Uchaguzi 2020 Nitamchagua tena Dkt. Magufuli kwa sababu hizi...

Kila nikiangalia, mahesabu yangu yananiambia kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 MAGUFULI anapigwa asubuhi na mapema tu

1. Kura za Kaskazini zitamkataa vibaya mno
2. Kura za kusini zitamkataa katakata
3. Kura za Waislamu ndiyo kabisaa maana teuzi zake nyingi wamezilalamikia
4.Kura za mji mikubwa kama Mbeya na Dar es salaam atazisikia katika bomba
5.Kura za Singida kwa Tundu Lissu na Nyalandu hizo asahau
6.Kura za wafanyakazi ambao hajawaongezea nyongeza za mishahara atazisikia katika bomba
7. Kura za Vijana wasio na ajira, Vijana wa vyuoni wanamwangalia wanasema hiiiiiii etc
8.Kura za Watanzania walioko kwenye social media wengi hawamkubali
9. Iringa atapigwa asubuhi na mapema tu
10.Kagera ndiyo kabisa wanasubiri wapitishe hukumu
11. Kule Kigoma kwa Mwami Zitto ndo asahau kabisa
12. Wafanyabiashara wanaosumbuliwa kodi na TRA wamenyuti hawana maneno mengi wanamsubiri kwa hamu wamsulubu
13. Wenye Magari waliogeuzwa ng'ombe wa kukamuliwa pesa na Matrafiki hawa wanamgojea kwa hamu kubwa wamuonyeshe kilichomnyoa kanga manyoya
Dar umeona picha leo hakuna mtu amehangaika na huyo mtu wako mpaka jioni sasa unapasemaje dar?
 
Wewe ni machinga, wewe huyo huyo mama ntilie, mara mjamzito hahaha! Kazi kweli kweli
 
Miaka hamsini ya Uhuru kuna mtu anakuja kushukuru eti selikali imeweka umeme kwa bei nafuu, ,hivi unajua mpka leo kuna vijiji havina zahanati kuna vijiji havina maji ya uhakika,kuna vijiji huo umeme haujafika alafu kukmbua umeme WA rea ni msaada uliofadhiliwa na mashirika ya nje kipindi cha kikweteeeeeeeeeee, Tanzania ina vyanzo kama vinne vya umeme lkn mpka leo umeme bei juu sana ,Zanzibar wanatumia umeme WA Tanzania lkn kule wametoa kodi kwenye sukari Zanzibar sukali kilo sh 1600 ongea vitu vya msingi

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Tuelewane vizuri hapa, tusilazimishane. Sisi tulioguswa na JPM tutamchagua tena Oktoba 28.
Na kwa ambao hawakuguswa pia tusilazimishane...kama unampenda, kanywe naye chai. Hata hivyo kwa nafasi ya Urais ataiota tu kwani tayari ina mtu sahihi. Zinduka ndugu yangu achana na zilipendwa, zama za washamba na limbukeni zimepita hiyo, wahi uungane na Tanzania mpya, Tanzania yenye uongozi unaoheshimu, unaotetea na unaolinda uhuru, haki na maendeleo ya watu. Amka kijana, hii ni karne ya 21, achana na tawala za imla, zisizo na busara wala hekima...ohooo, shauri yako!
 
Inashangaza kuona watu kama hawa wanakubali Nchi yetu iwe kama South Africa ya makaburu ambayo raia walikuwa wananyanyaswa, kudhalilishwa, kubaguliwa, kutekwa, kuteswa, kupotezwa na hata kuuawa. Mtu mwenye kauli kama hizi na matendo maovu mengi tu anastahili vipi kuendelea kuwepo madarakani!?

Kwanini tuchague uovu na uminywaji wa uhuru na haki badala ya kuchagua UHURU NA HAKI ya raia na vyombo vya habari ambavyo siku zote huinua Taifa na kuleta upendo, furaha na mshikamano!?

LadyRed chagua UHURU NA HAKI kwa raia pia kwa vyombo vya habari ili tuweze kuhoji bila woga wa kutekwa, kupotezwa au kubambikiwa kesi. HAKI NA UHURU HUINUA TAIFA.



