Uchaguzi 2020 Nitampigia Kura mgombea urais yeyote atakaejieleza kwa ufasaha kuhusu fao la kujitoa NSSF

Fortilo

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
4,722
14,247
Ndugu zangu wasalam,

Mimi ni mwajiriwa kwenye sekta binafsi na nimeanza kuchanigia NSSF tangu mwaka 2011, akiba yangu ni kati ya Mil 60-75, japo kuna kipindi nilijitoa nilipohama kampuni, muda si mrefu nataka niache kazi nijikite kwenye kufanya kazi zangu binafsi.

Kinachonisikitisha ni kauli za kwamba sheria ya mafao kwa sasa hairuhusu kujitoa, hadi nifikishe umri wa miaka 55, au ili niqualify unit 180 au michango ya miaka 15.

Mimi binafsi naona kama ni ukoloni mamboleo, mimi sikwenda kazini kukua.

Rafiki zangu wahindi, wazungu na foreigner wengi, yani hata wakenya tu hapo niliwahi fanya nao kazi wao wakiwa wanaondoka wanadai chao na wanalipwa bila makato wala wasiwasi wowote.

Mfanyakazi mwezangu Mkenya amekosa kibali karudi kwao Kenya na 100M, Mhindi kaondoka na 250M sisi Watanzania ndio tunaambiwa hadi tufikishe miaka 55.

Yule Mkenya kafungua biashara zake kaniambia sisi Watanzania tunaumizana wenyewe kwa wenyewe, yani imeniuma mno.

Sasa nikifikiria wanasiasa hasa wabunge wanalipwa hela zao CASH 200+ M wanapomaliza huduma ya miaka 5, mimi naambiwa lazima nifikishe 55.

Kuna kipindi Kigwangala alisema kwanini usitunze mwenyewe unasubiri serikali ikutunzie, swali kwake, pengine hajui chochote kuhusu kuajiriwa na kukatwa 10% ya salary kila mwezi, isitoshe pamoja na maneno yake mengi kaishia kuja kuomba pikipiki kwa mo, kwani mili 200 ni boda boda ngapi bei ya jumla China?

Sasa turudi kwenye hoja za kutumia hela zetu

1. Ujenzi wa miradi ya maendeleo kama chuo kikuu Dodoma, Soko la Karume na daraja la kigamboni, hivi wanafunzi si wanalipa ada. daraja linalipwa na watumiaji, soko na wafanyabishara, iweje bado hela zishikiliwe kwa kisingizio cha miradi kutokurejesha hela.

2. Miradi ya maendeleo inachangiwa na kodi zangu, kwanini nichangie mara mbili, kuna haja gani ya kutoa huduma bure ambazo kama nchi hatuna uwezo nazo tusifanye sharing na wananchi wa kima cha chini.

3. Wabunge wanaliokopeshwa hela za NSSF wamerejesha? Kama hapana wamepewa kama zawadi? Sasa kwanini Wafanyakazi tusikopeshwe na sisi kama ilivyo kwa wanasiasa, mbona SACCOS na VICOBA wanaendesha kwa faida na wanapewa gawio, hapo Kwenye mifuko shida nini.

4. Miradi inayoitwa ya hovyo na uwekezaji usio na mantiki, kwanini kipaumbele cha wapangaji isiwe wachangiaji wa mifuko, yani hata nyumba za bei nafuu?

5. Kuna upekee gani wa mfuko kukaa na hela ya mwanachama kwa zaidi ya miaka 20 then uje umlipe kiasi kile kile alichochangia bila percentage increase ikizingatiwa kuwa thamani ya pesa huisha kutokana na muda (Monetary value depriciate over time)

Narudia tena nitampigia kura mgombea urais yeyote atakae ongelea suala hili kwa ufasaha, kura ni maslahi binafsi.

Best,
PM
 
Umegonga mule mule mzeya. Tena katika hiki kipindi cha corona walitakiwa wawape watu hela kutoka kwenye michanga yao kwa wale ambao walifutwa kazi ama mambo hayakuwa shwari.

Kusubiri mpaka 55 kwani nina mkataba na muumba? Na pia wanaposema watu wajiajiri sasa ndio capital hiyo mtu kajiwekea mpe akafanye yake
 
Poor daddy,unawaza nssf tu?,mkipewa za mkupuo mnaolea hovyo ,kunywa pombe hovyo na starehe zisizo na maana ,kisha mnaanza kuilaumu serikali haiwajali ,pathetic
 
Ndugu zangu wasalam,

Mimi ni mwajiriwa kwenye sekta binafsi na nimeanza kuchanigia NSSF tangu mwaka 2011, akiba yangu ni kati ya Mil 60-75, japo kuna kipindi nilijitoa nilipohama kampuni, muda si mrefu nataka niache kazi nijikite kwenye kufanya kazi zangu binafsi...
Unataka kuwa muhujumu uchumi?

Hi nchi haitaki watu wake wawe na maisha mazuri
 
Kwenye ilani yetu CHADEMA tumesema tukiingia madarakani tutafanya marekebisho ya sheria ya hifadhi ya jamii na mifuko ya hifadhi ya jamii ili kurejesha fao la kujitoa.

Ilani yetu imeenda mbali zaidi kwa kufuta kikokotoo nyonyaji ambacho kitaanza kutumika January 2021.
 
Poor daddy, unawaza nssf tu? mkipewa za mkupuo mnaolea hovyo, kunywa pombe hovyo na starehe zisizo na maana, kisha mnaanza kuilaumu serikali haiwajali, pathetic
Kwahiyo mkuu hata serikali ingebidi itupangie matumizi ya mishahara sio?

Sipingi kuwa na hizo akiba kwa ajili ya uzeeni, lakini unadhani ni sahihi kuja kumlipa mtu 33% ya total accumulation at 55 years?
 
Poor daddy,unawaza nssf tu?,mkipewa za mkupuo mnaolea hovyo ,kunywa pombe hovyo na starehe zisizo na maana ,kisha mnaanza kuilaumu serikali haiwajali ,pathetic
Wewe dada,unaopopangiwa ununue nini kwa ajili ya kuwapikia mabosi zako,usitake kuwapangia Watanzania namna ya kutumia pesa zao.
Endelea na u Hg wako.
 
1602495182258.png
 
Back
Top Bottom