Nitashangaa wakikosa mikopo

Evvy jr

Senior Member
Apr 23, 2017
148
188
Nitashangaa wakikosa mikopo - Rais Magufuli
Friday , 27th Oct , 2017
Na Gerald Kitalima

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa atashangaa sana endapo wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wanastahili kupata mikopo watafungua vyuo na kukosa mikopo hiyo.

Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu Oktoba 27, 2017 na kusema yeye toka tarehe 29 ya mwezi uliopita alikuwa ameidhinisha fedha hizo za mikopo zaidi ya bilioni 145 hivyo anategemea wanafunzi wakifungua vyuo vikuu watapata fedha hizo.

"Toka mwezi uliopita kwenye tarehe 29 nilipitisha bilioni 147 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wanaostahili kupata mikopo, nitashangaa sana kama kutakuwepo na wanafunzi wapo kwenye orodha ya kupata mikopo na mikopo watakuwa hawajapata mpaka wanafungua vyuo, mimi najua nimeshaidhinisha hizo fedha sitapenda kuona wanafunzi wanafungua vyuo na kuanza kuteseka wakati fedha zipo" alisisitiza Rais Magufuli

Vyuo Vikuu nchini Tanzania vinategemewa kufunguliwa mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu kutokana na ratiba iliyotangazwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU)
 
The President's statement is still ambiguous,kuna watu wengi wana vigezo vya kupata mkopo Lakini Hata kwenye list za HESLB majina yao hayajaonekena na bado vyuo vinafunguliwa wiki kesho achilia mbali hawa ambao majina yao yameonekana kwenye list na Wenda wakafika vyuoni wasikute fedha kwa akaunti zao. Je wenye vigezo ni wale waliochaguliwa tiyari au hata wale ambao hawajchaguliwa na hawatachaguliwa kabisa?, maana list iliyobaki ni ndogo na watu ambao hawajapata ni wengi kwa kuzingatia jinsi wanavyotoa majina.Na wakikosa mkurugenzi wa Bodi ya mikopo ana kesi ya kujibu.....yangu masikio na macho tu....
 
Mbona sielewi sielewi hapa badru anasema bil 108 magu bil 147 Heslb Kuna jipu limeiva ...Mr president andaa pini tu dadadeki
 
Back
Top Bottom