao mengi. Lakini kilimo kinategemea hali ya mvua.

Karibu nusu ya eneo la mashamba yote hulimwa mahindi.

-Mazao ya sokoni hulimwa milimani.

Mkoa wa Morogoro ni eneo lililojaliwa na Mungu kwa uzalishaji wa sukari kwa wingi. Hasa Wilaya ya Kilombero ina mashamba makubwa ya miwa.

#Mimi ni,Msemakweli Chakubanga.
Nyumbani Morogoro.
0755078854.
 
Hivi kwann watu wanaamini Maendeleo huletwa na watia nia kama wewe?

Maendeleo ni falsafa, Maendeleo ni Mipango, Maendeleo ni mtambuka

Maendeleo hayaletwi na Mtu, Maendeleo huletwa na watu au Jamii ya watu walioamua wenyewe.

Kitu kibaya zaidi Maendeleo ni Mtazamo, yaani unachokiona au kukiita Maendeleo sio Lazima kiwe Maendeleo kwa mwenzako.

Kwa dhana hiyo hakuna Mtu au Jamii iliyoendelea ukilinganisha na mtu au jamii nyingine.

Isipokuwa kila mtu au jamii huyaona na kuyatafsiri Maendeleo kwa muono wake.

Asante
 
Back
Top Bottom