Nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa Yanga inakata upepo kipindi cha pili

Mtanzanias

JF-Expert Member
Jul 30, 2021
1,747
3,714
Naona kuna kawimbo kanaendelea kakusema yanga inakata upepo kipindi cha pili, mimi sikubaliani na icho kitu kwakuwa sijaona timu inayokata upepo ikiwa ikiwa inaruusu nafasi za wazi kwa wapinzani kunufaika nazo.

Mara nyingi timu inayokata upepo aiwezi ikacheza mechi zaidi ya moja bila kuruusu goli kwakuwa kunakuwepo na mianya mingi ya kutengeneza magoli kutokana na wachezaji kuchoka, kwa yanga ilo sijaliona likitokea na ata wapinzani wanapopata nafasi inakuwa ni nafasi ngumu Sana kufunga.

Jambo la muhimu na kulipongeza benchi la ufundi kuna jambo la kiufundi linafanyika pale ambalo ni Kama mtego kwa opponent, timu nyingi tiyali zimeanza kuingia kwenye huo mtego wa kufikilia yanga inakata upepo kipindi cha pili ivyo wanakuwa na matumaini ya kurudisha magoli kipindi icho kumbe wanakuja kukutana na surprise nyingine ya ulinzi shirikishi.

Na unapojisahau zaidi kushambulia unapigwa goli jingine biashara inaishia apo, aiwezekani mechi 4 mfululizo timu inayokata upepo isiadhibiwe ata kwa goli la penalt ni ngumu, mkishapigwa goli na yanga ndo kwaheri baba jeni.
 
Halafu watu wanashindwa kuelewa ligi Ni marathon

Unatakiwa kujipanga kwa gemu 30

Sio kucheza game moja halafu gemu inayofuata unashindwa kucheza kupata matokea.

Mechi 27 bado zipo mbele lazima kocha awe na mbinu za ushindi kwa kila mechi inayokuja mbele yake.

Eti yanga inakata upepo wakati gemu ya Geita yanga alinyimwa Gori mbili kipindi Cha pili za wazi kabisa.

Wabongo bwana Ni wachambuzi uchwara Sana wakina Edo eti yanga anakata upepo lakini akicheza na Simba wanasema anakamiwa.

Sasa tuchukue lipi? Mimi natamani yanga ije ifungwe Gori dakika ya 45 kuelekea mapumziko halafu ndio tuje tujue kipindi Cha pili inakata upepo au wanapoza game kulinda matokeo ambayo wanayo.
 
Naona kuna kawimbo kanaendelea kakusema yanga inakata upepo kipindi cha pili, mimi sikubaliani na icho kitu kwakuwa sijaona timu inayokata upepo ikiwa ikiwa inaruusu nafasi za wazi kwa wapinzani kunufaika nazo.

Mara nyingi timu inayokata upepo aiwezi ikacheza mechi zaidi ya moja bila kuruusu goli kwakuwa kunakuwepo na mianya mingi ya kutengeneza magoli kutokana na wachezaji kuchoka, kwa yanga ilo sijaliona likitokea na ata wapinzani wanapopata nafasi inakuwa ni nafasi ngumu Sana kufunga.

Jambo la muhimu na kulipongeza benchi la ufundi kuna jambo la kiufundi linafanyika pale ambalo ni Kama mtego kwa opponent, timu nyingi tiyali zimeanza kuingia kwenye huo mtego wa kufikilia yanga inakata upepo kipindi cha pili ivyo wanakuwa na matumaini ya kurudisha magoli kipindi icho kumbe wanakuja kukutana na surprise nyingine ya ulinzi shirikishi.

Na unapojisahau zaidi kushambulia unapigwa goli jingine biashara inaishia apo, aiwezekani mechi 4 mfululizo timu inayokata upepo isiadhibiwe ata kwa goli la penalt ni ngumu, mkishapigwa goli na yanga ndo kwaheri baba jeni.
Nafikiri hili jambo lipo kiufundi zaidi,hata mimi sometime naona kama Yanga inakata upepo kweli kipindi cha pili...
 
NONDO jana aliulizwa hilo swali la kwamba kwanini wanakata upepo kipindi cha pili... Jibu lilikuwa wao wanacheza kutokana na maelekezo ya mwalimu... Kuna muda wanatakiwa watulize presha ya mpira... Na kufanya mashambulizi dakika za mwisho za mchezo
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom