Nitapambana na mafisadi hadi kifo

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Mama Kilango, hutakuwa pekee yako katika mapambano hayo dhidi ya mafisadi. Watanzania tutashirikiana nawe bega kwa bega katika vita dhidi ya mafisadi mpaka wote washughulikiwe na mkono wa sheria.

Posted Date::4/28/2008
Kilango: Nitapambana na mafisadi hadi kifo

Na Daniel Mjema, Same
Mwananchi

MBUNGE wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela(CCM) ameapa kupambana kwa nguvu zake zote na viongozi mafisadi ndani ya Serikali hata kama kwa kufanya hivyo kutagharimu maisha yake.

Kilango alitoa kauli hiyo juzi nyumbani kwake Kijiji cha Uzambara wakati akijibu swali la mwandishi wa Mwananchi ikiwa hahofii maisha yake kutokana na msimamo mkali aliouonyesha katika mikutano ya 10 na 11 ya Bunge.

Katika mikutano yote hiyo miwili, Bunge lilipitisha maamuzi mazito na ya kihistoria likiwamo lile lililomlazimisha Edward Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu kutokana na kuhusishwa na kashfa ya kampuni ya Richmond.

Mbunge Kilango ni mmoja kati ya wabunge wachache wa CCM ambao wamejitoa mhanga na kuonekana kuwa msumari wa moto kwa viongozi wanaotuhumiwa kutumia vibaya nyadhifa zao kujitjirisha.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kijijini kwake, alisema siku zote katika jambo lolote analolifanya anamtanguliza Mungu na kwa kuwa anatetea maslahi ya nchi, haogopi kufa.

"Hata kama nikifa leo au kuuawa kwa sababu ya Richmond au suala lolote la kitaifa lenye maslahi ya kweli ya wananchi basi wajue kuwa atatokea Anne Kilango mwingine kuendeleza pale nilipokomea," alisema.

Alisema kati ya mambo yanayomchukiza katika maisha yake ni kuona watu waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali za nchi kwa manufaa ya wananchi wanazitumia isivyo ili kujineemesha.

Alisema haoni mantiki ya Mtanzania mzalendo kuhifadhi fedha zake katika mabenki ya nje badala ya kujivunia benki za nchini kwake.

"Fedha hizi kama zingewekwa katika benki zetu zingesaidia kuinua uchumi kwa mabenki yetu kuzikopesha na mzunguko wa faida wa mikopo hiyo ungeendelea kubakia nchini," alisisitiza Kilango.

Kilango aliwaomba Watanzania wawe wavumilivu, kwani Rais Jakaya Kikwete hivi sasa ana kazi kubwa ya kusafisha uovu uliofanywa na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tatu.

Mbunge huyo alitolea mfano wa mikataba mibovu ya madini, mikataba ya kufua umeme ambayo wawekezaji wanalipwa hata kama hawajazalisha, Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na mkataba wa kampuni ya TICTS.
 
Mama Malecela,

You are my hero! Give 'em boyz mafisadi a run for their illegal money. Tuko nawe na utapata support ya wapenda haki wa jambo na watanzania wote wanaofisadiwa day in night out.
 
Yap mama. Midume Bungeni imo inasubiri posho tu haifanyi lolote, vitambi vikubwa kama nini kazi kupiga makofi tu. Amkeni nanyi this is another Tanzania men.

Bravo mama Marechela
 
I cant believe JK was meant to be mgeni rasmi kwenye ule mkutano wa Diaspora, na kuwekeza nyumbani ilkuwa ni one of the main topics! Sasa kweli tunakuwa encouraged kuleta vijisents vyetu huko wakati viongozi wetu wanavuna mabilioni na kuyatoreshea nje?
On the other hand, I think wakati wa kupeana uwaziri kwa kujuana umepitwa na nyakati. Its really important kabla mtu yoyote hajapewa uwaziri awe vetted kabla ya kutangazwa, ikibidi hata interpol wawe involved. JK would have known everything about Chenge na wengine if he had wanted to know.I still dont know why watu kama huyu Mama au Dr Mwakyembe hawapewi uwaziri!!!
 
