WamLola
JF-Expert Member
- Aug 12, 2012
- 343
- 122
Nimepata kumsikiliza vizuri aliyewahi kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi Na pia aliyekuwa waziri mwenye dhamana ya vijana utamaduni sanaa na michezo.
Katika kuchangia hoja ya Mpango wa Taifa wa maendeleo 2017-2018 Nape nnauye analalamika Serikali kuzisahau sekta binafsi(Private Sector) katika ujenzi wa miradi mikubwa na badala yake Serikali kutumia fedha za mikopo kugharamia miradi mikubwa.
Kwanza kabisa napenda kumkosoa Nape juu ya hoja yake hii,Nadhani Nape amesahau kwamba moja ya misingi mikubwa ya Private Sector katika kuendesha miradi ni kutafuta faida kwanza
Sioni kwamba watanzania wanyonge hawa wataweza kumudu kupata huduma mbalimbali kutoka miradi kama Maji,Umeme, Reli nk ambapo gharama zake zitakuwa juu ili kurudisha gharama za wawekezaji.
Naomba kumkumbusha Nape kwamba Moja ya msingi wa kwanza kabisa wa mikopo kama Tanzania tunayokopa ni kwamba "Huruhusiwi kutumia pesa ya mkopo katika matumizi ya kawaida na badala yake Pesa ya mikopo inatakiwa iingie katika miradi ya maendeleo"
Sio dhambi kwa serikali yetu kutumia mikopo katika kujenga
Barabara.
Umeme.
Reli.
Maji.
nk
Serikali naamini kwamba iko makini, hatuko tayari kuwakabidhi wawekezaji (Private Sector) katika miradi mikubwa na baadae wanufaike kupata utajiri kupitia watanzania wanyonge
Naomba kurudia kumkumbusha Nape Nauye kwamba Sekta binafsi si suluhisho la maendeleo ya nchi yetu bali sekta binafsi zitakuwa mwiba na uchungu mkubwa kwa watanzania endapo tutazipa nguvu ya kutekeleza miradi yetu.
Nadhani Nape nnauye alikurupuka kuchangia suala hili Na napenda kumshauri kwamba si kila anachowaza yeye kiwe ndio kipaumbele cha serikali
Nawapongeza waziri Mpango(Wizara ya fedha na mipango)
Makame mbarawa (Wizara ya ujenzi na usafirishaji)
Medard Kalemani (Wizara ya Nishati na Madini)
Wanafanya kazi zao kwa weledi na wanahitaji kutiwa moyo na watanzania ili kuendeleza mengi ambayo wanapanga kuyatekeleza.
Ni hayo tu niliyotaka kuyafikisha kutokana na Kelele nyingi alizopiga Nape Nauye akizipigia Upatu sekta binafsi(Private Sector)