Nissan Dualis: Msaada mwenye uzoefu na hili gari naomba ufafanuzi

Nitajibu kama ifuatavyo...

Uimara.....Magari yote yaliyotengenezwa miaka ya 2004 na kuendelea yanafanana kwa silimia kubwa uimara wake bila kujalisha make...yaani ni magari ambayo uimara wake unategemea na unavyolitunza......Usitegemee dunia ya leo kupata SUV ngumu kama Jeep zilizotumika kwenye Vita bya Vietnam...
Hapo kwenye ubaya umenigusa nina Nissan Murano ya 2005. Bado iko bomba lakini wateja wanaliogopa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
chukua hilo gari mkuu kwa ufafanuzi wa wadau hapo juu liko poa, mwenyewe nampango wa kulinunua
 
Mimi namiliki Nissan Dualis 2008. What I can say ni it’s the best purchase I have ever made. Gari liko smooth on the road, posh inside yaani na ukipata ile ya rooftop kuwa na glass yaani ni kama unaendesha evogue. Pia iko juu sana. Nina kama mwaka sasa niko na hili gari, changamoto zake ni spare ni VERY EXPENSIVE.

Japo kuaribika ni nadra sana unless wewe ni mtu wa safari za mbali kama mimi ila kitu kikianza kulia either engine au miguuni aisee andaa hela sio za kitoto. Maana unakuta kifaa hiko hiko kwa Rav 4 kwako ni mara 3 mpaka nne ya bei.

But overall ni gari zuri sanaaa, ila kama waswahili wanavyosema, kizuri kina garama
 
Ukifuatilia Japanese cars, utagundua Nissan waliwahi kutumia technology mpya ya CVT kabla ya Toyota....sasa cvt za nissan zilipoingia mtaani,mafundi wa mwembeni wakaziponda na kuwaanisha watu ni mbovu, kumbe wao ndiyo wabovu...walizoea kuchokonoa Ordinary Automatic Transmission za Kwenye Corolla na Carina....

Nadhani wanaogopa CVT kwa sababu mbili kubwa.
1. Wabongo tunapenda vitu vya bei rahisi...mtu anataka kumwaga oil ya gear box asitumie zaidi ya 80k...
Nakuunga mkono kwa asilimia 100% but sio muuzaji wa puma but niseme tu pale kuna aina zote za ATF tatizo liko kwa wamiliki wa magari wenyewe maana wamekalili T-ii oil pekee kwamba ndo inaingia kwenye gari zao bila kuangalia chini ya dipstick wameandika nn
Mfano ni mteja wangu mmoja alikuja na premio yake akataka ATF ya bei rahisi nikamuuliza kwann ya bei rahisi na gari yako huwa inatumia hivyo?

Akasema uchumi mbovu na naitaka hiyo inisaidie kusukuma miez miwil hadi nipate pesa ya kuweka oil nzuri, lakin kwa kadri tulivyopigwa elimu la uuzaji wa vilainishi unashauriwa kuijali Mali ya mteja wako kama yako ili aishi nayo miaka mingi na azidi kuwa mteja wako lakn ukimpa kitu kibaya ataua gari yake na hatakua mteja wako tena, basi nikamwambia leta chasisi no tuangalie aina gani ya oil inayotakiwa kuwekwa na tukakuta inatumia WS ATF.

Point yangu hapa ni nn tupende kuweka vitu ambavyo viko recommended na watengenezaji wa gari zetu na pia fundi wa kwanza wa gari yako ni wewe mwenyewe mmiliki kwanza kabla hujapeleka garage na tambua mafundi wengi wa mtaani akishatoka pale Must mbeya au NIT hafikirii kusoma tena na kila siku kunavyokucha technologia inakua ndo hivyo hivyo waendesha magari wana upgrade kulingana na wakati
 
Mimi namiliki Nissan Dualis 2008. What I can say ni it’s the best purchase I have ever made. Gari liko smooth on the road, posh inside yaani na ukipata ile ya rooftop kuwa na glass yaani ni kama unaendesha evogue. Pia iko juu sana. Nina kama mwaka sasa niko na hili gari, changamoto zake ni spare ni VERY EXPENSIVE..
Tugusie kidogo hapa mkuu kwenye spare kwa mifano
 
Back
Top Bottom