Nitafurahi Kilimanjaro Stars wakipandishwa kwenye lori kurudi nyumbani baada ya mechi ya mwisho, wametuaibisha mno!

Si Utani wameniboa ile mbaya kama mtanzania mzalendo. Kiwango chao walichonacho ni tofauti na wachezaji wote wanaoshiriki hii michezo, Kwa kuwa wamefanya maksudi kutuaibisha, heshima yao ni kuwarudisha kwa usafiri wa lori na siyo ndege. Itapendeza zaidi
Tanzania kama nchi imewahi kufanikiwa katika lipi kiasi tuwabebeshe lawama vijana wasio na elimu hali ya kwamba hata tuliowagharamia elimu wanaboronga?

Tuanze na maprofesa wetu kwanza, maana kwa wenzetu Vyuo Vikuu ni sehemu za mavumbuzi, kwetu ni ofisi za kuchukulia mshahara.
 
Hapa ni soka hayo ya siasa tulishachoka nayo.
 
Yaani nina hasira na kile kikocha chao kinajifanya kuishi kwake ulaya tuonekane mazuzu anakera na mipango yake ya ajabu.

Kwanza naomba hata wapotee huko Machakos tutafute timu mpya ya taifa yenye vijana wenye uchu sio hawa wazee.
 
Back
Top Bottom