NITASHAWISHIKA WANANCHI WAKIRUDISHIWA NGUVU NA HESHIMA YAO.

Omulangi

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
1,036
265
Mengi yanaendelea katika mitandao na katika vyombo vya habari. Dalili zinaonyesha watu wanasisimuliwa na hatua mbali mbali za serkali mpya. Ukweli ni kuwa watawala wanatumia nguvu zao na vyombo vyote vya dola kuwatetea na kuwasaidia wananchi huku wakiwawajibisha wasiojituma.

Hatua hii imeanza kupongezwa toka kila kona. Vyombo vile vile vilivyokuwa vikitumiwa vibaya na wasio itakia mema nchi kuitafuna na kufunika au kunyamazisha yeyote anayehoji ulaji au uzembe katika mikono mibovu, sasa inaonekana vimeelekezwa katika kukata mizizi ya uovu kwa walaji waliojikinai na wasiojali wananchi waliowekwa kuwatumikia. Hadi hapo inaonekana kama matumaini mapya yanatokea.

Mimi napenda nieleze mashaka yangu. Kumbe vyombo na nyezo zilizo katika mikono ya watawala wetu zinaweza kutumiwa vibaya kama uongozi ukiwa legelege au kama ni mbovu. Lakini vyombo vile vile vikalazimishwa kufanya kazi ya manufaa mikononi mwa viongozi wema wenye mzigo na mapenzi mema nchi ikafurahi. Polisi ile ile, wizara zile zile, uhamiaji ile ile, mahakama zile zile, mamlaka zile zile. Hapo ndio nashtuka, kumbe vyombo vyetu havina shida!!! Shida kubwa imo katika mioyo ya watawala. Wale wanaokamata usukani.

Leo tunampata mwema, mambo yanabadilika. Je kesho ikiwa bahati mbaya tukampata mbovu au kama waliopita itakuwaje? Tutarudi huko huko na pengine pabaya zaidi. Hivyo tunachohitaji si mtu mzuri wa kushika vyombo hivi, tunahitaji utaratibu utakaoendesha vyombo vyetu kwa manufaa ya wananchi na si vinginevyo. Tunahitaji vyombo hivi uthibiti wake usitegemee mtu anayeingia. Tunahitaji utaratibu, kanuni na sheria zitakazomfanya mtu mbaya akose namna ya kutumia vyombo hivi vibaya. Tunahitaji utaratibu utakaowaweka wananchi kwenye usukani. Yaani yatakayofanywa na vyombo hivi yawanufaishe wananchi. Yatakayofanywa na vyombo hivi yawawajibishe viongozi kwa wananchi. Mikataba itakayofungwa ifahamike vizuri na wananchi. Si kwa huruma ya watawala bali kwa nguvu ya sheria na miongozi inayowabana watawala kuwa wazi.

Mtu atakaye leta mabadiliko ya ukweli awe yule atakayewarudishia wananchi meno yao na watawala wakaogopa kuwakosea na kuwajibishwa. (Hatutaki mtu wa kusema nawasaidia wananchi, tunataka mtu wa kusema nawatumikia wananchi. Mtu atakayesema naogopa wananchi wanaweza kukasirika wakaniwajibisha). Hapa lazima tufikiri vizuri je tumeshampata mtu wa aina hiyo au bado?? Je kuna anayetengeneza utaratibu wa kurudisha madaraka na nguvu kwa wananchi. Je yuko anayeamini katika demokrasia ambayo ni utawala wa watu. Yuko anayejenga nguvu ya wananchi kufanya maamuzi na kuwa na sauti katika nchi yao? Au ni mipango tu ya kuwaamulia wananchi na kufifisha sauti na uwezo wao wa kukubali au kukataa jambo? Je mifumo iliyopo inajenga ujasiri na heshima kwa wananchi kiasi cha kuwahoji na kuwatetemesha watawala? Je watawala wanakubali mifumo inayoweza kuwaongezea wananchi nguvu na kupunguza nguvu za watawala juu yao?

Leo yawezekana mifumo na sheria na kanuni zilizopo zinruhusu mtu mmoja kuzitumia akatusaidia? Lakini swali langu ni je ikiwa tunasaidiwa na kuhudumiwa kwa huruma tu ya mwenye nguvu za maamuzi na madaraka yasiyo na ukomo, siku akiingia mtu mbovu asiye na huruma nguvu hizo si atazitumia kutuhujumu na kutunyamazisha na kututesa!!! Haya ndiyo mashaka yangu.
 
Demokrasia ya kweli waachie wazungu, Usitegemee kuiona Afrika. Unapoteza muda kufikiria hivyo!
 
Rasim ya pili ya warioba inahusu hapa. Ccm walijifanya kichwamaji wakaichakachua live live. Sasa Jpm kama ana uchungu kweli na nchi hii, ajivue ganda jeusi asimamie ukweli wote uliomo katika rasim ya pili.

Vinginevyo hiyo itabakia ndoto, yeo akiwepo rais juha, nchi inaenda kama punda mgojwa
 
Demokrasia ya kweli waachie wazungu, Usitegemee kuiona Afrika. Unapoteza muda kufikiria hivyo!
Demokrasia inaweza kupatikanika popote pale, baada ya miaka 10 to 15 years tutaiona Africa. Kwani jinsi watu wengi wanavyozidi kupata elimu kuhusu haki zao na uchumi kukuwa itawalazimi viongozi kubadili tabia. Na katiba vile vile itabadilishwa tu. kwa sasa CCM wana buy time lakini wanajua wawawezi kuendelea hivi hivi bila mabadiliko ya katiba.
 
Demokrasia inaweza kupatikanika popote pale, baada ya miaka 10 to 15 years tutaiona Africa. Kwani jinsi watu wengi wanavyozidi kupata elimu kuhusu haki zao na uchumi kukuwa itawalazimi viongozi kubadili tabia. Na katiba vile vile itabadilishwa tu. kwa sasa CCM wana buy time lakini wanajua wawawezi kuendelea hivi hivi bila mabadiliko ya katiba.
Sawa, ngoja tuone.
 
Back
Top Bottom