Nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa Freeman Mbowe ni gaidi

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,549
Nitakuwa wa mwisho kwa akili zangu kuamini kua Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Mhe Freeman Mbowe ni GAIDI kwa sababu zilizo wazi kabisa. Mbowe hana chembe chembe za ugaidi na ni ajabu kuamini eti yeye ni gaidi.

Sababu za kunifanya niamini kua Mbowe si gaidi ni hizi:

1. Mbowe ndiye kiongozi pekee wa upinzani ambaye mbinu nyingi ovu za kumfifisha zimeshindwa.

2. Mbowe ameharibiwa mashamba na mali zake zote lakini hakuwahi kushuka kisiasa

3. Kupishana kwa kauli ya Msemaji wa polisi na hati ya mashtaka kua alikua na njama za kupanga kuua viongozi wa juu wa serikali, hizi zilikua tuhuma za uongozi za polisi kisha DPP akaondoa.

4. Kauli tata za wenye Mamlaka kua Mbowe alifunguliwa kesi toka mwaka jana na wengine wemeshshukumiwa wakati si kweli.Kesi ya Mbowe imefunguliwa mwaka huu.

5. Kauli aliyosema ameisikia Mbowe toka kwa RPC wa Kinondoni ndugu Kingai kua mara hii hachomoki. Hii inatoa taswira kua Ugaidi wa Mbowe ni wa kupewa.

6. Kauli ya IGP kua Mbowe naye ni binadamu anatenda makosa, hii ni kauli tata maana makosa huangaliwa kwa records za mtu na dhamira ya moyo wake. Hapa IGP alitaka kutuaminisha tuamini kua Mbowe ni gaidi.

7. Kauli ya Rais kua polisi walikua wanawabambikia watu kesi. Kama ikiwezekana hivyo,kwanini isiwe kwa Mbowe?

8. Kukamatwa viongozi wengine wa CHADEMA wanaozungumzia katiba. Kwani kuna dhambi gani kujadili katiba?

Kwanini tusiamini kuwa hili ndilo linalomweka Mbowe mahabusu hadi sasa?
 
Judge's walioteuliwa na mwenyekiti wa chama dola!majaji ni lazima waombe na wafanyiwe interviews kwa nafasi hizo! Amka wewe middle class wa Kitanzania
Tusubiri maamuzi ya majaji.

Unaweza ukamtetea mtu kumbe kweli kuna kitu nyuma ya pazia.judges
 
sio Gaidi ila anaweza amepanga kufanya kitu kinachoweza kuitwa ugaidi, kwa kuwa tunaambiwa akipanga kudhuru viongozi wa Serikali inawezekana alipanga kumdhuru Sir-Buyer kutokana na madhila famili yake na za watu wake wa karibu waliyopitia kiasi cha kuingia gharama kuihamisha familia Afrika Kusini

Kuna tetesi walikuwa wakinyanyaswa, kutekwa, kudhalilishwa kingono zamu kwa zamu. Na kwa kuwa alikuwa akilindwa, hakukuwa na namna kupatikana haki na kuamua kuchukua hatua

Ndio maana alisisitiza sana kukutana na Mama kumueleze haya yote, this was personel to him.

Uliwahi kusikia wapi mpaka IGP wanajitapa kuwa ushahidi wa kesi upo wa uhakika?

Naamini ataachiwa na Sir-Buyer anakwenda jela

Mawazo yangu tu
 
Kama hauamini Mbowe ni gaidi basi kajaribu kugombea uenyekiti wa Chadema.
Acha akili za kipumbavu, Mbowe ni mwanasiasa kwa karibia miaka 30 sasa ushawahi kumsikia kwenye kesi hata ya kupiga mtu kofi? Hii kesi inahusiana na kugombea uwenyekiti? Idiot!!
 
Sir-buyer amesema kuwa alikua anatumwa na aliyemtuma kafa. Ushahidi hakuna na kesi ndio kwaheri
 
Mleta mada utakuwa uijui CDM, ni bora ungenyamaza kwanza uulize ujuzwe, hiki chama sisi tuliokipigania miaka yote kilikuwa kikipata kiki za kisiasa kwa vitendo vya kigaidi na baadha ya wanachama wa kawaida hawajui ndiyo maana tulikuwa wengine tunaitwa nyumbu.

Kuna mbinu za kukubarika na jamii za kigaidi aliwai kuzitumia Aldof Hilter, za kulipua bundastag yaani bunge, kulipua mikutano na mengine mengi aliaminika na kuchukuwa nchi, CDM iliiga na kufanya mengi ila iliferi tu bahati mbaya kutokana na kutokuwa makini lakini ilisogea pazuri unadhani nani alikuwa straika. Usikichukulie hata kidogo kuwa Chadema kilikuwa chama cha kilaini, kipindi kile tulikuwa tukisema kama noma na iwe noma sijui kama ulikuwepo front.

Na ukiniudhi nitakutajia kikosi chote cha majasusi cha CDM.
Kaa kinya! tulia mwenyekiti ni kama yupo na madocta hospitali anachomwa dawa atapona tu.
 
Mleta mada utakuwa uijui CDM, ni bora ungenyamaza kwanza uulize ujuzwe, hiki chama sisi tuliokipigania miaka yote kilikuwa kikipata kiki za kisiasa kwa vitendo vya kigaidi na baadha ya wanachama wa kawaida hawajui ndiyo maana tulikuwa wengine tunaitwa nyumb...
Acha ujinga na kuongea uongo wa kipuuzi. Hivi tangu hayo matukio wanafanya kwanini hakuna kesi hata moja ya namna hiyo wala hakuna mfungwa yeyote? Hivyo vyombo vya dola hayo matukio vinayaangalia tu?
 
Judge's walioteuliwa na mwenyekiti wa chama dola!majaji ni lazima waombe na wafanyiwe interviews kwa nafasi hizo!amka wewe middle class wa kitanzania
Sawa lakini kwenye kesi ushahidi ndio unamfunga mtu au kumuacha huru na sio issue ya jaji amepatikanaje,tusubiri kama kambambikiziwa au la itajulikana
 
Acha ujinga na kuongea uongo wa kipuuzi. Hivi tangu hayo matukio wanafanya kwanini hakuna kesi hata moja ya namna hiyo wala hakuna mfungwa yeyote? Hivyo vyombo vya dola hayo matukio vinayaangalia tu?
Mi naona wewe ndiyo mjinga ni kama unaamini dunia haizunguki, tuko chini ya jua mwanangu kwamfano kule Arusha utamkamata nanani kirahisi au viongozi wa wa CDM unadhani walikuwa maboya katika mikakati yao.
 
Mleta mada utakuwa uijui CDM, ni bora ungenyamaza kwanza uulize ujuzwe, hiki chama sisi tuliokipigania miaka yote kilikuwa kikipata kiki za kisiasa kwa vitendo vya kigaidi na baadha ya wanachama wa kawaida hawajui ndiyo maana tulikuwa wengine tunaitwa nyumbu.

Kuna mbinu za kukubarika na jamii za kigaidi aliwai kuzitumia Aldof Hilter, za kulipua bundastag yaani bunge, kulipua mikutano na mengine mengi aliaminika na kuchukuwa nchi, CDM iliiga na kufanya mengi ila iliferi tu bahati mbaya kutokana na kutokuwa makini lakini ilisogea pazuri unadhani nani alikuwa straika. Usikichukulie hata kidogo kuwa Chadema kilikuwa chama cha kilaini, kipindi kile tulikuwa tukisema kama noma na iwe noma sijui kama ulikuwepo front.

Na ukiniudhi nitakutajia kikosi chote cha majasusi cha CDM.
Kaa kinya! tulia mwenyekiti ni kama yupo na madocta hospitali anachomwa dawa atapona tu.
Hahahaaa ... Kwa hiyo wewe unaamini Mbowe ni Gaidi?🤣🤣.. yaani humi ndani ya dhamiri yako siriniiii
 
Kila mtanzania anajua hizo ni hila za CCM maana kwa sasa hawana nguvu tena za kujibu hoja za wapinzani. wamebakia kutumia vyombo vya dola kutisha tisha wanaharakati na wanasiasa kitu ambacho hakina ustawi katika taifa lolote lile duniani.
 
Back
Top Bottom