She has already done a very wonderful job but she can do well her job while she is still in chama cha mapinduzi. SHE IS IRON LADY
 
Wasi wasi wangu wabunge wazuri kama huyu mama katika kutetea maslahi ya nchi hupewa uwaziri na ikishatokea hivyo basi inabidi afuate mstari wa serikali.

JK tunakuomba Mama Kilango usimpe uwaziri mwache bungeni ili arudishe imani ya wananchi kwa bunge letu. Labda yeye na Kimaro watakuwa mfano kwa wabunge wengine na wao kuanza kutetea maslahi ya Tanzania badala ya yale ya CCM.
 
Sidhani kama JK atampa huyu mama uwaziri. Fuatilia uone watu wanaopewa uwaziri na JK - nchimbi, malima, mkullo na wengineo ujue JK ni mtu wa namna gani wakati wa kuteua mawaziri.
 
Sidhani kama JK atampa huyu mama uwaziri. Fuatilia uone watu wanaopewa uwaziri na JK - nchimbi, malima, mkullo na wengineo ujue JK ni mtu wa namna gani wakati wa kuteua mawaziri.

Hey MWK, You never know!
 
Hey MWK, You never know!

Kweli kabisa na ninakubalia na lile ombi lako kuwa Mama Malecela asiwe waziri maana akishaingia huko kwenye hiyo timu ya kifisadi atalazimika kutetea ufisadi.

Hata hivyo kulingana na watu ambao naona JK anateua kuwa mawaziri kwenye serikali yake, sidhani kama atafanya hivyo.

Anyway, time will tell!
 
Mama kilango anatuzuga,tunajua kinachoendelea, watanzania mtakumbuka siku ile akimshambulia

Lowasa, akasema,"sitakubali Zito ndiyo aikosoe serikali yangu" unadhani ni kwanini alisema hivyo? hii yote ni kwa sababu ccm wameshaona watanzania tumegutuka.

Kama kweli yeye anachukizwa na ufisadi wa CCM basi ajiuzuru toka ktk chama chake
 
Mama kilango anatuzuga,tunajua kinachoendelea, watanzania mtakumbuka siku ile akimshambulia

Lowasa, akasema,"sitakubali Zito ndiyo aikosoe serikali yangu" unadhani ni kwanini alisema hivyo? hii yote ni kwa sababu ccm wameshaona watanzania tumegutuka.

Kama kweli yeye anachukizwa na ufisadi wa CCM basi ajiuzuru toka ktk chama chake

Haya aliyasema lini na wapi?
 
Mama Kilango kweli anahitaji watu wote wampe tafu. lakini napenda kumuliza mama kilango yeye na hao wabunge wote wa CCM
walikuwa wapi kwa muda wote huo mambo hadi yamefikia hatua mbaya kiasi hiki ndo wanajaribu kupaza sauti?

Walifikiri ufisadi unawaangamiza wapinzani peke yao na familia zao na jamaa zao tu. huu ni mwanzo si kila waziri au mbunge au kiongozi wa ngazi yoyote ile wa CCM ana maisha mazuri. Hadi hapo wabunge wote wa CCM watakapoamka toka kwenye ndoto zao na waachane kabisa na itikadi zao za chama ndiyo mabadiliko ya kweli ya kiuchumi yataonekana.