Nimesoma
Nikabaki nasema tu heeeee heheheeeeee
 
Chagua uendelee kuwa masikini
 

Attachments

  • Screenshot_20201006_222500.jpg
    Screenshot_20201006_222500.jpg
    43.8 KB · Views: 1
Serikali ya Chama Cha Mafisadi (CCM) ni muasisi na kinara wa ufisadi hapa nchini Tanzania. Hiki chama na serikali yake hawawezi kupambana na ufisadi kamwe. Mapambano dhidi ya ufisadi kwa CCM ni sawa na mkosaji kujiadhibu mwenyewe, jambo ambalo katika hali halisi, haliwezekani katu. Uliona wapi nyani anajizuia kula mahindi ya mkulima? Nyani wamezoea kula mahindi ya mkulima kiasi kwamba mkulima akiwafukuza au kuwaua wasimalize mahindi yake, watamuona kama anawaonea bure! Wanadhani kula mahindi wasiyoyalima ni haki yao ya msingi au ya kuzaliwa.

Jinsi ambavyo wanakula mahindi ya mkulima, vivyo hivyo CCM na serikali yake wamezoea kufisidi mali za umma kiasi kwamba inakuwa vigumu kwao kuwasikiliza wale wazalendo wanaowakataza au kuwashauri waachane na ufisadi. Wanadhani kwamba kufisidi mali za umma ama ni haki yao ya msingi au ni haki yao ya kuzaliwa! Hapo ndipo serikali ya kifisadi ya chama cha mapinduzi ilipotufikisha.

Na kama ambavyo ili mkulima ajiepusha na nyani anapaswa kuwaua au kuwafukuzilia mbali nyani, vivyo hivyo kwa chama cha mafisadi na serikali yake, ili kuepukana na ufisadi wao, hatuna budi kuwapiga chini mwaka huu wa 2020. Hii ndiyo njia rahisi na sahihi ya kupambana dhidi ya ufisadi. Huwezi kuitenganisha CCM na ufisadi. UFISADI na CCM ni kama kuku na yai. Ili upate yai sharti ufuge kuku; na ili upate kuku sharti uwe na mayai ya kutotolea vifaranga ambao wakishakomaa huwa kuku. Hivyo basi, ili kuepuka mayai (yanayotoa kuku), huna budi kuwachinja kuku wote na kuwafanya kitoweo. Vivyo hivyo, huwezi kupambana na ufisadi kikamilifu bila kuwang’oa CCM kutoka madarakani. Tukifanikiwa kuwang’oa CCM madarakani tutakuwa tumeumaliza ufisadi nchini.

Ndugu watanzania tukicheka na nyani (CCM) tutavuna mabua (umasikini). Hima wananchi tujitambue ili tusiendelee kunyonywa na kupe hawa wasioshiba kamwe. Tuwaulie mbali. Vinginevyo, itakula kwetu na hatutakuwa na mtu wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu sisi wenyewe kwa kutofanya maamuzi sahihi ya kuwafutilia mbali CCM kutoka kwenye utawala wa chi hii. Wazungu wana msemo mmoja usemao, “If a peron decieves you once, shame on him; if twice, shame on you”. Tafsiri isiyo rasimi ya maneno haya ni kuwa. “Ikiwa mtu atakudanganya mara moja, aibu iwe kwake; lakini ikiwa mtu huyo huyo atakudanganya mara ya pili, aibu na iwe kwako”. Ikiwa utakubali kudanganyika mara ya pili, basi akili zako hazina akili!

Ndugu wananchi wapenda maendeleo, Chama Cha Majambazi (CCM) wamekuwa wakitudanganya miaka nenda miaka rudi lakini hatujifunzi kutokana na makosa yetu ya nyuma; matokeo yake tumekuwa tukiwarejesha madarakani kila Uchaguzi Mkuu uitishwapo. Ndugu zangu tutajifunza lini? Mbona tunakuwa na akili kama za kuku wa kienyeji au punda?

Kuku wa kienyeji hupenda kuchakura mwenyewe vichakani kutafuta chakula bila kuhitaji uangalizi wa mfugaji. Ukiwafungia kuku wa kienyeji bandani, ukawaweka kwenye mazingira tulivu chini ya kivuli, na ukawapa chakula na maji tele, watakudharau sana. Watakuona kama unawaonea kwa kuwafungia ndani na kuwapa chakula chenye virutubisho vyote, badala ya kuwaachia wajitafutie wenyewe chakula duni walichokizoea huko kwenye vichaka.

Punda daima hupenda kubeba mizigo mizito. Ikitokea Bwana (master) akambebesha punda mzigo mwepesi, humdharau sana na kumuona kama hampendi. Anadhani kubebeshwa mizigo mizito ni haki yake ya kuzaliwa. Ukimbebesha punda mzigo mwepesi halafu ukakatiza karibu yake, hakawii kukupiga mateke ili kuashiria kwamba hajaipenda tabia yako mbaya ya kumbembesha mzigo mwepesi. Atakuchukia na kukuona humtakii mema katika harakati zake za kubeba mizigo mizito kupindukia.

