BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,098
Mama Kilango, hutakuwa pekee yako katika mapambano hayo dhidi ya mafisadi. Watanzania tutashirikiana nawe bega kwa bega katika vita dhidi ya mafisadi mpaka wote washughulikiwe na mkono wa sheria.
Posted Date::4/28/2008
Kilango: Nitapambana na mafisadi hadi kifo
Na Daniel Mjema, Same
Mwananchi
MBUNGE wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela(CCM) ameapa kupambana kwa nguvu zake zote na viongozi mafisadi ndani ya Serikali hata kama kwa kufanya hivyo kutagharimu maisha yake.
Kilango alitoa kauli hiyo juzi nyumbani kwake Kijiji cha Uzambara wakati akijibu swali la mwandishi wa Mwananchi ikiwa hahofii maisha yake kutokana na msimamo mkali aliouonyesha katika mikutano ya 10 na 11 ya Bunge.
Katika mikutano yote hiyo miwili, Bunge lilipitisha maamuzi mazito na ya kihistoria likiwamo lile lililomlazimisha Edward Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu kutokana na kuhusishwa na kashfa ya kampuni ya Richmond.
Mbunge Kilango ni mmoja kati ya wabunge wachache wa CCM ambao wamejitoa mhanga na kuonekana kuwa msumari wa moto kwa viongozi wanaotuhumiwa kutumia vibaya nyadhifa zao kujitjirisha.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kijijini kwake, alisema siku zote katika jambo lolote analolifanya anamtanguliza Mungu na kwa kuwa anatetea maslahi ya nchi, haogopi kufa.
"Hata kama nikifa leo au kuuawa kwa sababu ya Richmond au suala lolote la kitaifa lenye maslahi ya kweli ya wananchi basi wajue kuwa atatokea Anne Kilango mwingine kuendeleza pale nilipokomea," alisema.
Alisema kati ya mambo yanayomchukiza katika maisha yake ni kuona watu waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali za nchi kwa manufaa ya wananchi wanazitumia isivyo ili kujineemesha.
Alisema haoni mantiki ya Mtanzania mzalendo kuhifadhi fedha zake katika mabenki ya nje badala ya kujivunia benki za nchini kwake.
"Fedha hizi kama zingewekwa katika benki zetu zingesaidia kuinua uchumi kwa mabenki yetu kuzikopesha na mzunguko wa faida wa mikopo hiyo ungeendelea kubakia nchini," alisisitiza Kilango.
Kilango aliwaomba Watanzania wawe wavumilivu, kwani Rais Jakaya Kikwete hivi sasa ana kazi kubwa ya kusafisha uovu uliofanywa na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tatu.
Mbunge huyo alitolea mfano wa mikataba mibovu ya madini, mikataba ya kufua umeme ambayo wawekezaji wanalipwa hata kama hawajazalisha, Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na mkataba wa kampuni ya TICTS.