Nissan X-Trail

njiwa

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
12,046
2,000
Mkuu wacha niku add kwenye phone book yangu hembu fanya nipate namba yako nipo dar mm ni fundi umeme wa magari huwa nakuja sana moro..

Ishu ya nissan kwa upande wangu nilikuwa na mpango wa kuanzisha club au group la nissan.

Tena nawafanyia golo kwa watakao taka wawe wanaweza kuifanyia diagnosis popote pale watakapo kuwa dunian iki mkadi wawe na smartphone yao tuu tatizo likiwa kubwa nawapimia mm hata wakiwa nje ya nch na gari.

Juu ya dpf isikutishe sana.ukijua matumizi yake harafu wazungu sio wajinga sana dpf huwa wanaweka batan ukibonya inajisafisha yenyewe ishu ni kuwa wengi huwa hawajui na hawafanyi hivyo.

All in all solution yake ipo ikiziba inatolewa na kuidelet dpf kwenye control box mambo yana songa

Bro hilo group limefikia wapi
 
päiva

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
230
250
Habari za Leo, nahitaji kununua brake pads na CV joints za Nissan Xtrail NT31 ambazo ni nzuri, nitazipata wapi?, na bei zikoje?
 
njiwa

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
12,046
2,000
Habari za Leo, nahitaji kununua brake pads na CV joints za Nissan Xtrail NT31 ambazo ni nzuri, nitazipata wapi?, na bei zikoje?

Kariakoo duka linaitwa Master card karibu na salama bearing huyu ana spare originally za nissan
 
Valuer Mollel

Member
Aug 4, 2019
5
20
Vipi WanaJamii
Leo tuna 'real-life situation'. Gari letu hili la X-Trail likanipata ofisini na tatizo la kelele toka blower ya Climate Control - yaani feni ya ndani au kiyoyozi kikiwashwa kunakua na kelele hasa ukipiga kona upande wa kushoto.

Gari letu lilikua limesha badilishwa blower motor na nyingine used sio zaidi ya miezi tatu iliyopita. Mmiliki gari alikua anaelewa issue ni ipi pale, wakati huu alitaka a "permanent solution". Hivyo basi alipiga simu kwa wakala na akauliza bei ya blower mpya. Aliyesema 'Pride comes before a fall' labda alikua ameshaona kwa ndoto ile arrogance ya jamaa wangu.

Alipopewa bei yake, both in dollar and Tshs na pia kiasi cha deposit required, jamaa alinywea na kaagiza Mountain Dew baridi sana! Kwa kweli hata sasa hajanidokezea aliyopata pale, bei na nini, ila tu itabidi iagizwe toka nje na itachukua wiki tano, basi tu!
Kwa problem yetu basi - ile blower ilikua imemaliza bushes zake, ndio bushes sio bearings. Design yao ni kutumia pre-greased porus bushes kabla ya bearings. Udhaifu wa hii design au bush zenyewe ni kwa mda zalika kiupande sababu ya uzito wa motor ikitembea nje ya axis of rotation sababu ya movement ya gari - kama pale inavyopiga kona.

Kwa kulielewa tatizo liko wapi na la sababishwa na nini, tuliweza kupata ile "permanent solution" mteja wetu aliyotaka. Hadi leo Climate Control yatumika kama kawaida na bila kelele yeyote.

Toleo lililofata la X-Trail linatumia blower motor design tofauti na isio na udhaifu huu. Mambo mengine hayawezi onekana kwenye design au initial stages za kifaa/chombo, lazima kipitie matumizi na mazingira mengi ili kuonekana ustadi au udhaifu wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bro. Ofisi zako ziko wapi?
 
Valuer Mollel

Member
Aug 4, 2019
5
20
Mkuu wacha niku add kwenye phone book yangu hembu fanya nipate namba yako nipo dar mm ni fundi umeme wa magari huwa nakuja sana moro..

Ishu ya nissan kwa upande wangu nilikuwa na mpango wa kuanzisha club au group la nissan.

Tena nawafanyia golo kwa watakao taka wawe wanaweza kuifanyia diagnosis popote pale watakapo kuwa dunian iki mkadi wawe na smartphone yao tuu tatizo likiwa kubwa nawapimia mm hata wakiwa nje ya nch na gari.

Juu ya dpf isikutishe sana.ukijua matumizi yake harafu wazungu sio wajinga sana dpf huwa wanaweka batan ukibonya inajisafisha yenyewe ishu ni kuwa wengi huwa hawajui na hawafanyi hivyo.

All in all solution yake ipo ikiziba inatolewa na kuidelet dpf kwenye control box mambo yana songa
Asante kwa swali zuri sana Bw. Galindas. CAT converter ni kifaa kinacho nasa gesi na chembechembe haribifu kwa mazingira na kuziangamiza kw kuzichoma na kuzichanganya zikawa safi(harmless). Mle ndani kuna madini yanayosaidia katika shughuli hii, na pia muundo wake ni maalum kunasa chembechembe zile na kuzipika kwa joto la juu.
Tukilinganisha mfumo huu na kichujio, kwa hii ndio mmoja ya kazi yake, tutaona kua kuna uwezekano wa mfumo kuziba. Engine ikichoma mafuta mengi kupita kiasi, moshi hasaa carbon uzidi na kuziba mfumo. Kuliwasha gari ukiwa umekanyaga mafuta au kulipa mafuta linapowaka ni mwiko kw magari yaliyo na mifumo hii.
Magari ya Xtrail yanatumia mifumo electronic ya mafuta na kwa hivyo tatizo kidogo laweza leta majanga. Mfano, taarifa kuhusu jiko(combustion) kutoka kwa oxygen sensor zikikosa, injector umwaga mafuta mengi na kuzidisha carbon.
Kwa sababu ya i) madini nadra yanayotumika kuzitengeneza mifumo ya CAT converter na DPF, ii) sheria kali za kulinda mazingira hasaa ulaya na nchi zilizoendelea na pia iii) soko la kununua CAT/DPF mbovu mbovu ili kuvuna yale madini, mifumo hii ina bei sana mpya au used. Ile ya Xtrail niliinunua laki nane!
Mkuuuu weka Mawasiliano Yako Tukutafute. Unatoa Madini mpaka Raha Yani. Daaaah we Jamaaa unajua mpaka kero yani.. Hongera Bro.
 
Valuer Mollel

Member
Aug 4, 2019
5
20
Vipi WanaJamii

Kwa mda mfupi nliliokua hapa nimeona wengi wakilalamika kuhusu gari hizi za Nissan. Kweli kila mtu ana haki na uhuru wa maoni/mawazo yake ni muhimu kufanya maamuzi na kua na mawazo ya ukweli na kamilifu. Kwa hili, nimeona nianzishe uzi huu ambao utakua ni wa kuhoji na kuangalia kwa kina gari hili la Nissan.

Gari hili liko kwenye toleo la tatu sasa na hii ni kudhihirisha umaarufu wake na kupendwa kwake ulimwenguni mzima. Lisingalikua zuri na bora, lisingalinunuliwa kwa wingi na kwingi hivyo. Wala sidhanii mJapan/Nissan angaliendelea kulitengeneza na kuliboresha kwa miaka karibia ishirini. Hapa hapa nchini kuna wengi wanaapa kwa hili gari na sio matani, hata uumpe gari aina nyingine na hela juu hakuskii!
Basi shida iko wapi?

Gari hili ni la kisasa na lina tumia mifumo na teknolojia ya hali ya juu. Magari haya yanauzwa soko tofauti na lazima yazingatie sheria na kanuni za nchi au maeneo husika. Mambo haya mawili ni ya muhimu sana katika kuielewa gari hili.

Kwa minajili ya usalama, kuboresha na kutofautisha chombo chao, Nissan wametumia teknolojia za kisasa kw. mf. X-Trail ya diesel yawezakua na mfumo wa DPF, huu ni wa kumaliza gesi sumu kwenye moshi wa exhaust.

Engine hii utumia oili na ratba tofauti na ya kawaida kwa matunzo yake. Gari hili laja na transmission/gearbox ya manual(sawa kabisa) na automatic aina tatu; planetary, CVT na eCVT(hapo basi baharia). Bila kusisitiza zaidi mwaona hawa ni wanyama aina tatu labda wafanane kwa kua wanafungwa kwenye engine, shaft zatoka mle na hutumia mafuta ila sio sawa.

Gari la DPF usijaribu bidhaa na mambo ya uswazi.
Yani, mimi nina Nissan Xtrail 2008, nimeiagiza Juzi tu. But nimesikia watu wengi wanaziponda sana, na wengi wanalalamika kwamba hizi Gari tatizo Lake kubwa ni Ku chemsha. Sasa mimi ndo kwaaanza nimeanza kulitumia. Naogopa hili tatizo lisije likanitokea. Sasa nawaza ni precautions gani Nichukue ili gari langu lisije likapata hili tatizo la kuchemsha.
Kuna watu wananishauri nichomoe Thermostart ili maji yawe yana flow directly, alafu niongeze Njia kwenye Rejeta, lakini sasa naogopa je inaweza athiri mfumo wa Gari.? Naweza itumia hivi hivi bila kuathiri mfumo wake wa awali? What precautions should I take.? Naomba unishauri Mkuu, Asante sana
 
Boeing 747

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
3,283

Naomba nikuambie kitu, japo najua wenye Toyota zao watakuja kupinga, siwakatazi kupinga kwa sababu kila mtu ana uhuru wake...

Sikushauri utoe thermal start kama watu wanavyokushauri....Mjapan aliyeiweka si mjinga.

Hizo habari za kwamba Xtrail zina ugonjwa wa kuchemsha ni MYTHS tu ambazo watu wamekuwa wakiamini kwa sababu..

Nissan xtrail huwa halitaki kuweka maji ya bombani kwenye radiator, wabongo tunapenda urahisi wa mambo...unakuta mtu anamiliki vitz anaweka maji ya bombani, basi na kwenye x ttail anafanya hivyo....x trail iwekee coolant iliyopendekezwa... coolant hupooza gari kwa kiwango kinachotakiwa tofauti na maji ya bomba, kisima au mtoni.

