Nitaenda kushiriki mazishi ya Regia Mtema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nitaenda kushiriki mazishi ya Regia Mtema

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JoJiPoJi, Jan 14, 2012.

 1. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2012
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  Ni zaidi ya msiba
  ....tulishirikiana kwa kila hali, ninasitisha kila kitu kwa ajili ya kuhitimisha safari ya mwisho ya dada yetu mpendwa.
  bila shaka mazishi yatafanyika kwa mkuya ifakara mjini.
  pia tunaweza kufanya utaratibu wa kutuwezesha members wa jf kuhudhuria mazishi
  mungu aiweke roho yake mahali pema peponi
  AMIN
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kwa hapa dar msiba ni wapi wandugu? ie watu wanakusanyika wapi hapa dar
   
 3. vengu

  vengu JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 518
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 60
  Na mimi pia,naelekea msibani!
   
 4. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wana JF Morogoro watuwakilishe! Mungu awatie nguvu katika mpango mzima wa kwenda kumhifadhi mwenzetu! Glory be to GOD
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,255
  Likes Received: 19,383
  Trophy Points: 280
  tabata kwa baba yake
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,545
  Likes Received: 18,194
  Trophy Points: 280
  Joji Poji, kwanza nafarijika sana na uamuzi wako kushiriki mazishi, mpaka sasa ni wewe tuu ndio huenda ukawa mwakilishi wetu wa jf kwenye mazishi yake.

  Hivyo kama unaweza kunipa rough logistics ya Ifakara niingie kwenye timu ya uhamasishaji jf tuwakilishwe accordingly!.

  1. Kwa kuanzia kuna umbali gani Moro- Ifakara na hali ya barabara ikoje?.
  2. Wana jf wenye uzoefu wa transportation, rough estimates za kukodi hiece/coster/basi kubwa mpaka ifakara zikoje?.
  Leo mchana nilimpa Max ushauri huu ufuatao:

  Mkuu Max, kwanza pole kwa msiba huu.

  Pili samahani hii thead ndio naiona sasa.

  Ushauri wangu wa kwanza, msiba ni public issue hivyo please open this gates ili tunapojadili jf tufanye nini kuhusu msiba huu, discussion isiwe restricted, let it open kwa member wote wa jf kutoa maoni yao!.

  Pili iundwe kamati ndogo ya on line kuratibu mapendekezo ambayo itafuatiwa na physical implementation.

  Mapendekezo yangu
  1. Kuwauliza wana jf wenye nafasi kushiriki msiba huu tangu nyumbani Tabata, heshima za mwisho Karimjee na hadi wenye nia ya kuhudhuria mazishi Ifakara.
  2. Wazo la utambulisho kwa T-shirt is ok kwa wale walioko tayari kujulikana, wasio tayari waruhusiwe kujumuika wakiwa hivyo hivyo bila kujulikana.
  3. Kwa watakaoweza kusafiri, yafanywe makisio ya kukodi gari kwenda na kurudi ili kijua kila anayetaka kusafiri angalau achangie kiasi gani ila kwa Ifakara kwenda na kurudi haiwezi kuzidi 50,000 per person.
  4. Tukishapata idadi ya wenye nia ya kusafiri bila kutegemea uwezo ni wangapi na kupiga hesabu ya ni wangapi wanaweza kuchangia huo usafiri, mathalani wenye nia ni watu 120 lakini wenye uwezo ni watu 60, hii inamaanisha tutahitaji kukodisha mabasi mawili ya watu 60 kila moja.
  5. Kati ya mabasi hayo moja litalipiwa na wanajf watakao jilipia na jingine litalipiwa na wanajf wengine wote ili kuwadhamini hawa wanajf wengine wenzetu wenye nia lakini hawauwezo wa kuchangia gharama.
  6. Mabasi hayo yatabandikwa stika za jf na zile barners za Regia to provide jf visibility. Wahusika au watavaa t-shirt au hata kushika vibendera tuu vya picha ya Regia Jf member!.
  7. Mwana jf mmoja mwandamizi atateuliwa kuwa mkuu wa msafara ambae ndie atakabidhiwa ile michango ya rambirambi.
  8. Tutamuomba mwana mmoja miongoni mwa hawa mahiri wetu prefarably Mzee Mwanakijiji kutuandikia eulogy ya Regia hata lile shairi lake linaweza kuwa part ya hiyo eulogy.
  9. Kinadada kwenye kamati hiyo washughulikie mashada prefarably shada moja kubwa litakalo kuwa limndikwa jf.
  10. Jf nasi totoe press release yetu yenye salaam za rambirambi kwa Chadema, Bunge, na wanafamilia kwenye press release hiyo tuweke alipojiunga, jumla ya thread zake na jumla ya posts zake na tukimalizia ule mstari wa post thread yake ya mwisho aliotuagia ikiwemo kuwaomba msamaha aliowakosea.

  Binafsi sitakuwepo Dar ila nitashiriki kikamilifu kutoa logistic support.

  Pasco.
   
 7. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,041
  Likes Received: 6,479
  Trophy Points: 280
  RIP my baby.
   
Loading...