Nitarudi tena nchini Kenya

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,708
Kwanza kabisa niwape pole wale wote waliosongwa na shida za dunia kiasi kwamba hawajui la kufanya zaidi ya kukodoa macho na kupiga miayo isiyojulikana itakwisha lini!

Pili,niwape pole wale wote ambao tangu mwaka huu unaanza mpaka sasa hawajui ni lipi la kufanya kwasababu hali si shwari mtaani.

Tatu,niwape pole vijana wote waliohitimu, shule na vyuo na bado wameendelea kuwa mizigo majumbani kwao huku wakiendelea kusimangwa usiku na mchana, Mungu atawasimamia.

Nne,niwape pole wale wote tuliojiwekea malengo tokea mwaka huu unaanza lakini mpaka sasa hata robo ya malengo hatujatimiza!.

Tano na mwisho,niwape pole wale wote wanao haso lakini maisha yameendelea kuwa kichwa ngumu huku wakitamani kufanya ushirikina ili yalegee! Msikate tamaa ndugu zangu,Mungu amewasikia vilio vyenu!


Namshukuru Mungu mwaka huu nilibahatika kwenda nchi jirani ya Kenya kwa ajili ya kumuona jamaa fulani kwa shughuli za kibiashara, hapo kabla sikuwahi kabisa kufika nchini Kenya, hivyo nilikuwa nasikia na kusoma makala za watu mbalimbali wakitoa maoni yao kuhusu nchi ya Kenya katika nyanja mbalimbali.

Safari yangu ilianzia mkoani Dodoma na kujikuta nimepiga kambi ya masaa kadhaa wilayani Tarime pale kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania yaani Sirari,ingawa wenzetu wao wanaita "Sirare",Sababu ya kuzuiliwa masaa kadhaa pale Sirari ilikuwa ni kwamba sikuwa na pasi ya kusafiria(passport),hivyo nilitakiwa nirudi mpaka Tarime mjini kwa mkuu wa wilaya(bomani)kwenye ofisi za uhamiaji ili nikate pasipoti ya muda ili niweze kuruhusiwa kusafiri.

Baada ya kufika pale Tarime kwenye ofisi za Uhamiaji niliwakuta vijana wenzangu wakiwa ofisini wakiendelea kuchapa kazi,ingawa pia kuna vijana niliwakuta wameshikiliwa pale ofisini ikisemekana walikuwa wametokea burundi na walikamatwa kwa kuwa hawakuwa na documents zilizowafanya kuingia Tanzania.

Wakati pia nikiwa hapo ofisini huku jamaa wakiendelea kunikamilishia pasipoti yangu ya muda,kuna dada mmoja (demu) ambaye alikuja na jamaa mmoja hivi alikuwa mweupe kama mpemba,yule demu baadae wale jamaa waliniambia ni mkenya na wanamfahamu sana pale ofisini kwasababu haikuwa mara ya kwanza yeye kukanyaga pale akiwa na wanaume kadhaa wa kadhaa,kuna jamaa aliniambia yule demu ni muuzaji wa Kambale (nadhani tunaelewa), yule demu kiukweli niwe mkweli alikuwa pisi ya kimataifa,kama ukiwa na uchu na unahamu na kambale wabichi,basi kununua kambale kwa bei ya milioni ilikuwa ni jambo la kawaida!

Kwasababu mimi ni mtu mzima, inavyoonekana ni kwamba, yule demu huwa ametegesha pale Tarime na nadhani madereva mbalimbali ikiwemo wa malori huwa wanapeana namba za yule kiumbe,hivyo ukifika tu hapo Tarime kama unazo namba zake basi unamcheki mnavuka boda mnaenda kufurahia Ugali "Sima" kwa kambale mkiwa upande wa pili.Kiukweli Mungu alimuumba vyema sana yule mwanamke na anazo nyama za kutosha,bastola ndiyo usiseme!!.

Basi nilipokamilishiwa pasipoti yangu niliondoka zangu hapo ofisini nikawaacha huyo demu na jamaa yake nao wakiendelea kukamilisha documents zao.

Nilirudi tena Sirari nikagongewa muhuri ili nipite zangu kuingia Kenya, mpaka nakamilisha process zote na kuingia Kenya ilikuwa yapata saa 11 jioni.

Nilipofika upande wa pili,niliamua kubadili fedha yetu ya Tanzania na kupata shilingi ya Kenya, hapo sasa nikiwa eneo la Isebania. Nilipanda gari ndogo zilizokuwa zinaelekea sehemu moja inaitwa Migori, ingawa nilipokuwa naelekea ni Kisumu,lakini mwenyeji wangu aliniambia nikalale Migori ili nipumzike.

Basi nilipanda gari ndogo aina ya Toyota Pro box ambavyo vilikuwa vingi sana hapo Isebania. Isebania ni sehemu ya County ya Migori.

Nikiwa ndani ya gari niliendelea kuishangaa Isebania ilivyonakishiwa na nyumba za zamani kando kando ya barabara, kiukweli hapo Isebania kiujumla hali haikuwa tofauti sana na kwetu upande wa Tarime maana hata wenyeji wa Isebania pia ni wakurya lakini wakurya wa Kenya.

Ilitichukua takribani saa 1 mpaka kufika Migori. Kiukweli baada ya kufika sasa Migori ndipo niliona hali ni tofauti kwasababu Mwanzo nikiwa Isebania hali ya hewa na mazingira hazikupishana sana na Tarime, lakini kuanzia hapo Migori na kuendelea hali ya hewa na Mazingira yalianza kubadilika na kuwa yakupendeza sana.

Nilienda kutafuta chumba cha kulala ambapo nililipa Ksh 1000,kiukweli wenzetu kwenye suala la Lodge,Guests House bado naona wako nyuma sana, na ninasema hivyo kwasababu kuanzia hapo Migori mpaka nilipoishia (nitasema huko mbele), bado rooms hazikuwa vyema, yaani Guests ni gharama lakini haziendani na thamani ya pesa, kuna mtu nilimuuliza akaniambia wakenya si watu wa kwenda Guest sana ndiyo maana huwa hawajali, lakini nikajiuliza kwanini wasiweke mazingira bora kwasababu ya wageni?

Jamaa akaniambia logde hizi za kawaida huwa si nzuri tofauti na zile za kitalii, sasa hiyo Ksh 1000 niliyolipa ambayo kwa Tanzania ni kama 22000/= kiukweli hata ukiamua kulala pale Dodoma unapata Guests house nzuri sana.


Nitarudi kuendelea
 
Siti ya pili hapa na popcorn kabisa kucheki move

IMG_20210830_203748.jpg
 
Wadau wa story za NITARUDI aub ITAENDELEA hawaashtukia hii kitu au heading haijakaa kuwavuta waje!.
 
Yaani huu uzi ukisema umerud bila kula kambare wa kisumu utakuwa hujatuwakilisha vyema mkuu.
 
Kwa jinsi ulivyomwelezea dada Kwa mapana na kumsifia hivyo matumaini kuna mwendelezo Naina yake na wewe..nipo hapa nasubiri!!
 
Tuendelee



Basi nilichukua lodge jioni hiyo kwa ajili ya kupumzika,wakati huo hapo Migori kulikuwa na hali ya hewa ya kawaida sana na hakukuwa na baridi japo mazingira yalionyesha ni mji wa baridi,nadhani ilikuwa kipindi cha joto.

Niliendelea kukaa nje ya ile lodge huku nikitazama mazingira ya Migori namna yalovyovutia,kiukweli pale Migori ndipo sasa nilianza kuwaona wanawake wazuri kiasili wenye type ya lupita Nyong'o,ile county ya Migori imejazwa na wenyeji ambao ni waluo(JALUO),jamani labda tu niwaambie ya kwamba,kama hujabahatika kufika Kenya hebu nenda tu ukatembee halafu utaleta hapa majibu kwa maana mimi mwenzenu nilibaki nawashangaa wale wanawake wa kiluo pale Migori,siyo kwamba Tanzania hatuna wanawake wazuri,la hasha!,nadiriki kusema ya kwamba Tanzania tunao wanawake wazuri ila kiukweli naona kama wenzetu wamebarikiwa kuwa na wanawake wazuri.