Weka engine oil iliyopendekezwa na mtengezaji sana sana iwe 5w 30...kibongo bongo tunaamini zaidi Castrol au Total.....kumbuka oil mbali na kulainisha injini, pia hupooza injini..

Mara kwa mara hakikisha kiwango chako cha coolant hakishuki below the minimum level.

Kuna watu wapo wanamiliki x trail zaidi ya miaka 6 sasa, wameshafanya nazo masafa karibu mikoa yote na nje ya nchi mfano Kenya, Uganda bila kufanya modifications zozote kwenye engine....

Ingekuwa haya magari ni mabovu kama watanzania wanavyosema, Nissan Motors Corporation Japan wangeshasitisha uzalishaji wake...ina maana ni gari zinazofanya vizuri ndiyo maana uzalishaji wake unaendelea na sasa Nissan Xtrail wapo Generation ya tatu kama sikosei...

Mafundi wa Tanzania hawataki kusoma, wamezoea mifumo ya Toyota, hivyo wao ndiyo chanzo kikubwa cha kuwakatisha watu tamaa kwa upande wa xtrail....
Sisi watanzania ni watu wa ajabu..mtu akishindwa kitu hataki kukubali, anakiponda...mafundi wengi x trail zinawatoa jasho, kwa hiyo wanawadanganya watu hizi gari hazitengenezeki....

Kwa ninj zisitengenezeke, gari lina OBD, ni kiasi cha kusoma code na kuitafsiri inaashiria nini, then you do a replacement

Chonde chonde, x teail usiipeleke kwa mafundi makanjanja, mwembeni...ukihisi tatizo weka vipimo vya computer, replace parts with genuine ones......hapo x trail utaiendesha miaka 8 bila kujuta.
Siku zote usichukue experience ya utunzaji wa Toyota ukaihamiahia kwenye X trail..hapo utateseka...

Mwisho.....gari ni matunzo kwa kuzingatia instruction manul yake.....na si kwa kuzingatia maneno ya watanzania.
 
salari

JF-Expert Member
Jan 22, 2013
871
1,000

Mkuu inaelekea wewe una nissan kama hutojali na upo Dar toa mawasiliano ya mafundi wazuri wa nissan utakuwa umesaidia wengi sana
 
sakasaka

Senior Member
Feb 20, 2012
189
225

Je nitaijuaje coolant inayotakiwa kwenye nissan xtrail yangu?
Naomba jina la ya coolant unayotumia wewe kwenye xtrail yako.
Au coolant yoyote ile basi inafaa?
Au lazima niende nunua coolant kwa Nissan authorized agent ?

Asante
 
salari

JF-Expert Member
Jan 22, 2013
871
1,000
Je nitaijuaje coolant inayotakiwa kwenye nissan xtrail yangu?
Naomba jina la ya coolant unayotumia wewe kwenye xtrail yako.
Au coolant yoyote ile basi inafaa?
Au lazima niende nunua coolant kwa Nissan authorized agent ?

Asante
Mkuu sina gari hiyo ila nina uzoefu nayo kwa kuwa kuna ndugu yangu anayo na huwa naitumia mara kwa mara. Coolant inayotakiwa ni hiyo hapo chini. Aidha kumbuka xtrail ina engine parts ambazo ni aluminium hii ina maana kuwa ukichakachua coolant ukaweka ambayo haina viwango vinavyotakiwa basi ukipata majanga usilaum mtu na kumbuka Nissan Xtrail zina kawaida ya kuoverheat sanaaaaa incase hujafuata masharti yake. Kama upo Dar nenda duka linaitwa Mastercard, DT Dobie au kisangani utapata coolant original.

Summary download.jpg
Je nitaijuaje coolant inayotakiwa kwenye nissan xtrail yangu? Jibu Cheki manual ya gari lako zipo online au cheki picha chini
Naomba jina la ya coolant unayotumia wewe kwenye xtrail yako.Jibu Cheki manual ya gari lako zipo online au cheki picha chini
Au coolant yoyote ile basi inafaa? Jibu HAPANA weka ambayo NISSAN wamesema uiweke usijaribu kuweka nyingine
Au lazima niende nunua coolant kwa Nissan authorized agent ? Yes ili kuwa na uhakika halafu why ununue gari around 15M then uone ubahili kununua coolant nenda DT Dobie au Master Card au Kisangani ingawa nadhani Master Card bei yao itakuwa cheap kuliko hao wengine

download.jpg
 
Summary View attachment 1198672

View attachment 1198672
Shukrani mkuu
 
päiva

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
230
250
Habari wadau, nina Nissan xtrail ya mwaka 2008. Ikifika speed kati ya 40 na 60 gari inavuma sana na kuanza kutetemeka. Ila nikivuka hadi 80 mvumo unapungua kidogo. Je tatizo laweza kuwa nini?
 
G.T.L

JF-Expert Member
Jul 15, 2012
484
1,000
Huu uzi potential sana, nina mpango wa kuagiza Nissan X trail Axis
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom