Tanzania Nchi Yetu Sote
JF-Expert Member
- Mar 12, 2017
- 505
- 871
NAITAFAKARI ZAMANI YETU NA LEO YA WATOTO WETU.
Asubuhi kumekucha nipo kwenye gari la mwendo kasi naenda mjini kwenye mihangaiko yangu ya maisha ya kila siku. Kwa bahati nzuri nimefanikiwa kupata siti ya kukaa baada ya kusukumana na abiri wenzangu tuliokuwa tunagombania pamoja kupanda gari hili linaloelekea gerezani kariakoo. Baada ya kuketi kwenye kiti na gari kuanza safari yake kuinua macho yangu kwa mbele namuona Mama mtu mzima mwenye umri usiopungua miaka sabini mpaka themanini kasoro akiwa amesimama kwa kujikunja kutokana na uchovu wa utu uzima wake huku chini yake akiwa ameketi binti wa sekondari mwenye makadirio ya kuwa kidato cha tatu au cha nne akiwa anabonyeza bonyeza simu yake ya smart phone hana habari wala hofu ya kumpisha bibi yake mwenye uchovu wa uzee akae. Moyo wangu ukashituka kwa fadhaa na huruma nikijikuta namwita yule Mama mtu mzima kwa sauti ya upole "Mama njoo ukae hapa" yule Mama mtu mzima akanionesha uso wa tabasamu kisha akasogea nikampisha akakaa na mimi nikasimama. Kwa bahati mbaya hakuna hata abiria mmoja aliyediriki kumkosoa au kumuelimisha yule binti kwa kile kitendo alichokifanya kila mmoja alikuwa bize na simu yake na wengine wakipiga soga za hapa na pale. Tulimuacha binti aendelee kujilea mwenyewe sisi si jukumu letu tena, tunawaacha watoto wetu walelewe na smart phone, walelewe na mitandao ya kijamii.
Wahenga walisema "Ukiona kivuli kimepinda, basi ujue na mti nao umepinda" usihangaike kutafuta sababu za kupinda kwa kivuli.
Baada ya kupita kwa tukio hilo lenye aibu usoni mwangu safari yangu ikagubikwa na mawazo mithili ya mtu aliyepata msukosuko wa ajali. Niliingia kwenye ulimwengu wa fikra nikaanza kuikumbuka zamani yetu na mustakabali wa leo ya watoto wetu.
Nikaanza kukumbuka namna ya zamani watoto walivyokuwa ni mali ya jamii nzima. Kila mtu alikuwa na wajibu wa kumkanya na kumrekebisha mtoto pale anapokosea.
Kulikuwa na mfumo mzuri wa malezi kuanzia kwenye ngazi ya familia mpaka kwenye jamii iliyotuzunguka, mtoto alichukuliwa kuwa ni mtoto wa jamii ivyo jamii ilimlea kwenye kila kona alipopita hawakumuacha mtoto ajilee mwenyewe kama ilivyo leo.
Kwenye ngazi ya familia kulikuwa na mfumo mzuri uliomuandaa mtoto awe na nidhamu, pia awe mtu mwema kwenye jamii yake. Mtu atakayebeba huruma na unyenyekevu kwenye kila hatua ya maisha yake.
Zamani yetu watoto wote wa familia moja tulikuwa tunakula kwenye sahani moja na pia tulikuwa tunakula pamoja na wazazi wetu hii ilisadia kuimarisha upendo na umoja miongoni mwetu pia Baba au Mama aliweza kugundua makosa mbalimbali juu ya ulaji wako au kisirani chako au kama kuna chuki au ugomvi miongoni mwenu ivyo aliweza kuwakanya hapo hapo nanyi mkabadilika tabia. Lakini ya watoto wetu wazazi hawana tena mfumo huu wa malezi bali kila mtoto ndani ya familia anakula katika sahani yake peke yake, kila mtu anapakuwa chakula kilichopo kwenye chombo maalum cha kuhifadhia chakula kisha kila mmoja anakimbilia upande wake. Mwengine ataenda kulia barazani, mwengine uwani, mwengine chumbani na mwengine sebuleni hapa tayari mfumo wa leo unalazimisha kuwatenganisha watoto, hawatoweza kuwa na umoja tena kama zamani, upendo unapotea kama mawingu angani na chuki zitaanza kuchipua kama nyotera ya viazi miongoni mwao.
Naikumbuka zamani yetu, naionea huruma leo ya watoto wetu.
Zamani wazazi wetu walitulea wenyewe, tulilala nao wenyewe, walituogesha wenyewe, walitupikia na kutupakulia chakula wenyewe. Lakini leo ya watoto wetu hali imebadilika watoto wanalelewa na madada wa kazi, wanalala na madada wa kazi, wanaogeshwa na madada wa kazi, wanapikiwa na madada wa kazi, wanavalishwa na madada wa kazi. Kwa tafakari rahisi leo hakuna malezi watoto bali watoto wetu wanajilea wenyewe. Hakuna tena upendo kati ya mzazi na mtoto ndiyo maana mtoto wa leo hawezi kumheshimu mtu mzima yoyote atakayekutana naye popote pale. Jukumu la mzazi limebaki kwenye kununua chakula na kulipa ada ya mtoto tu lakini kwenye malezi tumewaacha watoto wajilee wenyewe. Najiuliza iko wapi zamani yetu? Leo ya watoto wetu inasikitisha mwana kwetu.
Zamani ya kwetu familia na ndugu wa ukoo walikuwa wanatembeleana kila msimu wa likizo au kwenye shida na kwenye matukio mbalimbali hii ilisaidia kuongeza umoja na upendo miongoni mwa familia na ukoo kwa ujumla. Lakini leo ya watoto wetu haina upendo tena kwakuwa kila mtu amekuwa mbinafsi hataki kuwa karibu na jamaa zake kwa kigezo cha maisha magumu au kubanwa na kazi. Hali hii imechangia kutenganisha watoto wa ukoo mmoja, hakuna tena upendo miongoni mwao hakuna tena kutembeleana, hakuna tena kupeana pole kwa wagonjwa, hakuna umoja wala mshikamano, chuki na kibri zimeongezeka miongoni mwao. Watoto wa leo tumewaangamiza sisi wenyewe.
Zamani yetu kwenye jamii ni ngumu kumpita mtu mzima bila ya kumsalimia au bila ya kumsaidia mzigo alioubeba hatosubiri kumwambia Mzazi wako bali atakuadhibu yeye mwenyewe hapo hapo. Lakini leo ya watoto wetu imekuwa mzoga wa mbwa yaani inanuka. Ni jambo la kawaida sana watoto kuwapita watu wazima huku wakiwaangalia kwa dharau na kebehi, hata pengine kuwapiga vikumbo hauwezi kumgusa mtoto wa mtu anaweza kukutukana matusi ya nguoni au akakurushia hata mawe. Tatizo hili tumelitengeneza kwa mikono yetu wenyewe kwani zamani wazee wetu waliwezaje kutulea kimaadili na sisi leo tunashindwaje kuwalea watoto wetu kimaadili? "Mwiba hutokea ulipoingilia" tunaweza kuwatekebisha watoto hawa bado hatujachelewa.
Zamani yetu watoto wa mtaa mmoja au kijiji kimoja kila siku jioni tunakutana kwenye uwanja wa kijiji tunakutanishwa pamoja na michezo ya kijadi inayojenga afya na kuimarisha akili kama vile kombolela, kidari poo, tunachora, tunaimba, tunacheza michezo ya kulenga shabaha, mpira wa miguu na kukimbia riadha hii ilisaidia kuongeza umoja na mshikamano miongoni mwetu. Lakini leo ya watoto wetu imekuwa tofauti sana kwani watoto wa kizazi hiki wanacheza michezo yao kwenye computer na simu za mkononi. Wanakutanishwa na mitandao ya kijamii kama ya whatsapp, instragram na facebook kwa kupitia simu zao za mkononi. Hawachezi pamoja tena bali muda wote wapo kwenye mitandao ya kijamii wanaongelea mapenzi, fitina, chuki, majungu na kuibua migogoro isiyo na maana katika jamii. Hakuna upendo tena miongoni mwao, hakuna umoja tena kila mmoja anachagua rafiki yake kwasababu zake. Naendelea kujiuliza ipo wapi zamani yetu, na ni kweli tumeikubali leo ya namna hii ya watoto wetu?
Zamani yetu nakumbuka wavulana walipelekwa jandoni na wasichana walipelekwa unyagoni huko kila jamii ilikuwa na mila na tamaduni zake za namna ya kutoa mafunzo na malezi kwa watoto. Kulikuwa na mafundisho ya kila namna kwa watoto kwa mfano walifundishwa jinsi ya kuishi na watu, shughuli za uchumi, tabia njema, mapishi, malezi ya watoto na kila jambo jema. Lakini leo ya watoto wetu imepoteza muelekeo. Mtoto apelekwi jandoni au unyagoni tena kwani zinaonekana ni mila za kishenzi zilizopitwa na wakati bali anapelekwa kwenye jumba la sinema na baharini kuogelea. Hapewi mafunzo tena bali anafundishwa ubinafsi na majivuno.
Ipo wapi zamani yetu? Bado naitafuta
Mwisho namalizia kwa kusema kwamba, naitamani zamini yetu ndiyo iwe leo ya watoto wetu. Tuwapende watoto wetu lakini upendo wetu usizidi kipimo, tuwadhibiti katika matumizi yao ya simu za mkononi pamoja na mitandao ya kijamii, tuwaelimishe kuwaheshimu watu wa rika zote wakubwa kwa wadogo, tuwe nao karibu mara kwa mara hii itasaidia kugundua maovu yao na mwenendo wa tabia zao kiujumla. Sisi kama jamii tuna wajibu wa kuwalea watoto hawa. Kila mtu ni mzazi hata kama bado haujabarikiwa kupata mtoto lakini ni lazima tushirikiane katika kidhibiti vitendo vya utovu wa nidhamu vinavyofanywa na watoto wetu.
Leo ya watoto wetu haina maana, kuirudisha zamani yetu inawezekana.
Mimi na jamii