Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Kaimu Katibu Idara ya Hamasa, Sera, Utafiti na Mawasiliano UVCCM TAIFA, Ndugu Abubakar D. Asenga. akizungumza na Vijana wa CCM.
Vijana wa CCM tunataka maelezo ya kina juu ya waliotusaliti wakati mgumu wa kampeni kwa kuama chama? eti sasa wanarudi, ILI iweje?
Chama hiki si cha mtu, eeh kama katiba na kanuni tubadili tu, jambo la kupokelewa watu hawa liamuliwe na vikao vikubwa si Kata ama Wilaya tu, watu wakipewa Milioni.
KWANINI MNASAHAU MACHOZI YA WAPAMBANAJI HASA VIJANA MAPEMA HIVI? AMA KWAKUWA SISI TUMESHAPATA VYEO?
MTAKUJA KUTUONA WATUKUTU NA JEURI SASA HIVI.
Eti Mteketa karudi!
Nasikia yupo Waziri Mkuu Mstaafu anatakakurudi!
Nasikia Mzee Ngombale anataka kurudi!
Nasikia Mzee Msindai,Mgeja na Guninita wanarudi!
NITAONGOZA MGOMO WA VIJANA HAMASA WA CCM NCHI NZIMA endapo wasaliti wanarudi bila vijana kupewa maelezo ya kina na kushirikishwa, Haikubaliki.
Ehh Maana watu watasaliti tu wakijuwa wakirudi kwa kutoa Milioni moja watapokelewa.
TUACHE BESENGA HAMKAWII KUSEMA SISI WATUKUTU NA JEURI. Maana hakuna namna.
Chanzo: UVCCM Taifa