Nadharia hizi mbili zinaelekea kufanana na namna ya maisha ambayo watanzania wamechagua kuishi. Watanzania wamezoea kuishi maisha ya dhiki na taabu kama ambavyo punda na kuku wa kienyeji wamezoea kuishi kwa kuchakura na kubeba mizigo mizito mtawalia (respectively). Chama Cha Magamba (CCM) kimefanikiwa kuwafukarisha watanzania kwa zaidi ya miaka 50 sasa! Pamoja na ufukara wote ambao chama hiki kimeusababisha, bado wananchi wamekuwa wanakiunga mkono na kukifanya kiendelee kubaki madarakani mpaka leo. Ni lini watanzania tutafunguka macho na kuzibuka masikio na hatimaye kuacha kuchagua maisha ya utumwa chini ya CCM na serikali yake?

Ndugu zangu, saa ya ukombozi ni sasa. Naomba tujitambue na tujisahihishe; tujutie na tutubu makosa kwa kuendelea kumkubatia huyu shetani, ibilisi mtoa roho (CCM). Tutafungwa nira na kubebeshwa mizigo mizito na huyu shetani mpaka lini? Hebu tuitue mizigo yetu chini tukimbilie kwa Mkombozi (CHADEMA) ili tupate kupona. Dhambi ya kukubali kufungwa nira na kuchapwa mijeledi kama punda na huyu ibilisi (CCM) itatugharimu uhai wetu na vizazi vyetu sawia. Tubadilikeni ndugu zangu. Tusikubali kufungwa nira tena mwaka 2015. Tukatae kutumiwa na CCM kama ngazi ya kuning’inia madarakani.

Nimetumia hii logic rahisi ili hata wale ambao hawakwenda shule (wanaCCM) wanielewe barabara. Kwa hiyo, wito unatolewa kwa wananchi wote kuwang’olea mbali CCM, kupitia sanduku la kura tarehe 28/10/2020. Sote tukiungana kwa pamoja bila kujali rangi, kabila, jinsia wala dini zetu, tutawafuta hawa kupe kutoka kwenye uso wa ardhi ya Tanzania. Kumbuka kwamba njia nzuri ya kupambana na kupe ni kumnyima chakula (damu) kwa kuwaweka mifugo mbali na kupe. Kuna baadhi ya kupe ambao wamekuwa sugu, hata uwapulizie dawa kali kiasi gani hawafi. Na hawa kupe (maCCM) walishakuwa sugu. Huwezi kupambana nao kwa kuwashitaki mahakamani kwa kuwa wameishakuwa sugu wa mahakama. Njia nzuri ya kupambana nao ni kuwanyima ulaji (uongozi) kama vile ambavyo kupe wakinyimwa damu hujifia kwa njaa! Kumbuka kwamba hawa kupe wamekuwa madarakani kwa zaidi ya nusu karne (zaidi ya miaka 50) lakini tukitazama maendeleo waliyoyaleta katika nchi hii hayalingani na maendeleo waaliyoyaleta MABEBERU wa kikoloni.

Ndugu watanzania, kwa hiyo mifano michache nadhani mtakuwa mmeona kwamba serikali ya Chama Cha Mashetani (CCM) haijafanya chochote cha maana zaidi ya kujitapa na kaulimbiu ya “Hapa Kazi Tu”, kaulimbiu ambayo haina mashiko tena, hasa baada ya wananchi kugundua ulaghai uliojificha kwenye kaulimbiu hii. Ni maneno matupu tu ambayo hayawezi kuuvunja mfupa huku wananchi wakizidi kutopea kwenye lindi la umaskini. Hivi sasa Tanzania ni nchi ya tatu kutoka mkiani mwa nchi maskini baada ya Somalia na Afghanistan. Deni la taifa limekuwa kutoka Tsh trillion 22 alizoziacha Mkapa hadi Tsh trillion 55 sawa na ukuaji wa 150%! Ndugu zangu, naomba tuukatae umasikini kwa kuiondoa serikali ya Chama Cha Mafisi (CCM) madarakani. Tusikubali kuendelea kuburuzwa tena kama maboya. Tanzania yenye neema inawezekana tu kwa kuiondoa CCM madarakani kwa kuwa CCM na serikali yake dhaifu na ya kifisadi ndicho kizingiti (bottleneck/hurdle) cha maendeleo ya nchi hii. Kuikataa CCM ni kuukataa umaskini, ufisadi, udokozi, unafiki, uzandiki, nk. Ukitaka kuishi maisha bora tushirikiane kuiondoa CCM madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020.

Tuhakikishe wote, wake kwa waume, vijana kwa wazee, tunajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na tuzitunze shahada zetu vema hadi siku ya uchaguzi, twende tukampigie kura Mgombea wa CHADEMA, Tundu Antipas Lissu ili atuondoe kinywani mwa mamba mla watu (CCM), ambaye daima amepanua domo akitaka kutumeza bila huruma. Hii ndiyo hatua muhimu ya kujinasua kutoka utumwani (Serikali ya CCM) kuelekea katika nchi ya ahadi (Serikali ya CHADEMA), nchi itiririkayo maziwa na asali (maendeleo endelevu na maisha bora kwa kila mtanzania).

Miongoni mwetu kuna watu waliokata tamaa. Tuwe makini na watu hawa na daima tuwatie moyo na chachu ya mabadiliko (M4C). Hawa ‘wakata tamaa’ ni wale ambao hawaoni umuhimu wa kupiga kura kwa kisingizio kwamba hata kama wakipiga kura magamba wanaziiba. Msidanganyike ndugu zangu. Ukigoma kwenda kupiga kura humgomei mgombea wa gamba wala wa CHADEMA bali unajigomea mwenyewe. Usipopiga kura unawapa mwanya magamba wapite hata kama kwa tofauti ya kura chache. Kumbuka kwamba anayepata kura nyingi ndiye anyeshinda, hata kama akipigiwa kura na familia yake tu. Katika uchaguzi uliopita tumepoteza majimbo mengi kwa tofauti ya kura chache sana. Tusifanye makosa tena safari hii. Tujitokeze kwa wingi kupiga kura kuwachagua wagombea wote wa CHADEMA tukawafutilie mbali magamba. Kazi ni kwako ndugu mtanzania unayeishi maisha ya utumwa huku ukitembea juu ya ardhi iliyosheheni almasi, dhahabu, tanzanite, uranium na rasilimali nyingine nyingi tulizojaaliwa na Mungu. Tafakari, chukua hatua ya kuing’oa CCM madarakani kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020!
 
Polepole aliwahi sema uchaguzi ukiwa huru na haki ccm wajiandae kuwa chama cha upinzani
 
Mbona unawasemea watu? Jitizame wewe binafsi maana Kura ni Siri ya Mtu.
 
Wadau, tarehe 28 ndiyo hiyo inakaribia.

Wagombea wa urais wako wengi lakini mimi nimepanga kumchagua Magufuli. Sababu ninazo:

Kwa miaka mingi tulimsubiri Rais ambaye atarudisha nidhamu serikalini ili kusudi kwamba wananchi wote wapate huduma stahiki. Magufuli amefanya hivyo, nitamchagua.

Nilisubiri sana kupata Rais anayepambana na rushwa kwa vitendo kwani rushwa ni adui wa haki. Magufuli ameonesha kwa vitendo kuwa anaichukia rushwa na anapambana nayo.

Watanzania tulisubiri Rais ambaye atatuletea maendeleo ya watu na vitu. Magufuli amefanya hayo kwa vitendo kwani ameimarisha miundombinu, ameongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba. Anajenga zahanati na hospitali pamoja na kutoa elimu ya msingi bila malipo. Kura yangu nitampa.

Magufuli ni mzalendo haswa ambaye amejitoa sadaka kwaajili ya watanzania. Ni vigumu sana kupata Rais wa aina hiyo. Hajajilimbikizia mali, anapigana vita ngumu na zote anashinda. Kwanini nisimchague?

Magufuli ana uthubutu wa hali ya juu. Marehemu mzee Mengi alisisitiza sana kuwa ili ufanikiwe unahitaji uthubutu. Magufuli ameonesha uthubutu mkubwa kwenye mambo mengi ambayo yalionekana kama hayawezekani mfano ukiwa ni bwawa la Nyerere ambalo likikamilika litaboresha maisha ya watanzania kwa kushusha gharama za uzalishaji na kuhakikisha kila eneo la nchi hii lina umeme. Huyu anastahili kura yangu.

Magufuli amepigania madini yetu na sasa tumeanza kunufaika. Amepambana kubadilishana sheria za kinyonyaji, sasa tuko salama. Kura zote apewe.

Mambo ni mengi siwezi kuyaandika yote. Hebu niambie, naachaje kumchagua? Nimchague nani mwengine ambaye atafanya zaidi yake?

Amani Msumari
Tanga
 
Back
Top Bottom