Nitafurahi Raisi wangu aendeleze utaratibu wa kuuliza matumizi ya hela za majimbo kwa wabunge wote asiishie kwa wale tu

msulupwete

Senior Member
Dec 9, 2013
155
59
Hongera na pongezi zikufikie raisi wetu mpendwa. Nafuatilia ziara yako vizuri kuna mengi nayafurahia hasa unaposimama kinara kuuliza fedha za jimbo zimetumikaje kuwanufaisha wananchi wako wanyonge. Napata furaha isiyokifani unavyowabana wabunge mpk wanajikamua kujibu maswali unayouliza ni dhahir unauchungu na fedha za walipa kodi .

Ombi langu kwako mh raisi uulize kila jimbo wala usiishie kwenye majimbo hayo tu, uulize kila ziara yako ili tujue wananchi maana tumepigwa sana.

Mie niseme tu mi ni mwanachama wa CCM sasa hawa waccm ndo nataman kuona wanabanwa zaidi ili kuonesha mfano maana CCM ndio ipo madarakani na ni lazima chama kioneshe mfano hadharani.

Natumai utanisikiliza mwananchi wako mnyonge
 
Anataka kuwadhalilisha wa upande ule ili wananchi waone nyumbani kumenoga. Kwahiyo hatazingatia ushauri wako ingawa mi nauona ndo alipaswa kufanya na kuondoa double standard
 
Anataka kuwadhalilisha wa upande ule ili wananchi waone nyumbani kumenoga. Kwahiyo hatazingatia ushauri wako ingawa mi nauona ndo alipaswa kufanya na kuondoa double standard
Yeh wengine wasiwe wanapiga sarakasi mpk boksa zinaonekana wengine wanabanwa hahaha
 
Yeye yupo ktk kuwadhalilisha wale wa upande ule waonekane hawajuwi walifanyalo. Na matukio yale yanakuwa staged mapema kabisa.
Kwa upande wa chama baba, wanakuwa wameshapewa majibu ya mtihani.
Hukumbuki Arusha kuna mtu aliitwa mpumbavu baada ya igizo kubuma
 
Back
Top Bottom