Kama wataendelea kuwa watu wa kupitisha tu mambo hakika moto huu utatula na kutumaliza wote. At least sasa wameanza kuona na kugundua kwamba kumbe matabaka baina hata ya wao kwa wao ni makubwa mno. Wao wabunge wa CCM ndiyo waliochangia kwa haya yote kufikia hapo mambo yalipo kwa sasa. Ole wenu amkeni haraka na kwa kishindo.​
 
wewe maisha ya ccm,iko kwa maslai yake tu....chenge ni mtu gani,msabaha ni mtu gani,kigoma malima ni mtu gani? je lowassa ni mttu gani,,,,+ticts karamagi anatisha ni nani!!!! wanashindana na mengi au nani!!ccm inanuka
 
Nakubaliana na quote ya hapo juu kuhusu mama Kilango. Kweli siku ile ya kujiuzulu kwa waziri mkuu alisema hawezi kuwaachia akina zito ndiyo waikosoe serikali. huyu mama anaonyesha bado anadhani kwa moyo wake kabisa kwamba watu wa upinzani hawapaswi kupata credit yoyote kwa lolote walisemalo juu ya utendaji mbovu wa serikali ya JK. kwa mawazo yake tunaweza kukumbuka maneno hayati Nyerere aliyomwambia mrema wakati wa uchaguzi wa 95 akisema hawezi kuiacha nchi mdomoni kwa mijibwa. nyerere hakuamini kuna mpinzani aliyekuwa na hekima au sifa ya kuliongoza taifa hili. hali hiyo ndiyo hiyo bado wana CCM wanafikiri liko hivyo hivyo. Wamepotea tena sana. wako wapi hao wa CCM wenye kuweza? si wote Mafisadi toka juu kabisa hadi chini , na chini hadi juu? sisi wananchi tunawaambia bado kitambo kidogo na watakiona, kama wanataka watu waingie msituni hilo mbona halina shaka hata kidogo wasifikiri wataweza kuuzima moto kwa silaha walizokuwa nazo. tunasema bado kitambo kidogo tu wasipoongeza kasi ya wao kuuelezea uma wanachokijua basi na wasitie shaka bado kitambo kidogo ole wao.
 
Thanx M/Kike but subsidizing wouldnt solve the long standing people's mayhem. the only solution JK and his government needs to do amicably is to dissolve all this horrible and horrifying contract Tanesco entered with all these unscrupulous power companies. this is were all the Tanesco revenue is being sent think of IPTL, Songas, Aggreco, Dowans, Richmond and now Tan Power. siphoning 29 bl every month from Tanesco coffers. Jamani what is this. then tunaambiwa wanataka kuwapa Tanesco trillion + kwa ajili ya kimarisha tanesco. that means that money is also going to pay outstang debts Tanesco has with those dubious power companies. wavunje hiyo mikataba yote na power bills will naturally come down. after roll kwa nini wazalishe umeme waiuzie Tanesco? kwa nini wasizalishe na wasambaze wenyewe kwa kujenga infrustructure zao wenyewe? na kama watatumia Tanesco infrustructure wailipe Tanesco wao wanajua kuzalisha tu na kuunganisha kwenye national Grid. let them inccur costs, hicho wanakikwepa. they want quick and easy money then Tanesco ndo aanze kuhangaika kupeleka umeme huku na huko wao wakisubiri tu malipo yao ya kila siku. this is sickening. Shame on them all.
 
Mwakyembe,kimaro na Mama Malecela inabidi wasipewe uwaziri ili wawe kama watch dogs kwa wengine.
Usishangae watu kama hao wakipewa uwazili majukumu yanawazidi then utakuta wako kimya.
Izi changamoto za apa na pale tutazikosa bungeni.
Mwakyembe,kimaro na mama yetu keep it up,God is behind your efforts as well as JF
 
Mama Sitta alikuwa vivyo hivyo wakati akiwa Rais wa Chama Cha walimu Tanzania, lakini alipopewa Uwaziri tu, mambo yakabadilika. Naomba huyu mama naye asiwe anatafuta madaraka tu!!
 
Hivi Mzee Chrisant Maliyatanga Mzindakaya yupo wapi siku hizi?

Tunahitaji backbenchers wazuri na wengi zaidi..si vema akina Mwakyembe, Seleli, Anne Kilango n.k. wakawa mawaziri. Inawezekana pia si watendaji wazuri wakiwa mawaziri..
 
Back
Top Bottom