Nitakuwa wa mwisho kuamini kama Rais Samia ataendelea na Urais baada ya 2025

The Burning Spear

JF-Expert Member
Dec 23, 2011
3,436
8,276
Ndugu zangu, Uraisi siyo kazi ya kitoto. Urais siyo lelemama. Hata Nyerere alilitambua hilo hadi akasema mtu anayetumia nguvu au fedha kuingia ikulu ni wa kuogopwa kama ukoma.

Tafasiri ya haraka haraka ni kwamba mpaka Dakika hii Samia nchi imeshamshinda, hakuna nchi ngumu kuongoza kama Tanzania ukizingatia ni Mzanzibar hata jiografia ya bara inampiga chenga.

Iko hivi, kuna maeneo watu wanajipigia bila uoga wala aibu kwa sababu wote ni wezi kuanzia TAKUKURU, Polisi hadi mawaziri Hakuna wa kumchunguza mwenzake. Huko kwenye halmashuri hali ya wizi ni mbaya sana.

Kikwete mwenyewe alishawahi kukiri. Nanukuu, "Nawaletea chuma hiki maana mlikuwa mnasema Mimi ni mpole, sasa anakuja mkali". Mwisho wa kunukuu.

Watanzania hawatakiwi kudekezwa utavuna mabua, nchi ilipokuwa imefikia kipindi cha kikwete Magufuli alikuwa hakwepeki that is why Hayati alipitishwa. Sawa?

Je, mlimsikia Mzee Makamba kipindi hicho? Nanukuu, "Huyu atawabatiza Kwa moto siyo maji tena" Walimtabua Kuwa alikuwa mtu sahihi kwa Watanzania.

Sasa nakuja kwa mama Samia ni hivi, Maza hana meno wahuni wa mjini wanamdhalilisha hajui afanye nini. Muda utafika wanachi hawatataka Hata kusikia jina lake.

Maana hawezi kubatiza Kwa moto wa siyo mkali, upole wake umezidi wa Kikwete. Kwa Mwenendo huu ubadhilifu wa kodi zetu kutumiwa na watu binafsi upo pale pale ndiyo maana kila kukichwa wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

Kama wewe unalipa Kodi PAYE, afu mwisho wa SIku unasikia watu wamepiga pesa afu wanaishia kusutwa tu badala ya kurudisha hela inauma sana. Aiseee tunafanyia KAZI watu. Mishahara yetu inakatwa kodi ili watu wale badala ya kuleta maendeleo.

Busara ilikuwa ni kukamilisha miaka 10 ya Awamu ya tano akae pembeni kwa heshima Tofauti na hapo atapata tabu sana. Pia kama taifa tutakuwa tumepata hasara kubwa mno.

Nawasilisha.
 
Hakuna kipindi ambacho hii nchi haijawahi kuibiwa, huyo jiwe mnaye sema sijui kipindi chake hakukuwa na wizi ndo kipindi akina makonda walimiliki majumba na magari kifahari yenye thamani ya mabilion ya pesa wakati wanapokea mshahara wa million 6 tu kwa mwezi.

Pia kipindi hicho cha jiwe ndo profesa Asad alifichua ubadhirifu wa trion 1.5 lakini jiwe akamshukia kama mwewe.

Miaka 6 ya jiwe hatukuwahi kuona fisadi yeyote akihukumiwa kwenda jera hali ya kuwa mafisadi yanajulikana.

Jiwe kitu ambacho alikifanya mpaka nikamkubali ni kukomesha tabia za uzembe makazini na kuanzisha baadhi ya miradi mikubwa ya kimkakati lakini kuja kunambia eti alidhibiti wizi hilo nakukatalia mpaka nakufa.
 
Ndugu zangu uraisi siyo kazi ya kitoto......uraisi siyo lelemama.....Hata Nyerere alilitambua Hilo Hadi akasema MTU anayetumia NGUVU au fedha kuingia ikulu ni wa kuogopwa kama ukoma.

Tafasiri ya haraka haraka.....ni kwamba mpaka Dakika Hii Samia nchi imeshamshinda,....Hakuna nchi ngumu kuongoza kama Tanzania ukizingatia ni Mzanzibar Hata jiigrafia ya bara inampiga chenga,

Iko Ivi kuna maeneo watu wanajipigia bila uoga Wala aibu Kwa sababu wote ni wezi kuanzia TAKUKURU, Polisi Hadi mawaziri Hakuna wa kumchunguza mwenzake. Huko kwenye halimashuri Hali ya wizi ni mbaya sana

Kikwete mwenyewe alishawahi kukiri. Nanukuu" Nawaletea chuma hiki maana mlikuwa mnasema Mimi ni mpole, sasa anakuja mkali". Mwisho wa kunukuu.

Watanzania hawatakiwi kudekezwa utavuna mabua, nchi ilipokuwa imefikia kipindi cha kikwete Magufuli alikuwa hakwepeki that is why Hayati alipitishwa........Sawa....

Je mlimsikia Mzee makamba kipindi hicho nanukuu" Huyu atawabatiza Kwa moto siyo maji tena" Walimtabua Kuwa alikuwa MTU sahihi Kwa watanzania

Sasa nakuja kwa mama Samia ni hivi.....maza Hana meno wahuni wa mjini wanamdhalilisha hajui afanye Nini.....muda utafika wanachi hawatataka Hata kusikia jina lake.

Maana hawezi kubatiza Kwa moto wa siyo mkali, upole wake umezidi wa kikwete, Kwa Mwenendo huu ubadhilifu wa Kodi zetu kutumiwa na watu binafsi upo pale pale....Ndo maana Kila kukichwa wanampaka mafuta Kwa mgongo wachupa.

Kama wewe unalipa Kodi PAYE, afu mwisho wa SIku unasikia watu wamepiga pesa afu wanaishia kusutwa tu badala ya kurudisha hela inauma sana......aiseee tunafanyia KAZI watu.....mishahara Yetu inakatwa Kodi ili watu wale badala ya kuleta maendeleo.

Mama Samia Hana wa kumsaidia pamoja na kujaza wazanzibar bara but they will not help any thing.kwa sababu nao wapo Kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar

Busara ilikuwa ni kukamilisha miaka 10 ya Awamu ya tano akae pembeni kwa heshima Tofauti na hapo atapata tabu sana....pia kama taifa tutakuwa tumepata hasara kubwa mno.

Nawasilisha.
Mimi nitakua wa mwisho wako zaidi
 
Akigombea ntamshangaa
Kwanini asigombee mkuu,atagombea na huenda akaendelea tu hadi miaka yake 10 yaani mpaka atakapomaliza term zake mbili.

Nchi nikweli ngumu sana kuiongoza sababu kumuongoza binadamu mwenye utashi wake siku zote siyo rahisi, lakini naona kama kadri muda unavyozidi kwenda anazidi kuwa sawa na confidence yake inazidi kuongezeka.

Katika suala la upigaji nafkiri hata hata kipindi cha mwendazake wapigaji walikuwepo tena walikuwa wapiji haswa ingawa walikuwa ni wachache sana hasa wale walio karibu naye ndiyo hasa walikula keki ya taifa.

Kwa hitimisho:

Naona ulichokiandika kiwe katika sehemu tu ya ushauri wako kwake na serikali yake ili yeye ajue mapema namna gani au wapi pakurekebisha au watu wake huenda kusikia habari zipi (Utumbuaji).

Ila kuendelea aendelee tu sababu hayo mawazo yako ya kuwawajibisha atayafanyia kazi kwakuwa yanamanufaa kwa uma pia.
 
Inategemea na wajeda wanasemaje! Wakimkubali umchague usimchague 2025 atapeta! Utabaki na kura yako ya hapana kwenye mabox ya kura!
 
Mazungumzo kati ya Samia na CAG :
""Samia:- tafadhali kwa wakati huu naomba weka kila kitu wazi tunataka kufahamu kila aina ya uchafu ndani ya Taifa letu.
CAG :-Nimekusika mh rais nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuweka kila kitu wazi hata yale yaliyokuwa yakifichwa toka kitambo tutayaangalia mh.
Samia: tafadhali fanya hivyo ili watanzania wafahamu na pia tupate kujua njia sahihi ambazo zitamaliza matatizo hayo moja kwa moja nafahamu upotevu ni mkubwa lakini hakuna namna ni lazima tufahamu kila uchafu and then tuuondoshe au tuwajibishane, naomba ripoti sahihi sitaki ripoti ambayo itaficha madudu kama ilivyokuwa kwa watangulizi wangu ""
N. B, Dr samiah alimpa kazi ya kata funua CAG,
Nimpongeze kwa hili maana mwingine angiliamrisha mengi tu yafichwe na yasiwekwe publics.
 
Samia : tafadhali fanya hivyo ili watanzania wafahamu na pia tupate kujua njia sahihi ambazo zitamaliza matatizo hayo moja kwa moja nafahamu upotevu ni mkubwa lakini hakuna namna ni lazima tufahamu kila uchafu and then tuuondoshe au tuwajibishane, naomba ripoti sahihi sitaki ripoti ambayo itaficha madudu kama ilivyokuwa kwa watangulizi wangu ""
N. B, Dr samiah alimpa kazi ya kata funua CAG,
Nimpongeze kwa hili maana mwingine angiliamrisha mengi tu yafichwe na yasiwekwe publics.
Wakati wanaongea haya,wewe ulikua umejibanza wapi unawaskiliza?
 
Mleta mada ni msukuma anaefurukuta Sukuma Gang . Rais wetu Samia hana mfano hata Nyerere hakuti. Hajawahi tokea Rais ndani ya miaka 2 katutoa kwenye shimo la wasukuma wachawi wa Gambosh mpaka shule na zahanati kila kata. Mpaka MACHADEMA magaidi yanachekelea. Waliobaki wachawi ni Sukuma gang tuu sababu wamezoea uchawi basi hawataacha wakidhani shetani wao Magufuli atafufuka. Mnataka afoke kama yule mchawi mwenzenu? Maveee.
Samia mpaka 2030 na akitaka tunamuongezea. Povu ruxaaa.
 
Hakuna kipindi ambacho hii nchi haijawahi kuibiwa, huyo jiwe mnaye sema sijui kipindi chake hakukuwa na wizi ndo kipindi akina makonda walimiliki majumba na magari kifahari yenye thamani ya mabilion ya pesa wakati wanapokea mshahara wa million 6 tu kwa mwezi.

Pia kipindi hicho cha jiwe ndo profesa Asad alifichua ubadhirifu wa trion 1.5 lakini jiwe akamshukia kama mwewe.

Miaka 6 ya jiwe hatukuwahi kuona fisadi yeyote akihukumiwa kwenda jera hali ya kuwa mafisadi yanajulikana.

Jiwe kitu ambacho alikifanya mpaka nikamkubali ni kukomesha tabia za uzembe makazini na kuanzisha baadhi ya miradi mikubwa ya kimkakati lakini kuja kunambia eti alidhibiti wizi hilo nakukatalia mpaka nakufa.
Kwani si ndio haya wanayosema alikuwa anachukua tu kwa watu mpaka mkamfungulia kesi. Kwa hiyo hakuwa anaiba. Hayo majumba ya kifahari ni yapi? Mbona ana nyumba ya kawaida tu.
 
Mazungumzo kati ya Samia na CAG :
""Samia:- tafadhali kwa wakati huu naomba weka kila kitu wazi tunataka kufahamu kila aina ya uchafu ndani ya Taifa letu.
CAG :-Nimekusika mh rais nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuweka kila kitu wazi hata yale yaliyokuwa yakifichwa toka kitambo tutayaangalia mh.
Samia: tafadhali fanya hivyo ili watanzania wafahamu na pia tupate kujua njia sahihi ambazo zitamaliza matatizo hayo moja kwa moja nafahamu upotevu ni mkubwa lakini hakuna namna ni lazima tufahamu kila uchafu and then tuuondoshe au tuwajibishane, naomba ripoti sahihi sitaki ripoti ambayo itaficha madudu kama ilivyokuwa kwa watangulizi wangu ""
N. B, Dr samiah alimpa kazi ya kata funua CAG,
Nimpongeze kwa hili maana mwingine angiliamrisha mengi tu yafichwe na yasiwekwe publics.
Mbona kuna mengi tu yamefichwa ambayo yakiachiwa nchi itapasuka. Kuna pesa nyingi mno huyu mama ka,itoa nje ya utaratibu wa bunge na bajeti.

Mfano aliwalipa dowans billion 360 bila hata bunge kujua, amempa January Makamba trillion moja wanazosema wanaboresha mitambo ya tanesco ambapo Januari alisema zinatakiwa trilioni 4 ili kukamilisha zoezi.

Kuna pesa ambazo Nape alikiri wamewapa wenye maduka ya kubadilisha fedha kama kifuta machozi.

Kuna billions of shillings zimepigwa wakati wa zoezi la anuani ya makazi na hakuna chochote cha maana zaidi ya kuchukua mitipori na kupachika.

Huko NHIF alipo Makinda wamepotea ripoti sababu Makinda alimsifia sana Magu kiasi cha kuwabeza wanaomsema vibaya Magu ndio maana file lake limeachiwa.

Ndugu kila kitu kikiwekwa wazi tutakimbiana. Ikumbukwe mpaka sasa mama ameshakopa zaidi ya trilioni 20 ndani ya miaka miwili na mpaka sasa thamani ya vitu alivyofanya haifiki hata trilioni 7.
 
Back
Top Bottom