Nitajiunga na CCM kama Rais Magufuli nae atajiuzulu urais na kujiunga na CCM

Yericko Nyerere

Verified Member
Dec 22, 2010
16,801
2,000
Mimi nitahama CHADEMA na kujiunga na CCM mpya kama rais wangu Magufuli nae atajiuzulu urais na kujiunga na CCM, hili nalisubiri kwa hamu, Nasema wazi na msemakweli ni mpenzi wa Mungu, Nasubiri siku John Pombe Magufuli nae "ajiuzulu" urais ili ajiunge na "CCM mpya" ya Humphrey Polepole kwa kuwa inapambana na ufisadi inayotekeleza ilani yake nk.... Kama kuna mtu anamshauri rais aina ya siasa anayofanya basi hamtakii mema taifa, na huyo ndiye adui wa watanzania kwakuwa kwakushauri kwake, analiangamiza taifa na chama cha mapinduzi cha mapinduzi.....!

CCM mpya haitajengwa kwa unafiki wa upanga, haitajengwa kwa dola wala haitajengwa kwa vitisho. CCM Mpya itajengwa kwa kuongoza nchi kwa kufuata katiba na sheria, kwakujenga chama cha siasa cha hiari sio hiki cha lazima, kwakupeleka mafawa hospitali, kwakuhakikisha mgao wa umeme unakuwa historia, kwakuhakikisha mikopo kwa wanafunzi vyuoni, kwakuhakikisha hakuna mtanzania anayebomolewa nyumba yake bila kulipwa fidia, na mambo mengine yote yenye kukiuka haki za kiraia na za kibiadamu

Jambo muhimu eleweni, njia hiyo haitaleta madawa hospitali, haitaleta elimu bora, haitaleta nchi ya viwanda, wala haitaleta bei ya sukari kuwa chini dukani.

Dukani kwa Mpemba ama kwa Mangi ukienda huendi na kadi ya CCM, unaenda na sarafu yenye kichwa cha Mwalimu Julius Nyerere na mwenge wa uhuru tu, ama utakwenda dukani na sarafu yenye kichwa cha Abeid Amani Karume na mmea wa Karafuu tu...

Ati kuna mtu anafurahishwa na utendaji wa Rais Magufuli ndio anajiuzulu uongozi wa kisiasa aliopewa na wananchi??? Kwani Magufuli anawatumikia watu gani kama sio haohao wananchi?

Ninaomba mtu yoyote nchini awe Chakubanga au Kinana au yeyote yule, aje hadharani akiwa HURU kabisa aseme Rais Magufuli amefanya nini KIPYA kikubwa CCMMASLAHI kwa Taifa tofauti na watangulizi wake?????

Mmoja ya wanachadema aliyelazimishwa kwenda CCM kwa shinikizo la vyombo vya serikali vinavyotumia kodi za umma amenululiwa akisema:,
______________________
"Wapendwa kazi zangu zimevulugwa Sana. Na urudisha mwili CCM, kulinda zilizo baki. Nature ya kazi yangu inategemea Sana serikali, I will never speak negativity about CHADEMA, is a part which I love most. Wachache wanajua niliwashirikisha namna nilivyofilisiwa kupitia TRA, kuporwa Zahanati yangu, kuzuiwa biashara yangu ya mbao. Kuondolewa kwenye jengo la ofisi yangu makao makuu kwa hila. Kuzuiwa kwa hila mchakato wa kupima shamba langu kirare. Hivi karibuni Shughuli zangu Lushoto kuzuiwa kwa hila. Mengi na mengi haya ninayosema ni machache....

David Chanyeghe"
______________
Ukweli unabaki kuwa ukweli, hata kama utasimamiwa na mtu mmoja tu ama ule uliosimamiwa na Mtume Mohamed na Yesu Kristo, Safari ya Mabadiliko bado inaendelea, wapo ambao tulianza nao safari na hawatafika mwisho, wasiwakatishe tamaa, kwani wapo wapya ambao watajiunga nasi kwenye safari hii. Ila kwa uhakika ni safari ngumu inayokutaka ujikane kwaajili ya taifa lako.

Na Yericko Nyerere
 
Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,842
2,000
Ni vigumu kwa Magufuli kujiunga na CCM iliyojaa majizi akiifikria CCM anahisi kutapika mpaka anashindwa kusema CCM hoyee.
 
mitigator

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,933
2,000
usiendelee kuwa karai
Mmekua vijitu vya ajabu kweli mithili ya shetani kushangilia kichaa akijeruhi wananchi.Shamelessly, mtu mzima eti naunga mkono.Haki ya nani endeleeni kutoa ushuzi tu,Mungu wa Mbinguni hadhihakiw ni suala la muda tu
 
Kikarara78

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
1,496
2,000
Boss Yericko Nyerere Well Said and Noted, Mpaka upate uwezo wa KIROHO tu ndio utaelewa ili Bandiko. Tuzidi kuliombea Taifa.

