Nissan Dualis: Msaada mwenye uzoefu na hili gari naomba ufafanuzi

Wamiliki wengi wa magari hawako realistic, wanaigiza maisha na wanasema ukweli nusu nusu.

Ukitaka ujue ukweli wa ubora wa magari pita karakana za kutengeneza magari mitaani, tazama, uliza na kudadisi kuhusu magari mbali mbali kisha utapata majibu.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb

Ni kweli ila kwa mfano garage zote za hapa Arusha Matoyota ndiyo yamejaa huko....
Ina maana haya matoyota ni mabovu kuli brands nyinginezo..?
 
Ni kweli ila kwa mfano garage zote za hapa Arusha Matoyota ndiyo yamejaa huko....
Ina maana haya matoyota ni mabovu kuli brands nyinginezo..?
Ndio maana yake. Na ukienda kwenye hizo garage hukuti Nissan imelala au benz, utakuta tu za Toyota hadi zimeotea majani kwa chini
 
Wakuu nianze kwa kuwasalimu na kuendelea kukumbushana pia kuhusu namna ya kujikinga na hili gonjwa la sasa.. Corona

Naomba nije kwenye topic kuu sasa.

Nimekuwa nikitamani sana kumiliki gari lililo juu juu (wenyewe wanaita SUV), kutokana na mazingira niliyopo, gari la chini linaumia sana.

Nimejipanga nimepata 15Mil, kuna mdau akanishauri kwa bajeti yangu gari la juu juu ninaloweza kupata ni ilo gari tajwa Nissan dualis

Sasa nimekuja kwenu wataalam kuomba ushauri pia kabla sijafanya maamuzi ya kununua ilo gari

  • ni kweli naweza kupata nissan dualis kwa bajeti ya 15Mil?
  • vipi kuhusu vipuli vyake?
  • Uimara wake upoje?
  • shida na matatizo ya hili gari ni yapi?
  • 15km kwa lita moja, fuel consumption ni kweli?
  • kuna SUV yoyote ninayoweza kupata kwa bajeti ya 15Mil?
  • kuna model ngapi za hili gari?

Nakadharika nakadharika, naamini kupitia JF, nitapata mawazo na ushauri mzuri kabla ya kufanya maamuzi

Nilichokifanya mpaka sasa nimegoogle tu nikaliona muonekano wake na likanivutia pia kimuonekano

Natanguliza shukrani zangu kwenu wakuu
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa million 15 labda utafute ya mtu mkononi ila kwa kuagiza, TRA wana ufala wao wamefanya sasa hivi itakubidi uongeze kama million 3 hapo kwenye bajeti ndipo utaweza kuitoa bandali. Ila hadi kiasi hicho ulichonacho unaweza agiza wakati ipo njiani uwe unajikusanya hela ya bandari, tra, na clearance.

Ni gari nzur mimi pia najikusanya niuze kibaby walker hiki nichukue hiyo nivimbe nayo mjini. Hizo prado tutanunua baadae maana watu wenye roho mbaya wameshika uchumi kwa sasa.
 
Sio mtaalamu wa magari niseme nitayajibu maswali yako mkuu. Nichokoze mada.

Kwa muonekano ni kagari kazuri na portable saana. Niseme napenda muonekano wake.

Parts...nina wasiwasi maana bongo sijayaona mengi.

Ulaji wa mafuta....kuna ndugu yake wametoka kabila moja hilo hilo la Nissan anaitwa Primera...tank halijai na ni kama umemwagia maji kwenye mchanga. Hili lilinifanya niogope jina Nissan.

Kwa muonekano nje na ndani nalipa 98%. Sema naona wapenda Nissan wanakimbilia saana Qashkai (sijui nimepatia jina) kuliko Dualis
Labda haujatazama vema barabarani but hizi gari zipo nyingi kwa sasa na kuhusu spare zinapatikana vema tu na hata ukikosa hapa tz kuagiza ni rahisi sana kwasasa. Pia wanadealer wa nissan hapa tz nadhani.

Hii aliyopost hapo sio body ya Nissan Dualis, bali ni body ya Nissan Qashqai iliyobandikwa jina la dualis kwenye plate.

Nitakiwekea picha ujue tofauti ya bodi ila zote ni gari moja ni sawa sawa n kusema Iphone 7 na Iphone 7 plus......
 
