Nitafundisha computer bila ada

KANOSAWA

Member
Sep 16, 2016
55
39
Ajira duniani hutolewa kwa wenye ujuzi au maarifa husika. Ni mara chache sana kusikia mtu kaajiriwa kwa sababu ya elimu aliyonayo. Isipokuwa elimu ya mtu huwa ni kiungo kwa ujuzi au maarifa aliyonayo.
Mfano: Kijana amesoma hadi kidato cha NNE, kisha akaenda chuo cha Hotel Management, atapata ajira ya Hotel Management na sio elimu ya kidato cha NNE.

Watu au vijana wetu mitaani hawana ajira kwa kuwa hawana maarifa ambayo waajiri wanayataka.
Lingine ni kuwa wengi hawawezi kugharamia maarifa wanayoyatamani kwa sababu mbalimbali.

Naomba kuungwa mkono kwa nia njema kuisaidia jamii/vijana kwa kutoa maarifa ya Computer bure yaani bila kulipia ada.
Lengo ni kuwasaidia jamii inayotamani kufikia malengo lakini inashindwa sababu ya kushindwa gharama.
Lengo lingine ni kuwa kama vijana 2000 watafanikiwa kupata ajira au kujiajiri baada ya huduma hii, na fikiria kila mmoja akazalisha 2,000 kwa Siku, kutaongezeka pato la Tsh 4,000,000 kwenye mzunguko wa uchumi wa nchi yangu ya Tanzania.

Masomo nitakayotoa ni
1. Introduction to computer (Kuitambua computer: ina mada / topics 30)
2. Application in a computer (Kuitumia computer: ina topics 12)
3. Microsoft Word 2003 (Kuandika: Ina topics 70)
Na
4. Internet & Emails(Mawasiliano: ina topics 7)
Masomo hayo tu yatakuwa ni free au bure bila ada. Yatafundishwa kwa wiki nane.

Faida zitakazojitokeza hapo ni mlengwa kuwa na uwezo wa kujiendesha mwenyewe bila uhitaji wa msaada wa mtu mwingine. Hususani watanzania tunahitaji kuwa na watu wengi kama sio wote wenye uwezo wa taaluma hii. Faida nyingine ni kujiajiri. Faida nyingine ni kuajiriwa, nk.

Walengwa ni wakazi wa jiji la Makonda na kwa mikoani nitaenda kwa mwaaliko maalum.

OMBI LA KUUNGWA MKONO
1. Kwa yeyote mwenye kunielewa, namwomba ajitolee chumba au ukumbi au anilipie chumba au ukumbi ili niweze kuwagia maarifa hayo.
2. Kwa yeyote mwenye kunielewa, namwomba ajitolee vitendea kazi kama computers, projector au au viti dawati ili niweze kuwagia maarifa hayo.

Kazi hii ya kuinua uchumi wa watu ni yetu sote, na sio serikali peke yake.
Unaweza kuni PM
Naomba kuwakilisha.
 
OMBI LA KUUNGWA MKONO
1. Kwa yeyote mwenye kunielewa, namwomba ajitolee chumba au ukumbi au anilipie chumba au ukumbi ili niweze kuwagia maarifa hayo.
2. Kwa yeyote mwenye kunielewa, namwomba ajitolee vitendea kazi kama computers, projector au au viti dawati ili niweze kuwagia maarifa hayo.

Kazi hii ya kuinua uchumi wa watu ni yetu sote, na sio serikali peke yake.
Unaweza kuni PM
Naomba kuwakilisha.


Mawazo mazuri! Nadhani uki PM Makonda mwenyewe na kutafuta NGO'S kadhaa huwezi kuangukia Pua.
Je wewe mwalimu wa mtaani(Uzoefu) au mwalimu kwa uhalisia (Fani). Hongera na chukua hatua kutimiza ndoto hiyo.



dar es salaam - Tanzania Non-Government Organisation [NGO ...
UrlAdvisorGoodImage.png

Tanzania Non-Government Organisation [NGO] - National Coordination

Tanzania Non-Government Organisation [NGO] - National Coordination
 
Back
Top Bottom