Mimi nitahama CHADEMA na kujiunga na CCM mpya kama rais waCCM Magufuli nae atajiuzulu urais na kujiunga na CCM, hili nalisubiri kwa hamu, Nasema wazi na msemakweli ni mpenzi wa Mungu, Nasubiri siku John Pombe Magufuli nae "ajiuzulu" urais ili ajiunge na "CCM mpya" ya Humphrey Polepole kwa kuwa inapambana na ufisadi inayotekeleza ilani yake nk.... Kama kuna mtu anamshauri rais aina ya siasa anayofanya basi hamtakii mema taifa, na huyo ndiye adui wa watanzania kwakuwa kwakushauri kwake, analiangamiza taifa na chama cha mapinduzi cha mapinduzi.....!

CCM mpya haitajengwa kwa unafiki wa upanga, haitajengwa kwa dola wala haitajengwa kwa vitisho. CCM Mpya itajengwa kwa kuongoza nchi kwa kufuata katiba na sheria, kwakujenga chama cha siasa cha hiari sio hiki cha lazima, kwakupeleka mafawa hospitali, kwakuhakikisha mgao wa umeme unakuwa historia, kwakuhakikisha mikopo kwa wanafunzi vyuoni, kwakuhakikisha hakuna mtanzania anayebomolewa nyumba yake bila kulipwa fidia, na mambo mengine yote yenye kukiuka haki za kiraia na za kibiadamu

Jambo muhimu eleweni, njia hiyo haitaleta madawa hospitali, haitaleta elimu bora, haitaleta nchi ya viwanda, wala haitaleta bei ya sukari kuwa chini dukani.

Dukani kwa Mpemba ama kwa Mangi ukienda huendi na kadi ya CCM, unaenda na sarafu yenye kichwa cha Mwalimu Julius Nyerere na mwenge wa uhuru tu, ama utakwenda dukani na sarafu yenye kichwa cha Abeid Amani Karume na mmea wa Karafuu tu...

Ati kuna mtu anafurahishwa na utendaji wa Rais Magufuli ndio anajiuzulu uongozi wa kisiasa aliopewa na wananchi??? Kwani Magufuli anawatumikia watu gani kama sio haohao wananchi?

Ninaomba mtu yoyote nchini awe Chakubanga au Kinana au yeyote yule, aje hadharani akiwa HURU kabisa aseme Rais Magufuli amefanya nini KIPYA kikubwa CCMMASLAHI kwa Taifa tofauti na watangulizi wake?????

Mmoja ya wanachadema aliyelazimishwa kwenda CCM kwa shinikizo la vyombo vya serikali vinavyotumia kodi za umma amenululiwa akisema:,
______________________
"Wapendwa kazi zangu zimevulugwa Sana. Na urudisha mwili CCM, kulinda zilizo baki. Nature ya kazi yangu inategemea Sana serikali, I will never speak negativity about CHADEMA, is a part which I love most. Wachache wanajua niliwashirikisha namna nilivyofilisiwa kupitia TRA, kuporwa Zahanati yangu, kuzuiwa biashara yangu ya mbao. Kuondolewa kwenye jengo la ofisi yangu makao makuu kwa hila. Kuzuiwa kwa hila mchakato wa kupima shamba langu kirare. Hivi karibuni Shughuli zangu Lushoto kuzuiwa kwa hila. Mengi na mengi haya ninayosema ni machache....

David Chanyeghe"
______________
Ukweli unabaki kuwa ukweli, hata kama utasimamiwa na mtu mmoja tu ama ule uliosimamiwa na Mtume Mohamed na Yesu Kristo, Safari ya Mabadiliko bado inaendelea, wapo ambao tulianza nao safari na hawatafika mwisho, wasiwakatishe tamaa, kwani wapo wapya ambao watajiunga nasi kwenye safari hii. Ila kwa uhakika ni safari ngumu inayokutaka ujikane kwaajili ya taifa lako.

Na Yericko Nyerere
 
Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
11,039
2,000
TISS aliyepandikizwa image ya UCHADEMA si tumeshakujuaga muda sana.Na ungekuwa CHADEMA ungeshapotezwa muda sana nilikusikilizaga siku moja you tube nikajua mengi kuhusu wewe kupitia ile interview
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom