NIT: Serikali yaanzisha kozi za Marubani na Wahandisi wa Ndege

jerrytz

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
5,975
4,264
Serikali ya Tanzania imeanzisha kozi maalumu kwa ili kufundisha Marubani na Wahandisi wa ndege(Aircraft Engineers) katika chuo cha Usafirishaji (National Institute of Transportation) katika kusaidia kupata wataalamu kwa shirika la ndege la Tanzania (ATC) ambalo linakuzwa ili kuwa miongoni mwa mashirika makubwa ya ndege duniani.
Akizungumza Katibu mkuu wa wizara husika amesema kuwa Tanzania ina uhaba wa wataalamu katika sekta ya masuala ya anga na uhandisi katika matengenezo ya ndege.
"Hivyo basi kozi hizo maalumu zitasaidia kutoa wataalamu watakaofanya kazi katika shirika hilo".

Kwa habari zaidi soma The Guardian la tarehe 9 Jan 2017
 
Good news ingawa tumechelewa sana wenzetu walianza zamani

Ila pongezi sana kwa hatua moja mbele......

Government names 19 institutions approved to offer aviation courses
Serikali ya Tanzania imeanzisha kozi maalumu kwa ili kufundisha Marubani na Wahandisi wa ndege(Aircraft Engineers) katika chuo cha Usafirishaji (National Institute of Transportation) katika kusaidia kupata wataalamu kwa shirika la ndege la Tanzania (ATC) ambalo linakuzwa ili kuwa miongoni mwa mashirika makubwa ya ndege duniani.
Akizungumza Katibu mkuu wa wizara husika amesema kuwa Tanzania ina uhaba wa wataalamu katika sekta ya masuala ya anga na uhandisi katika matengenezo ya ndege.
"Hivyo basi kozi hizo maalumu zitasaidia kutoa wataalamu watakaofanya kazi katika shirika hilo".

Kwa habari zaidi soma The Guardian la tarehe 9 Jan 2017
 
Great Joke in 2017 found early on the 9th day of the year lol! kwa hizi ndege 7 zilizonunuliwa?
 
Lengo ni zuri, ila nashauri kuwa, Wale vijana waliofaulu vizuri kabisa masomo ya PHYSICS, MATHEMATICS nk. kwa alama "A" wachukuliwe wasomeshwe bure kozi za urubani na Uhandisi wa Ndege, tukisomesha vijana kama 300 hivi tukawalipia kila kitu, nchi itakuwa na marubani na wahandisi wengi sana wa maswala ya ndege, kwani Tanzania inashindwa kutenga kila mwaka Bilioni 16 za kusomesha hao wataalamu?

Tunaweza pia kuwaita wakufunzi wataalamu wa urubani waje wawafundishe hapa hapa nchini, na tunaweza kununua ndege nyingine kwa ajili ya kufanyia mafunzo kwa vitendo, Kupanga ni kuchagua, msidhani Nchi nyingine ziliamka asubuhi na kufika hapo zilipo siku hiyo hiyo.
 
Nimeipenda hii,nadhani hata gharama za mafunzo zitakuwa chini hivyo kuwavutia vijana wengi kwenye hiyo fani.
 
Great Joke in 2017 found early on the 9th day of the year lol! kwa hizi ndege 7 zilizonunuliwa?
Mkuu hizo kozi hapo chuoni zilikuwepo kwenye mchakato hata kabla ya wazo la bombardiers, ndio maana nikashangaa kuna siku Mh Rais alishangaa NIT kua chuo kikuu, nikagundua hakukitembelea hivi karibuni kujua kinaendelea na mikakati gani ya ndani na nje.
 
Great Joke in 2017 found early on the 9th day of the year lol! kwa hizi ndege 7 zilizonunuliwa?
Litakuwa ni jambo la kusikitisha iwapo tutafikiri kuwa tunasoma ili tuajiriwe na Serikali. Aidha hatutakuwa tunafikiri nje ya box iwapo tutasoma ili tupate ajira hapa nchini tu. Kwa sasa inatakiwa tufikiri kufanya kazi nje ya nchi ili tulete remittances zijenge nchi yetu.
 
Lengo ni zuri, ila nashauri kuwa, Wale vijana waliofaulu vizuri kabisa masomo ya PHYSICS, MATHEMATICS nk. kwa alama "A" wachukuliwe wasomeshwe bure kozi za urubani na Uhandisi wa Ndege, tukisomesha vijana kama 300 hivi tukawalipia kila kitu, nchi itakuwa na marubani na wahandisi wengi sana wa maswala ya ndege, kwani Tanzania inashindwa kutenga kila mwaka Bilioni 16 za kusomesha hao wataalamu?

Tunaweza pia kuwaita wakufunzi wataalamu wa urubani waje wawafundishe hapa hapa nchini, na tunaweza kununua ndege nyingine kwa ajili ya kufanyia mafunzo kwa vitendo, Kupanga ni kuchagua, msidhani Nchi nyingine ziliamka asubuhi na kufika hapo zilipo siku hiyo hiyo.
Mkuu, Urubani wa ndege hauhitaji A za Physics au Mathematics ..................!!
 
Hahahahah Mkulu ameshasema hiki sio Chuo, na ameshangaa eti kuwa NIT nao wanatoa degree. Sasa leo akisikia kuwa wanatoa Course hizo si ndio atakifunga kabisa??? Nimeuliza tu kwa nia njema
 
Back
Top Bottom