Nitampongeza Rais Magufuli kwa hili.

Joshua Hagai

Senior Member
Jul 8, 2015
111
20
Rais anajitahidi japo mimi sikumchagua ila nawezakiri anajita kwa upande wake.
Kupambana na makundi ya kimafia yaliyokita mizizi ndani ya taifa ni kazi ngumu sana.

Kwani makundi haya yameshika na kuitawala misingi ya kiuchumi na kisiasa ya taifa letu.
Kuing'oa misingi hii ya wadhulumaji na wanyang'anyi Rais anahitaji juhudi kubwa kutoka kwa jamii hasa maombi na ushirikiano wa kimawazo.

Rais Magufuli ni wajibu wako kuing'oa misingi hiyo kwani waasisi ni mfumo uliokuweka wewe madarakani.

Matatizo yote ya taifa hili yameasisi na CCM na wakudhulumiwa ni ninyi.

Endapo utarejesha rasimu ya pili katiba nitakupongeza na kukuona wewe kuwa mzalendo wa kweli kwa taifa hili.
Siwezi kukupongeza kwa sasa kwani bado sijaona hilo.

Rais anayezingatia na kuyaheshimu maoni ya wananchi wake ni rais bora.
Rais turudishie maoni yetu wananchi tutakupongeza na kukuona wewe shujaa.

Weka mbele maslahi ya taifa la watanzania wote,na maslahi ya chama baadae.
Taifa kwanza,Wazalendo tutakupongeza.

TUNAKUOMBEA.
 
Wewe Rasimu ile inapigiwa makelele ni kwaniaba ya kutawala Na si mengineyo
wengine wameona ndio kick ya kutokea kisiasa
 
Back
Top Bottom