Uchaguzi 2020 Nitahakikisha wakulima wa pamba wanalipwa fedha zao"Prof. Lipumba" Maswa, Simiyu

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
IMG_20201001_164126_813.jpg
NITAHAKIKISHA WAKULIMA WA PAMBA WANALIPWA FEDHA ZAO"PROF. LIPUMBA"

MASWA, SIMIYU

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof.Lipumba amesema kuwa endapo atachaguliwa kuwa rais atahakikisha wakulima wa pamba wanapata fedha zao kwa wakati.

Pia, Prof.Lipumba amesema atasimamia kwa makini katika sekta ya kilimo na maendeleo ya viwanda.

Dira ya Mabadiliko ya CUF inakipa kilimo nafasi ya pekee katika mikakati ya kukuza uchumi na hivyo kuwaondolea umasikini wananchi wengi na hasa wa vijijini, na kuhakikisha Taifa linakuwa na chakula cha kutosha na ziada ya kuuza nje ya nchi.

Katika miaka mitano ijayo, bajeti ya sekta ya kilimo itakayoandaliwa na serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itakuwa kati ya
asilimia 10-15 ya bajeti yote, na italenga katika kuimarisha maeneo yafuatayo:

 Utafiti na elimu kwa wakulima na huduma za ugani;

 Upatikanaji wa mbolea na pembejeo nyingine kwa bei nafuu;

 Kurahisisha upatikanaji wa zana za kilimo ikiwa ni pamoja na matrekta;

 Masoko ya uhakika ya ndani na nje ya nchi;

 Bei nzuri kwa wakulima;

 Kutengeneza barabara za vijijini; na

 Kusambaza umeme vijijini kwa kutumi

Dira ya mabadiliko ya CUF inakusudia kuasisi Mapinduzi ya kweli ya kilimo nchini, yatakayoongeza uzalishaji na tija kwa kuijenga upya sekta ya maendeleo ya viwanda.

Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF intaweka mkakati madhubuti wa kuanzisha na kuendeleza viwanda vinavyotumia malighafi ya
ndani ya nchi na kuajiri watu wengi - kama vile viwanda vya nguo na mavazi, viatu na bidhaa za ngozi, vifaa vya matumizi ya nyumbani na vifaa vya umeme na elektroniki.
 
Back
Top Bottom