Nitapata wapi generator nzuri ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nitapata wapi generator nzuri ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbwambo, Jul 13, 2011.

 1. M

  Mbwambo JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Wapendwa, nimechoka na kero za kukatika umeme kila mara. Nimeamua kutafuta generator japo napo ninatafuta makelele ya mngurumo wake.
  Je nitapata wapi generator nzuri kwa kijihela changu cha laki 4? Yaani 400,000/=.

  Vitu vyangu ni vya kawaida: fridge 2, taa kama 13 hivi, microwave, tv set, pasi 2, etc.
  je kwa hela kama hiyo nitapata generator?. Aina gani ndio nzuri?

  Nisaidieni waungwana
   
 2. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,826
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  Wadau wa majenereta tunawasubiri mtumwagie mautaalam,teh teh teh!
   
 3. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,292
  Likes Received: 2,369
  Trophy Points: 280
  Nenda Kariakoo, mtaa wa uhuru, karibu na ile petrol station ya total,ilo dukaliko opp na na icho kituo cha mafuta.

  Kwa laki 4, unapata generator nzuri kabisa.
   
 4. M

  Mbwambo JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  asante kaka yangu , nitakwenda hapo kariakoo karibu na petrol station ya total. Asante na ubarikiwe
   
 5. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  naomba mnaotumia generators mtufunze ni capacity gani inahitajika kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya nyumbani, yani kuwasha freezer, taa za vyumbani, tv na computer.
   
 6. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Achana na zi-jenerator ndogondogo zitachoma na kuunguza vifaa vyako. jenereta nzuri kwa maana hiyo hazipatikani Tanzania. wachuuzi wetu wanaleta bidhaa duni kutokana na uwezo wetu wa kutonunua vifaa ghali na vyenye ubora.
  Ungelikuwa na kama $2000 ningelikushauri utumie solar na inverter ya 5000watts ingelitosha kwa usalama wa vifaa vyako na kubana matumizi. Panel za solar zinadumu zaidi ya miaka ishirini na tano na betri hudumu si chini ya miaka mitano. hesabu za LUKU na MAFUTA YA GENERATOR sidhani kama zitakuwa na uwiano na za solar.
  Matumizi ya generator ni makubwa mno kwani ikiwa inabana matumizi ya mafuta kama wanavyosema utatumia kwa uchache lita tano kwa masaa kumi na nane!!!!!!!!!!!!! Aidha unaweza kujibana na kutumia lita 2-3 kwa siku kutokana na uchache wa vifaa utakavyotumia. lakini ukiongeza vifaa ndipo balaa la mafuta linapokuja!!

  Ila jitahidi upate jenereta za Honda au YANMAR 3500 zinaweza kukufaa. (kuwa makini katika kusoma majina -uchakachaji ni mwingi unaweza kukuta inasomwa KHONDA au YMYMAR)
   
 7. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,292
  Likes Received: 2,369
  Trophy Points: 280
  Ni kweli umeme wa solar (Solar Energy Businesses in Tanzania). (Rex Investment Limited - Tanzania's leading solar energy contractor - Rex donates solar system to Kerege orphanage) ni bora kuliko jenereta ya laki 4.

  Tatizo ni ku raise io hela (2.5m-3m). Kwa wengine sio rahisi, pale wanapoamua na kuwa na uhakika wa kupata hizo hela.

  Jenereta ni nzuri na itakusaidia kwa wakati wa emmergency, hasa kama ukiiwasha kwa 3 au 4 tu. kwa siku.
   
 8. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,059
  Likes Received: 7,279
  Trophy Points: 280
  Je vipi substitute ya inverter?
  Nimeambiwa kuna za mpaka laki 2 kisha nikaongezea laki 1.2 ya betri, ni kweli?
  zinadumu na chaji kwa muda siku ngapi?
  durability yake ikoje? wapi nitapata nzuri?
  Tusaidiane tu jaman kukabiliana na huu mgao wa Giza-nesco!!
   
 9. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,292
  Likes Received: 2,369
  Trophy Points: 280
  Inventer nazo sio mbaya, hata zile za kutengeneza, ila kama ujuavyo, zinaweza kudumu na zinaweza kubuma.

  Jirani hapa bunju b anatumia io, anachofanya ni kuichaji betri ya inventer mara 2 au 1 kwa wiki.

  Umeme wake sio mkali ila kuondoa giza kwa kuwasha taa tu utaweza, na itategemea inakupa watts ngapi ili uweze hata kuwasha ka feni au tv.

  Wapi utapata hapo kasheshe, maana mafundi wako kibao, na siku kuna kautapeli tapeli kwenye swala hilo, ndio, kama mafundi seremala, utazungushwa na kupigwa tarehe, mpaka uipate ujue na urafiki na hata hamu ya io inventer itakuisha!

  Uliza uliza kwa ndugu na marafiki, za dukani sina uhakika kwa hela yako.

  Durability, hakuna guarantee mkuu, swala ni kwenda na reputation ya huyo fundi.
   
 10. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,059
  Likes Received: 7,279
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana mkuu, ukweli umejitahidi kuelezea na nimekupata vizuri,Ila ukweli pia umezidi kunichanganya sana. Maana hata naogopa tena kwenda kununua.Kwa maelezo yako zinahitaji imani zaidi kuliko uhalisia wake.Yaani ukimbiwa ni ya watt 500 inabidi uamin tu
   
 11. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Kaulizieni Tanesco maana wanawakatia umeme ili wakubwa wauze majenereta. Kwahiyo watakuwa na data za kutosha sababu wana wataalam pia!
   
 12. M

  Mbwambo JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  hapo umenena mkuu, ni muhimu wataalamu watufahamishe capacity gani inatosha kwa mfano wa vitu nilivyosema?
   
Loading...