Nitajibu kama ifuatavyo:

Uimara
Magari yote yaliyotengenezwa miaka ya 2004 na kuendelea yanafanana kwa silimia kubwa uimara wake bila kujalisha make...yaani ni magari ambayo uimara wake unategemea na unavyolitunza......Usitegemee dunia ya leo kupata SUV ngumu kama Jeep zilizotumika kwenye Vita bya Vietnam..

Upatikanaji wa vipuri
Vipuri vya sehemu nyeti kama engine, miguu vinapatikana kwa sababu kwa asilimia kubwa vinavaliana na x trail ambazo ni nyingi sana....Ila bei ipo juu kidogo..body parts ndiyo changamoto mfano taa,vitasa n.k.

Ulaji wa mafuta
haijaachana na wakina xtrail, rav 4 na SUV nyinginezo za saizi hizo..

Model zake
Hii ndiyo generation ya kwanza kwa bongo bado hatujapata generation ya pili...Ualaya na America inauza kama Nissan Quashqui..

Ground clearance
Ipo poa sana hivyo inamudu barabara mbovu...

Ubaya wake
Ukitaka kuliuza mteja hapatika haraka, na bei ya kuuzia si nzuri kwa sababu Tanzania Toyota ndiyo zinapendwa zaidi ikiaminika kuwa hata masikini anaweza kumiliki toyota.

General conclusion
Nissan dualis ni gari nzuri kama wewe ni mpezi wa Nissan...au kama umechoshwa na Rav 4, Clugger, basi Dualis ni mbadala mzuri..
Karibu NISSAN..

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya asante mwanachi kutoka kijiji cha Nissanians.....
 
Nissan Dualis
images%20(28).jpg
 
Ukifuatilia Japanese cars, utagundua Nissan waliwahi kutumia technology mpya ya CVT kabla ya Toyota....sasa cvt za nissan zilipoingia mtaani,mafundi wa mwembeni wakaziponda na kuwaanisha watu ni mbovu, kumbe wao ndiyo wabovu...walizoea kuchokonoa Ordinary Automatic Transmission za Kwenye Corolla na Carina..

Nadhani wanaogopa CVT kwa sababu mbili kubwa...
1. Wabongo tunapenda vitu vya bei rahisi...mtu anataka kumwaga oil ya gear box asitumie zaidi ya 80k...
Kwa upande wa CVT lazima ujipange, oil peke yake maeneo mengi ya TZ haipungui 130k kwa gharama za chini, hapo bado hujamlipa fundi..

2. Elimu...Nimegundua wamiliki wengi wa magari hawana elimu ya kutosha juu ya magari wanayoyamiliki...mtu haelewi gari lake lina gear box ya mfumo gani, yeye anachojua ni kushift kutoka P na kwenda R au D...Mafundi nao hawana elimu ya kutosha....
Umeshawahi kujiuliza kwa nini watu wengi siku hizi wanaomiliki Toyota latest hawakawii kuua gear box...?

Unakuta Toyota imekuja na VCT gear box, siku ya service wanaweka cheap ATF kutoka PUMA Patrol station....Walishakariri Carina zinatumia ATF za pale Puma, basi wanaweka hizo hizo kwenye Passo, IST na nyinginezo....hawana taarifa kuwa hata hizi passo na ist zipo za CVT..

Conclusion
CVT ni transmission nzuri sana ukiweza kuitunza na kuipa fluid yake iliyopendekezwa kwa sababu inakupa smooth driving bila kusikia mshtuko wa kubadilika kwa gear.

Hivyo nimawaasa watu wawe waangalifu, CVT kwenye Nissan zimeshakuwa common, kwa sasa zinakuja kwa kasi kwenye baadhi ya Toyota, Mitsubish na Suzuki. Wale wamiliki wa Toyota wanaopenda cheap services kutoka Puma petrol station, mtaua gear box zenu kila siku.

Soma kwenye kweny deep stick ya oil ya gearbox uone umeambiwa uweke fluid ya aina gani, ufanye hivyo na si vinginevyo.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Safi. Umeelezea vema sana na ungekuwa karibu nikununulia japo Pepsi big.....

Safi sana wewe unayajua magari ya sasa na unafuatilia. Safi sana kijana
 
Nissan ni kama simu za samsung, hizo ni gari za kiduwanzi sana ukinunua leo baada ya mwezi utakuja kuuza robo bei. Hiyo dualis mwaka jana ilikua ni milioni 23 -28 milioni, Nissan Qashqai iilikua 34-38 soko la leo ukiagiza japan mpaka kuiingiza barabarani dualis ni 12-14 milioni Qashqai ni 18M-20M. Extrail mpaka milioni 8 unapata kudaadeki gari gan hizo? Bado service yake ni gharama sana.
Sio kweli hiyo milioni 12 - 14 sio kweli hebu kacheki na source ya details zako upya.....
 
Unanunua gari ili uuze au utumie? Kuna wanaokaa na magari miaka hata 8.

Kichwa chako kiko sawa?
Nane kidogo sana. Nina mjomba wangu alinunua Suzuki escudo, tokea 2000 yupo nayo hadi sasa hesabu ni miaka mingapi sasa!
 
Ni gari nzuri ina power na speed ila mafuta inameza haswa.
Sio kweli.... Wewe unajua gari inayomeza mafuta.....?!

Mimi natumia passo ya piston tatu ila mafuta unywaji wake haiifikii hiyo Nissan dualis.

Niulize kwann mtoto wa dada nikuelezee....
 
Sasa mimi ni mpenzi mkubwa wa Nissan, tema Murano. Ninaimiliki ila imenitesa sana sio kidogo ila imekuja kutulia hadi nashangaa.
Ipo hv, nilipoinunua hii gari sikupata shida. Siku moja nikampa fundi anifanyie service ya oil ya gear box na Engine. Fundi akanunua oil ya Puma(manjis Arusha) badala ya Matic J(Murano inatumia matic). Akaweka hiyo oil na mimi sikujua. Baada ya kama mwezi mmoja tu gia ya rivers ikaanza kuwa haikubali gari ikipata moto. Yani ilianza kelele hapo. Mimi sikujua shida ni nini. Gari ilinisumbua sana kama miezi 4-6 nateseka tu. Mara ikaanza kuwa inazima tu yenyewe, mara inaua coil, mara betri inakufa kwa muda mfupi. Nimetembeza karibu garage zote Arusha, niliwasiliana na mafundi wa dar nao vilaza tu. Diagnosis machine nazo zinataja codes ambazo hata uki Google inaeleza vingine. Nikibadilisha control box, coil zote, pulgs zote bila muafaka. Hadi pump ya mafuta niliweka mpya ila gari hamna kitu. Nilitokea kuichukia sana. Nilibadili hadi camshaft sensor, crankshaft sensor, oxygen sensor ila bado hamna kitu.
Katika kutafuta msaada nikakutana na fundi mmoja akaniambia hii gari imeua sensor kwenye gia box na imewekwa oil ambayo sio yake. Akaniambia tatizo hapo ni gear box tu hmhamna kingine, nilishindwa kumuamini ila mwisho wa siku ilibidi nimuamini. Akaniambia nimpe hizo sensor zote coil na vifaa vya zamani avirudishie vyote halafu tuagize gear box nyingine(alinishauri kuwa gear box haifai kutengeneza) wakuu nialiagiza gear box, akafunga, akarudisha vile vifaa vyake vya zamani vyote. Hadi lei gari imetulia na sikuamini kama ni ile Murano iliyokuwa inawasha taa zote ukianzia na check engine.
Conclusion ni kuwa magari ya Nissan sio mabaya bali mafundi wetu elimu chenga. Na bei za vifaa mafundi ndio wanapandisha.
Nissan murano ni gari comfortable sana na ni nzuri ukiitunza na kuipa vitu vyake original
Sahihi kabisa.... Umeongea ukweli kabisa.
 
Ila jamaa wewe kweli ni Car enthusiast wa ukweli. Umepambana hadi umesolve tatizo. Wewe hakuna gari itakuja kukupasua kichwa tena kama umeweza kuvumilia hiyo kash kash ya murano.

Safi sana. Big up kwako
 
Sasa hizo gharama zote si ungeagiza mpya tu?
Mahaba mama... Sisi wanaume magari huwa yanatuteka akili sana na hatukubali kirahisi yatushinde.

Nikikuhadithia kisa cha rafiki yangu aliekuwa anahangaika kutengeneza Subaru yake utasema nyie wanaume mnavichaa na magari yenu.
 
Back
Top Bottom