Nitapata wapi chapisho la kitaaluma la Dkt. Joseph Pombe Magufuli

Shebbydo

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
1,174
1,937
Habari wakuu

Ni kawaida ya wasomi kutoa machapisho mbalimbali ya kitaaluma katika fani walizobobea. Mimi nimekuwa interested na kusoma machapisho ya Mh. Rais wetu ya kemia kama nikiyapata. Lakini kwa bahati mbaya nimepekuwa huku na kule sijapata chochote. Yeyote ambaye anaweza nielekeza andiko la Mheshimiwa naweza lipata wapi anisaidie.

Ni hayo tu wakuu.
 
Hivi pale mlimani machapisho haya ni public record?
Nataka kwenda kuona andishi la udaktari laMheshimiwa Sana
 
Inawezekana JPM akawa na machapisho machache, au bado hajachapisha...Ninavyoelewa mimi mara nyingi (siyo rule lakini) hapa Tanzania wenye machapisho ni Lecturers au professors ambao kupanda kwao cheo kitaaluma pia huzingatia idadi ya machapisho..JPM hajawahi kufundisha Chuo Kikuu chochote hapa Tanzania au nje hivyo siyo rahisi kuwa na machapisho...lakini ni kweli pia kuwa, kuwa na machapisho siyo lazima uwe lecturer au profesa.
 
Thesis zipo pale mlimani maktaba kuu, kama sikosei sehemu ya periodicals. Kama sio member wa udsm nadhani bado unaweza kuingia pale kwa kibali. Department ya kemia pia watakuwa na kopi.

Magufuli, J.P.J., 2009. The potential of anacardic acid self-assembled monolayers from cashew nut shell liquid as corrosion protection coatings. Ph.D. Thesis, University of Dar es Salaam, Tanzania.

Ila kama unaongelea journal publications, sina uhakika kama ni lazima pale udsm uwe ume-publish ili upate PhD. Kama ni optional, nadhani ilikuwa ngumu kwake, ukizingatia kwamba amesoma hiyo Ph.D akiwa waziri wa wizara ngumu ya Ujenzi!
 
Inawezekana JPM akawa na machapisho machache, au bado hajachapisha...Ninavyoelewa mimi mara nyingi (siyo rule lakini) hapa Tanzania wenye machapisho ni Lecturers au professors ambao kupanda kwao cheo kitaaluma pia huzingatia idadi ya machapisho..JPM hajawahi kufundisha Chuo Kikuu chochote hapa Tanzania au nje hivyo siyo rahisi kuwa na machapisho...lakini ni kweli pia kuwa, kuwa na machapisho siyo lazima uwe lecturer au profesa.
Labda sasa akiwa prezidaa atafanya kama alivyofanya mwenzake Obama:
US Health Care Reform: Progress and Next Steps
 
Sadam Huseein ni rais wa kuwait....qwi qwi qwiqwi nacheka kwa dharau.....

andiko??? my foot! ukilipata uniitee nami aisee!

Huyo magufuli ni mkemia, muulize mambo ya Chemical formula, Salicilics, anatase, hemihydrates nk. Mambo ya raisi wa Oman anaitwa nani hata chekechea wanaweza, sio issue. Angalia huyu mtoto wa 2 years anaweza kutaja maraisi wa nchi karibu zote Africa.

Nina uhakika wewe huwezi. Kama ni issue, unajilinganishaje na huyo mtoto?
 
Back
Top Bottom