Kwanza,ni wanawake warefu kwenda juu,pili wamejaaliwa nyama za kutosha,tatu ni wazuri wa asili ambao wana rangi moja tu ambayo ni nyeusi(black),nilipoenda huko ndipo nikafahamu ya kwamba Tanzania ndiyo nchi pekee afrika mashariki ambayo wanawake wake(si wote bali wengi) wana rangi mbili.
Wenzetu wao rangi yao ni moja tu!,sikubahatika kumuona mwanamke mweupe hapo Migori na kama walikuwepo basi ni weupe wa kuzaliwa nao!!,Siyo kama huku kwetu mwanamke anazaliwa mweusi lakini akienda you-dsm au you-dom anarudi amekuwa mweupe.


Sasa kuna kitu kilinishangaza sana ambacho nilijaribu kuwauliza wenyeji ili kupata majibu.Nilipofika hapo Migori karibia kila mwanamke niliyekuwa nikimuona alikuwa amevaa mini sketi(ki/vi-mini),sasa kumbe wenyeji wao walishazoea ile hali na wanaona ni kawaida tu!,mimi niliyetoka nchi ambayo kila mwanaume akipishana na mwanamke mwenye shepu matata lazima ageuze shingo,kiukweli nilipata taabu!,pia hata jamaa yangu aliniambia biashara ya nguo za kike hasa mini sketi kule zinalipa sana na soko ni kubwa,hivyo kama unasoma uzi huu na una mtaji wa kutosha hebu fanya biashara ya nguo za kike na peleka huko,kuhusu wenyeji mimi nitakupatia namba za wenyeji kadhaa ambazo ninazo na utajenga urafiki ili uone wapi pa kuanzia.

Asubuhi palipokucha niliamka nikaingia kwenye mgahawa mmoja ulikuwa jirani na hapo lodge nilipolala kwenda kupata chai ya strungi!,ile nimeingia ndani nikakutana na jamaa wamevaa magwanda ya kijeshi kama wote huku wakinitazama,sasa kumbe wale jamaa walikuwa ni askari na hao askari wa kikenya ndivyo wanavyovaa,ile lodge kumbe ilikuwa jirani na kituo cha polisi kikuu cha hapo migori na huo mgahawa ndiyo huwa sehemu yao ya kupata vifungua vinywa!,basi sikuwa na wasiwasi kwasababu niliingia Kenya kihalali,bahati nzuri hakuna aliyenighasi!.

Nilipomaliza kunywa strungi nililipa nikaondoka zangu kuelekea stage(stendi ya bus),sasa wenzetu vituo vya magari wanaita "stage" na siyo "stendi" kama tulivyozoea huku kwetu.Pia kule hakuna ma-bus makubwa kama huku kwetu,kule wanatumia Hiace ambazo wanaziita "shuttle" au "matatuu".
Basi nililipa nauli kutoka hapo Migori kuelekea Kisumu ambapo ni Ksh 600,kutoka hapo Migori mpaka Kisumu ni takribani masaa 3,hizo shuttle zikiisha jaza hapo stage(stendi)zinaondoka na kwenye gari hakuna mtu anayeitwa Konda(kondakta),huu utaratibu niliupenda sana,natamani tujitahidi na huku kwetu ungekuwepo.

Wakati nikiwa kwenye gari jamani uongo dhambi,mimi nilikuwa nikiwashangaa wanawake tu wanavyopita wakiwa ndani ya vi-mini huku wakitepesha nyama zilizoshikilia makalio yenye haja(Lazima nirudi Kenya).
Ndugu zangu watanzania,nilichojifunza hapo Migori ni kwamba,wakenya wanapiga kazi na wala siyo mchezo,hawana muda wa kupiga stori na mtu,nilikuwa nikiangalia sehemu ambazo bodaboda wanapaki lazima utakuta kuna vibanda vizuri ambavyo vimejengwa kwa ajili ya kuwasitiri kwenye mvua na jua,siyo kama Tanzania bodaboda wanaishi kama majambazi kutwa kufukuzana na polisi barabarani.

Safari ya kuelekea Kisumu ilianza sasa,nashukuru Mungu nilikaa siti ya mbele ya ile Shuttle,hivyo nilikuwa naangalia mandhari nzuri ya ile miji niliyopita,Kuanzia pale migori kuelekea Kisumu sikuona kitu kinachoitwa "Nyumba ya nyasi",narudia tena kuanzia pale Migori mpaka Kisumu sikuona nyumba ya nyasi,nyumba za tope zipo nyingi sana lakini huwezi kukuta zimeezekwa kwa nyasi,nyumba zote hata kama niza tope zilikuwa zimeezekwa kwa nyasi!,nilimuuliza dereva wa ile shuttle akaniambia kwamba " Huku kwetu kuezeka nyumba kwa nyasi ni ishara ya laana,hivyo hakuna mluo anataka laana kwenye boma yake".

Hayo ndiyo maneno aliyoniambia dereva wa ile shuttle,pia aliendelea kuniambia kwamba,bei ya bati Kenya ni nafuu sana ambayo kila mwananchi anaweza kuimudu na ndiyo maana huwezi kuona nyumba ya nyasi,ndugu zangu kwa ambao wamefika huko wanaweza wakaweka hapa shuhuda hizi ninazo zisema.

Kuhusu barabara kiukweli ndipo nilifahamu viongozi wetu wanatutania watanzania,ile barabara ya kutokea Migori kwenda Kisumu ilikuwa ni pana sana kiasi kwamba ukii-compare na barabara ya morogoro Road inayoanzia kibaha,basi inaingia mara moja na nusu kwa ukubwa.Ule mji wa Migori kiuhalisia unaizidi miji mingi tu hapa Tanzania kwa uzuri.
Tulitembea kwa umbali mrefu huku nikiendelea kushangaa mandhari nzuri za ile nchi,nilichobaini pia kule mtandao wa simu wenye nguvu ni Safaricom,mitandao ipo mingi lakini huwezi kuona ikiwa imetapakaa kama huku kwetu,Safaricom niliambiwa kule ndiyo kila kitu na wananchi wanaupenda sana kwasababu una huduma za uhakika,siyo kama huku kwetu ma-mitandao ni mengi lakini kila siku wananchi wanalalamika kuhusu huduma mbovu na serikali ikiwa inakodoa macho tu isijue cha kufanya!
Pia nilikuta mavazi yenye nembo ya "WCB WASAFI" yanavaliwa kama njugu,bado sijajua hawa watu wa wasafi kama wanalifahamu hili jambo ama la!,yaani vijana karibia wote niliyokutana nao basi lazima utakuta kavaa shati au sweta lenye nembo ya "WCB WASAFI",mimi kuhusu mavazi pia nahitaji nirudi huko kuanzisha hiyo biashara na wala sijachelewa maana jamaa aliniambia nguo huko zinalipa sana hasa za kike!,ndugu zangu mnaofanya kazi ya kuuzia dada zetu nguo nzuri hapo Mwenge hebu ingieni kule mkajionee na mtanipa mrejesho,msiendelee kulalamika biashara imekuwa ngumu wakati wenzetu wanauhaba wa mavazi mazuri!!,kuhusu mtu wa kuwapokea nitawapatieni mawasiliano!.

Pia wakati tukiwa njiani tunaelekea kisumu sikuona ma-bar kabisa,siyo kwamba wao hawanywi pombe,la hasha!,wanakunywa sana ila jamaa aliniambia kwa kule ma-bar yanapaswa yawe ndani siyo nje!!,nikawa najiuliza hebu anzia pale kibaha maili moja kama unaelekea mjini Daslam umejionea ma-bar mangapi barabarani,yawezekana hata yakawa zaidi ya 10000,sasa hiyo kitu huwezi kuikuta kule!.

Kilichonishangaza zaidi ni kutokuona kabisa mabango ya "dawa za kuongeza nguvu za kiume",narudia tena huwezi kuona!!,Jamaa aliniambia ukiona hilo bango mahali,basi tambua kuna mjanja katokea bongo kapeleka utapeli huko,lakini wao hawana huo muda wa kubandika mabango ya dawa za kuongeza nguvu za kiume kwasababu ni mashababi ki-kweli kweli(kuna kisa nilikishuhudia Kisumu usiku nitakieleza vizuri,hapo ndipo nikagundua jamaa kweli ni mashababi kwasababu yule mwanamke asingeokolewa na meneja wa ile lodge jamaa alikuwa anamuua kwa mkuyenge)


Nitarudi baadae kidogo
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom