Nitaanzia hapa endapo nitakosa fedha za kununulia nyumba ya kupangisha mwaka 2023

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Ili niweze kujenga utajiri kupitia uwekezaji kwenye ardhi na majengo ninatakiwa kujihusisha na;-

✓ Umiliki wa ardhi na majengo.

✓ Au Utoaji wa huduma za uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Njia ya kutengeneza kipato cha haraka na kipato endelevu nikiwa umelala ni kumiliki ardhi za kukodisha au nyumba za kupangisha.

Lakini umiliki wa ardhi au nyumba unahitaji niwe na mtaji fedha. Baadhi ya benki wanaweza kunipa mkopo wa kununulia nyumba ya kupangisha yenye kipato chanya (positive cashflow).

Lakini kwa mazingira yetu yenye changamoto kubwa ya sera nzuri za uwekezaji kwenye majengo ya kupangisha, imekuwa vigumu sana kupata nyumba inayokidhi vigezo vya kuombea mkopo wa majengo kutoka benki.

Njia hizi 3 sio njia za mkato za kupata mtaji fedha wa kumiliki nyumba ya kupangisha. Hivyo ninahitaji uvumilivu. Lakini ni njia za uhakika, endapo nitaendelea kuwa kwenye mchakato sahihi.

Hivyo moja ya maeneo matatu ambayo nitaanzia ili kufikia lengo la kujenga utajiri kupitia ardhi za kukodisha au nyumba za ni kama ifuatavyo;-

✓ Moja; Kumiliki mtandao wa mauzo ya viwanja, mashamba na majengo.

✓ Pili; Kutoa huduma za udalali wa viwanja, mashamba na majengo.

✓ Tatu; usimamizi wa nyumba za kupangisha.

Njia zote hizi 3 ninaweza kuzifanya kwa wakati mmoja kwa zinaendana sana katika utoaji wa huduma zake. Lakini hizi njia zote 3 ninatakiwa nizifanye kwa muda wa ziada kwa sababu mwanzoni zinaweza kukidhi kunipatia mahitaji yangu ya msingi kama binadamu.

Mafanikio ya kusimamia nyumba za kupangisha na udalali wa ardhi na majengo hayatagemea sana mitandao ya kijamii kwa miezi ya mwanzo wa huduma zangu.

Hii ni kwa sababu katika mji ninaoishi ninazungukwa na kundi kubwa la wateja wanaohitaji huduma za udalali na huduma za usimamizi wa nyumba za kupangisha.

Kwa mwanzoni, nitalazimika kufanya kazi nyingine ili niweze kula, kuvaa na kupata mahali salama pa kulala. Lakini huduma zangu hizi tatu zikianza kukua nitalazimika tena kuacha kazi yangu ya kunipatia chakula, mavazi na kodi ya chumba.

Hutaji Kuu Kutoka Kwenye Moyo Wangu.

Ninajua njia ya kujenga utajiri haitakuwa rahisi. Itakuwa ni njia ngumu. Nimechagua njia ambayo jamaa zangu wanaweza kujiona chizi.

Nimeamua kutangaza kupambana dhidi ya adui umaskini ambao pengine umetoka kwa babu zangu bila kuvunjwa mnyororo wake.

Mimi leo nimeamua kubeba jukumu hili. Njiani nitaongoza na wasaidizi wangu, ndugu zangu, marafiki zangu wa kike na kiume, na wengineo.
Lakini nafsi yangu ndiyo ijuavyo jinsi ambavyo nimejitolea kupambana na adui huyu umaskini kwa moyo wote.

Hii ewe imani usiondoke moyoni mwangu. Inawezekana kujenga utajiri kupitia uwekezaji kwenye ardhi na majengo kwa kuanzia hapa nilipo.

Hivyo, nitatumia simu yangu kuwafikia wateja wangu wa huduma za udalali wa ardhi na majengo na huduma za kutangaza mauzo ya ardhi na majengo.

Njia Za Kukusanya Mtaji Fedha.

Moja.

Kujenga mtandao mkubwa wa mauzo ya ardhi na majengo.

Kwa Tanzania yetu hii ni fursa kubwa. Kwa sababu hakuna hata mtandao mmoja ambao unajina kitaifa wa kutangaza mauzo ya ardhi na majengo. Nitawekeza nguvu kwenye mkoa ninapoishi ili niweze kuwafikia watu ambao watanufaika na huduma zangu za kidigitali mapema zaidi.

Ninaiahidi nafsi yangu kuwa mwaminifu ili wateja wangu wachache wa mwanzo wawe wananiongelea vizuri. Kwa kuwa mwaminifu na kutoa huduma bora ya kukidhi mahitaji ya mteja wangu ni njia pekee ya uhakika ya kulinda wateja wa zamani na kuongeza idadi ya wateja tarajiwa.

Nitatumia mitandao mikubwa ya watu maarufu wenye wafuasi wengi. Hii ni kutokana na nilivyojifunza kutoka kwenye kitabu kiitwacho The Art and Business Of Online Writting.

Nitatumia mitandao yao kwa uadilifu kwa uadilifu ili kuepuka kujenga picha mbaya ya kwanza (bad first impressions).

Kwa kutumia kanuni ya mwana uchumi wa kiitalia Vilfredo Pareto isemayo kuwa matendo machache ufanyayo ndiyo huchangia mafanikio yangu kwa 80%. Hivyo basi, nitawekeza nguvu kubwa, muda mwingi na maarifa mengi kwenye mitandao miwili tu;-

✓ Mtandao wa facebook na.

✓ Mtandao wa whatsapp.

Kupitia mitandao hii nitawakusanya wafuasi wangu pamoja. Hivyo, kile nitakachowashikisha wakiwa pamoja kitakuwa na thamani kubwa sana ukilinganisha na kumshirikisha mfuasi mmoja au wafuasi wachache.

Mtandao wa facebook unafaa sana kwa ajili ya kuwafikia watu ambao hatufahamiani kabisa. Lakini mtandao wa whatsapp utanifaa zaidi kwa

Mitandao mikubwa ambayo ninaweza kuanzia kushirikisha huduma zangu ni kama ifuatavyo;-

✓ JAMIIFORUMS.

✓ Kurasa za watu wenye wafuasi wengi.

Nitakuwa nikitoa thamani kubwa sana kwa wafuasi wangu kiasi kwamba kuacha huduma zangu ninazowapa bure ni kitu ambacho hawataweza kuvumilia.

Jina La Mtandao Wangu Wa Mauzo Ya Ardhi Na Majengo.

Jina la mtandao huu ni lazima ufafane kwa mitandao yote ya kijamii kuanzia facebook, whatsapp na instagram (kwa baadaye). Hii ninayo itaongeza kasi ya kufahamika haraka na wafuasi wapya wa mitandao yangu.

Mfano; Jina la makundi ya whatsapp itakuwa ni UZA VIWANJA/NYUMBA. Jina la ukurasa wa facebook litakuwa ni UZA VIWANJA/NYUMBA. Jina la kundi la facebook litakuwa ni UZA VIWANJA/NYUMBA. Jina la ukurasa wa akaunti ya instagram litakuwa ni UZA VIWANJA/NYUMBA, hii itakuwa ni baada ya kukuza mitandao ya facebook na whatsapp.

Nitajifunza kutoka kwa wabobezi wa mitandao ya kijamii akiwemo MR.AKILIKUBWA. Huyu ndiye muanzilishi na mkurugenzi wa kampuni ya AKILIKUBWA COMPANY.

Ninaamini ndani ya miezi nitakuwa nimefikia wafuasi zaidi 1,000 kwenye makundi ya whatsapp. Hii itakuwa rahisi kutokea ikiwa nitafuata maarifa adhimu ya ukurasa huu.

Njia ya pili nitaendelea kwenye makala ijayo. Tafadhali nishirikishe chochote kuhusu makala hii. Je umekugusa kwa kiasi gani?. Naomba uwe rafiki yangu ikiwa umechagua kupambana na adui umaskini kupitia uwekezaji kwenye ardhi na majengo na huduma zake.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Attachments

  • flyerdesign_18122022_064916.png
    flyerdesign_18122022_064916.png
    29.7 KB · Views: 17

ni mbinu ambayo niliitumia na kufika hapa nilipo leo but kutengeneza hyo connection na loyal customer's haichukui chini ya mwaka mzima for daily activities.

ukisema uifanye huku unachanganya na shughuli zako inaweza kukuchukua mpaka miaka miwili japo mie nilianza na kuifanya kwa shughuli nyingine
 
Nashukuru sana rafiki.

Nimetukutumia ujumbe kule inbox.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom