Shairi: Nitainuka

simba29

Senior Member
Jun 22, 2011
193
67
Nichezee upate raha,
Kwa ujinga jazie furaha,
Ni binadamu kwako Mi kifaa,
Sote twafa hatuijui saa,

Kwangu umefanya kwako,
Mjinga mkubwa tacheka kifo chako,
Yote Yana mwisho,
Na yako kikomo kesho,

Moyo unazizima,
Hasira nafura cheche natema,
Navuja jasho nyayo mpaka juu,
Naapa kifo chako sikukuu,

Damu yangu namwaga,
Kwa fahari wanangu pate mwanga,
Sijali wangapi wametonga,
Mstari wa mbele nasonga,

Nikuondoshe mwanaharamu,
Mizimu na mababu wakaramu,
Sasa yatosha kipimo,
Pokea ya uovu mavuno,

0655880157
-S1mba
 
Mashairi yapo aina nyingi na yenye bahari nyingi, nachelea kusema umekariri lakini vema ungeuliza kama waona mushkeli badala ya kumtilia shaka mtunzi.
Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe.
Sitakuambia maana kwa kuwa wewe na SIKIRI mna tabia zinafanana.
Utenzi unakufaa kiweka shairi utakufa.
 
nimechelewa kurudi huku..... nashukuru ndugu Dotto kwa kunisaidia kujibu , umenena vyema kabisa. asante sana
tuendelee kuelimishana na kujengana
 
Naomba unifundishe kutofautisha shairi na utenzi.
Mimi ni mwanafunzi wako.
ushairi na utenzi hauna tofauti yeyote bali utenzi ni mona kati ya muundo ama sifa katika mtindo au jinsi mshairi alivyoandika.
katika utenzi huwa tunafanya kipande kimoja katika mshororo.
na kwa kawaida wengi tumezoea vipande viwili katika mshororo vyenye mishororo minne.
na katika utunzi wa ushairi kuna mambo mengi sana na kulingana na mabadiliko ya kishairi,ushairi kwa sasa umegawanywa katika mafungu mawili.
moja ni mapokea na pili n huru.
yote hayakayakataliwi kwa kuwa kila mtu na uhuru wake katika utunzi na wala hakuna makosa.
makosa ni pale mtu anapoenda tofauti na aina yake ya utunzi.
mtunzi yupo sahihi kabisaaaaaaa.
 
Mkuu umeelea kwenye lugha kiasi kwamba imekuwa vigumu kumuelewesha msomaji mgeni wa ushairi, ingeleta maana kama ungetofautisha uhuru wa tungo na tungo ya kimapokeo yaani vina na mizani tujue umebobea wapi.
Hata hivyo nasubiri mchanganuo huo kwa faida ya wanajamvi mkuu.
 
Mapokeo ni aina zote za mashairi ambazo zinafata sheria zote za ushairi,kama vina na mizani
na mashairi huru ni yale yasofata sheria yoyote ya ushairi bali mtunzi anaweza kutunga kama anavyotaka.
 
Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe.
Sitakuambia maana kwa kuwa wewe na SIKIRI mna tabia zinafanana.
Utenzi unakufaa kiweka shairi utakufa.
Tutoke kwenye ushairi sababu huko mimi si mjuzi sana pamoja na kwamba najaribu kuungaunga beti.

Kwenye misemo na methali za kiswahili si mbobezi, lakini mwenye kutaka kunidanganya katika uga huu afanye kazi sana, hivyo kama kuna pungufu lolote naliona mapema.

"Mchelea mwanakulia hulia mwenyewe" methali hiyo hujaitendea haki sababu umeitumia ndivyo sivyo.

Nitakuja..... inshallah!
 
Mapokeo ni aina zote za mashairi ambazo zinafata sheria zote za ushairi,kama vina na mizani
na mashairi huru ni yale yasofata sheria yoyote ya ushairi bali mtunzi anaweza kutunga kama anavyotaka.
Siyo nia yangu kukupinga, napenda kupata ufafanuzi kama ambavyo umekuwa ukifanya.

Nimefurahi kuona kuwa unajua kwamba mashairi yana sheria zake. Usipofuata hizo sheria unakuwa nje ya ushairi.

Mshairi Andanenga alipata kuandika shairi lisemalo "mcheza hawi kiwete, ngoma yataka matao"

Ili uweze kughani shuruti shairi liwe na mizani na vina.
mfano wa "mcheza" ni shairi na "matao" (matako) ni mizani na vina.

Sasa basi utanenguaje kwenye tungo iso vina wala mizani?

Au unakusudia mashairi ya bongo fleva???!!!
 
Umefafanuliwa vizuri kuwa kuna mashairi ya namna mbili, ya kimapokeo na huru.
Mosi.
KUHUSU KUIMBIKA.

mashairi mengi si kama yote ya kimapokeo yanaimbika, hii kutokana na uzingatiaji wa mizani na vina. lakini haimaamishi kuwa mashairi huru au ya kisasa hayambiki, hii ni kwasababu wanamuziki wengi hutumia mashairi ya kisasa.

Pili.
KUHUSU MATAO.

Matao si matako kama ulivyosema hapo juu, matao ni uchezaji wa ngoma kwa kufuta mdundo wake kama inavyotakikana, pia hujulikana kama mbwembwe.
Siyo nia yangu kukupinga, napenda kupata ufafanuzi kama ambavyo umekuwa ukifanya.

Nimefurahi kuona kuwa unajua kwamba mashairi yana sheria zake. Usipofuata hizo sheria unakuwa nje ya ushairi.

Mshairi Andanenga alipata kuandika shairi lisemalo "mcheza hawi kiwete, ngoma yataka matao"

Ili uweze kughani shuruti shairi liwe na mizani na vina.
mfano wa "mcheza" ni shairi na "matao" (matako) ni mizani na vina.

Sasa basi utanenguaje kwenye tungo iso vina wala mizani?

Au unakusudia mashairi ya bongo fleva???!!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom