BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,167
Kama kweli una nia ya kuisafisha BOT basi aanza na kuwafukuza kazi wale wote waliohusika na malipo hewa ya shilingi 133 bilioni na uhakikishe wanatiwa ndani mara moja ili wasivuruge ushahidi. Hiyo ndio inastahili iwe hatua yako ya kwanza, vinginevyo itakuwa ni usanii tu ambao umeshatuchosha.
Nitaisafisha BoT - Ndulu
na Joseph Senga
Tanzania Daima
GAVANA mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, amesema jukumu lake la kwanza litakuwa ni kusafisha mazingira machafu ndani ya taasisi hiyo nyeti, ambayo inakabiliwa na tuhuma mbalimbali za ubadhirifu.
Ndulu ambaye ndiye aliyetangazwa kuchukua nafasi ya Daudi Balali, aliyeachishwa kazi jana, aliyasema hayo jana hiyo hiyo wakati alipofanya mahojiano ya ana kwa ana na Tanzania Daima ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Alisema anatambua wasiwasi ambao umewajaa Watanzania ambao sasa hawana imani na Benki Kuu, kutokana na tuhuma za ubadhirifu katika taasisi hiyo kubwa na nyeti.
"Nitahakikisha tunasafisha kwa kila hali chombo hiki ili kurudisha imani ya Watanzania, hasa kutokana na maovu haya ya ubadhirifu mkubwa wa fedha uliojitokeza. Hiki ni chombo cha Watanzania, nawahakikishia kwamba nitasimamia hilo kwa nguvu zangu zote," alieleza.
Aidha, alikitaja kipaumbele chake cha pili katika wadhifa wake huo mpya kuwa ni pamoja na kuweka nguvu na akili zote katika kudhibiti mfumuko wa bei ili kuufanya uchumi uendelee kuwa imara na usioyumba.
Akielezea mikakati ya kukamilisha hilo, alisema atahakikisha anaanzisha mipango ya kiuchumi itakayofanikisha kushuka kwa kiwango cha riba, ili kuwawezesha wananchi kukopa katika mabenki.
Kipaumbele cha tatu ambacho alikitaja gavana huyo mteule ni kusimamia vizuri uendeshaji wa mabenki, ili kujenga kizazi kipya kwa kuwapa nafasi zaidi vijana ambao wana uwezo na nguvu kubwa.
Akizungumzia kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo, Profesa Ndulu alisema uteuzi huo ameupokea kwa moyo mmoja na kwamba Rais Kikwete ameonyesha kuwa ana imani kubwa kwake.
Alisema kutokana na imani hiyo, atajitahidi na yeye kwa upande wake kutoa mchango mkubwa katika kuiendesha taasisi hiyo.
"Kwa ujumla nimefurahi sana, pamoja na hali ngumu, lakini rais ana imani na mimi kuwa nitatoa mchango mkubwa kurudisha hadhi ya BoT, ninamheshimu sana, ninamfahamu vizuri, nimewahi kushirikiana naye wakati nikiwa Mwenyekiti wa kwanza wa TRA, nitampa support ya kiakili na nitakuwa mkweli," aliongeza.
Profesa Ndulu pia alisema atatoa ushirikiano mkubwa kwa timu iliyoundwa na rais, ambayo itayafanyia kazi kisheria matatizo ya ubadhirifu uliobainishwa kupitia ukaguzi uliofanywa na Kampuni ya Ernst & Young.