Nissan X Trail aka Kimeo

Feb 10, 2017
98
316
1656925845461.png

Samahani kwa kuita gari yako pendwa Kimeo ila twende pamoja utanielewa huko mbele, Kaa vizuri andaa Juice yako bariiidii ule MADINI..
.
X trail ni moja ya SUV [compact crossover] ya Kijapan iliyoingia sokoni November 2000, Ikiwaa ni crossover SUV ya Kwanza kutoka Nissan. Nissan X trail mpaka sasa ina generation 4, Generation ya 1 ikianza [2000-2007] coded T30, Generation ya 2 [2007-2013] coded T31, Generation ya 3 [2013-2020] coded T32 na Generation ya 4 [2021- Leo] coded T33. Sasa kwa leo tutamgusa Generation ya 1 tu [T30].
.
1656925888885.png
1656925910161.png
1656925950301.png
1656925977845.png


Generation ya Kwanza alikuja Mwaka 2000-2007 akitumia platform za ndugu zake Nissan Almera na Nissan Primera. Alikuja na Engine option 4. Petrol Engine ikiwa na 2.0L QR20DE, 2.0L SR20VET turbo na 2.5L QR25DE, Pia kulikua na Diesel Engine ya 2.2L YD22DDTi.
.
Engine zote zikiwa ni Cylinder 4 zikiwa linked na 4-Speed automatic na 5&6-speed manual transmission, Gari ikiwa na option za 2WD na 4WD, Hiyo Turbocharged Engine ilikua special kwa GT models ikiwa na Hp 276 na Katika Generation 1 walitoa special Edition Auxi na Rider Autech.
.
Hizi zilikua na features za ziada kimuonekano na interiors, Kimuonekano gari iko vizuri exterior styling yake iko poa ikiwa na boxy shape inayotoa nafasi ya kutosha ndani kwa ajiri ya Abiria na mizigo na Upande wa Seats na Sehemu za miguu ziko poa miguu inakaa vizuri kabisa.
.
1656926144254.png
1656926161928.png
1656926198457.png

.
Seats ni high-quality fabric au optional leather upholster na unaenjoy ukiwa unaendesha hata abiria anaketi vizuri tu, Interior ina features kama waterproof ceiling, ina heater seat za mbele, Music sytem pia iko poa[standard], Iko na safety equipment kama dual airbags, brake assist, EBD [electronic brake distribution] na ABS.
.
Standard features zingine ni kama Headlights zake ni bright na clear halogen main na low beams, Auxiliary fog lamps, ina automatic climate control system. 2003 X trail walifanya face uplift kukiwa na minor changes kwa muonekano.

Walifanya mabadiliko kama kuweka option za pop-up steering system, Wakaweka hyper roof rail, carwing infotainment system na navigation system. X trail ninaweza sema ni gari moja inayokupa uwezo wa kupita off road vizuri na town pia ukawa unapiga misele yako town fresh tu.

Na hii ni kutokana na ground clearance ya kutosha na option za 4WD walizoipa, kwenye Mafuta gari inatumia wasitani wa 9.5Km/l-12.8km/L, Hii ni kwa zile za 2000-2002 [Hizi zinabwia sana mafuta], Kuanzia 2003 atleast zinaenda mpaka 14km/L Kutokana na maboresho waliyozifanyia.
.
1656926373949.png
1656926385481.png
1656926514397.png

.
Kama unapenda Generation ya 1 nakushauri anzia mwaka 2003 Kwenda Juu tena its much better kuagiza/Kununua ambayo haijatumika Bongo, Yani gari wewe ndo uanze nayo Maisha, Kwa hizi gari huwa siwashauri wateja wanunue za mikononi Sababu utaijua huko mbele we twende pamoja tu.
.
Ila kama ndo umeamua kununua mkononi basi jiridhishe na ujue historia ya hio gari vizuri isije ikakupa kimuhe muhe au mdondo kuhusu Maintanance za gari gharama ziko juu kidogo, vilainishi vyake bei iko Juu kidogo na ni muhimu kutumia vilainishi vyake [recommnded ones] tu ila ni affordble.
.
Parts nyingi ni genuine bei imesimama ukifunga ni mkataba unasahau, Wabongo wengi tunapenda gari ambazo hata usipoifanyia service au inatatizo bado itaendelea kupiga kazi tu, Kwa hizi X trail haziko hivyo unaweza i force lakini itakua swala la muda tu itakutoa kamasi.
.
Gari ina umeme mwingi na iko na sensor za kutosha [Kukuzimikia barabarani ni kawaida sana]. Unaweza ukawa zako barabarani ki sensor kikafa ikazima ghafla na Hapa kwenye sensor ndo huwa panakera sana sababu sensor zake baadhi zinawahi kufa na baadhi ya sensor zinaenda mpaka 200K.
.
Matatizo mengine common ya hii gari yanayokua reported ni kuchanganya oil na maji, Kuua gasket mapema na hii inatokana sana na malfunction ya thermostart kwenye engine inayosababisha block kupata joto sana.. . Sometime inasababisha na kuchemsha hasa ukiwa safari ndefu..
.
Hii issue ya gasket inasababisha na oil leaks kutokea kwenye cylinder head cover na sometime kuingia kwenye plugs. Sasa sababu ya tabia ya kulimbikiza matatizo Engine ya hii gari ikiaanza kusumbua Lazima Ilale tu na kuitengeneza ni gharama sana uki compare na SUV wa toyota..
.

1656926960254.png
1656927018829.png
1656927064470.png


X trail kukutoa 2M kwa ajili ya matengenezo tu ni kawaida sana, NI gari flani ipo delicate na kama sio mtunzaji na hauko vizuri kiuchumi bado uchumi ni things fall apart by chinua achebe haikufai. Watu wengi wameziagiza kwa mbwembwe bila kujua wakazinyima matunzo elekezi zikaanza kusumbua wakaishia kuzipark ndani au kuuza.
.
Ukitaka ku enjoy hii gari kwanza usiwe bahiri, Service usipitilize, kwa radiator hakikisha unatumia coolant sio maji ya mto Ruvu. na Engine zake ni za kisasa ukiona tatizo lolote nenda kwa fundi fanya diagnosis upate majibu Yani hata ukiona Muungurumo umebadilika au ina miss au kuna ki taa kimewaka kwenye dashboard mapema tu nenda kwa wataalamu wa diagnosis Waangalie shida nini then irekebishwe. Usitumie mafundi wa kubashiri matatizo atagusa vitu visivyokua na shida vingi tu atavi disturb bure..
.
1656927238926.png
1656927259854.png

.
All in All Nissan X trail ni gari nzuri kikubwa Ipende sana na itakupenda pia. Ipe inachositahili sio inachohitaji na hakika utaenjo hii gari, Inshort hii gari sio kimeo ila ukiinyima matunzo ni kimeo Kweri kweri. Bei kuagiza inaanzia 13M ++ kama unahitaji kuagiza au kununua showroom Tunaweza kuku assist on the same. .
.
Tunafanya kazi na dealers wa Japan, UK, Singapore na hapa nchini, dealers wanaotupa gari nzuri kwa ajili yako, Simpy bofya link [Samatime Cardealers] njoo whatsapp au ofisini Posta Phoenix House mkabala na Mkapa tower tutaku assist..
.
Kama uko mkoani na unahitaji kuagiza gari karibu pia, Utatupa hitaji lako tutakupa ushauri then tutakutumia options za gari ukishachagua utapewa invoice na utafanya malipo at cost [no extra cost] huko huko ulipo mpaka gari itafika na utakuja kuichukua au kuletewa ulipo..
.
Asante
Samatime Car Dealer Co Ltd
Get A smart car like You
Mob: 0714547598
 

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,528
15,046
tanzania asilimia kubwa ya mafundi wa nisani hawapo sawa na mafundi simu wa kariakoo na mikoani.

nisani inamfumo mwingi wa umeme na teknolojia ambayo ni ngeni kwa mafundi na hawa taki kusema ukweli ndio maana mafundi wanasingizia ni kimeo.

jiulize kwa nini range inamafundi wa kuhesabu na sio wakuokota kama toyota
 
Feb 10, 2017
98
316
tanzania asilimia kubwa ya mafundi wa nisani hawapo sawa na mafundi simu wa kariakoo na mikoani.

nisani inamfumo mwingi wa umeme na teknolojia ambayo ni ngeni kwa mafundi na hawa taki kusema ukweli ndio maana mafundi wanasingizia ni kimeo.

jiulize kwa nini range inamafundi wa kuhesabu na sio wakuokota kama toyota
Uko sahihi nakubaliana na wewe 100%
 
9 Reactions
Reply
Top Bottom