Nissan Dualis: Msaada mwenye uzoefu na hili gari naomba ufafanuzi

Ni kweli ila kwa mfano garage zote za hapa Arusha Matoyota ndiyo yamejaa huko....
Ina maana haya matoyota ni mabovu kuli brands nyinginezo..?
Haijarishi ni brand gani, ubovu upo tu kwenye magari ya brand zote.
Sasa ni ubovu upi na unagharimu kiasi gani? Kama wewe sio mzoefu wa magari, na unataka kudadisi kujua ubora wa gari unayotaka kununua, basi kuwa mdadisi kwa kupita kwa mafundi wa magari na garage kadhaa, utapata ukweli mkubwa zaidi kuliko kumuuliza mmiliki wa gari husika akwambie ukweli mchungu.

Tukubali tu, watanzania hatuko honest kuusema ukweli mchungu unaotugusa moja kwa moja.
 
Kwa uzoefu wangu mdogo wa magari, magari mengi ya brand ya Nissan yanamuonekano mzuri, Comfortable nzuri ukiwa ndani na gharama nafuu ukitaka kuyamiliki ukilinganisha na brand zingine, lakini yana gharama kubwa zaidi katika services&maintanance.
 
Nissan iko overrated.
Nakumbuka wakati Nissan Xtrail zinaanza kuingia Tz ilionekana kama zingekuwa mshindani au mbadala wa Toyota Prado, kilichotokea sote tunakijua, leo hii sokoni Xtrail inashindana na Toyota IST !

Vivo hivyo kwa Nissan Morano, zilionekana labda zingeweza kuiondoa Toyota Prado sokoni, lakini wapi, hata kuiondoa Toyota Kluger au Harrier imekuwa haiwezekani.

Ukija kwa Nissan Dualis vivyo hivyo utadhani ingeitoa new model ya Rav4 au Escudo sokoni, lakini wapi, hakuna kitu. Mambo ni yale yale.
 
Nissan ni kama simu za samsung, hizo ni gari za kiduwanzi sana ukinunua leo baada ya mwezi utakuja kuuza robo bei. Hiyo dualis mwaka jana ilikua ni milioni 23 -28 milioni, Nissan Qashqai iilikua 34-38 soko la leo ukiagiza japan mpaka kuiingiza barabarani dualis ni 12-14 milioni Qashqai ni 18M-20M. Extrail mpaka milioni 8 unapata kudaadeki gari gan hizo? Bado service yake ni gharama sana.

Kwa kifupi gari Nissan ni sawa na Utopolo Yanga , spare part zake kuzinunua ni bei mbaya kama bei ya akina Sarpong wakati mafundi wa kufunga mtaani hawapo na ukiwapata wanazidi kuharibu kwa sababu hawajui nini wanachokifanya, binafsi nilitaka kutupa gearbox ya gari yangu kwa ushauri wa kishenzi kwa sababu mafundi wengi walikuwa hawajui nini cha kufanya kumbe tatizo nilikuwa natumia a different ATF, kuanzia hapo niliamua kuwa member wa wengi kwa kuzingatia, Total price must be cheap, Spare part availability, Technician availability, uhitaji wa barabara zetu na uchumi wetu wengi uwe na uwezo wa kuinunua pale nitakapoamua kuiuza,

Kwa mfano leo hii ukitaka kumuuza Sarpong nani atapiga hodi nyumbani kwako? kila la kheri na tukutane kesho
 
Nissan iko overrated.
Nakumbuka wakati Nissan Xtrail zinaanza kuingia Tz ilionekana kama zingekuwa mshindani au mbadala wa Toyota Prado, kilichotokea sote tunakijua, leo hii sokoni Xtrail inashindana na Toyota IST !

Vivo hivyo kwa Nissan Morano, zilionekana labda zingeweza kuiondoa Toyota Prado sokoni, lakini wapi, hata kuiondoa Toyota Kluger au Harrier imekuwa haiwezekani.

Ukija kwa Nissan Dualis vivyo hivyo utadhani ingeitoa new model ya Rav4 au Escudo sokoni, lakini wapi, hakuna kitu. Mambo ni yale yale.

Kwa kifupi tu hakuna gari (kwa ujumla wake) inaweza shindana na TOYOTA kwenye suala la reliability. TOYOTA hawatengenezi magari sophisticated, luxury au yenye usalama zaidi kuliko wengine ila wanatengeneza magari yenye mifumo inayoweza kudumu na kuaminika kuliko wengine (in most cases/kwenye segment karibia zote. Kwa mfano Rav 4 matoleo karibia yote yana mauzo mazuri Ulaya na marekani kwa sababu nilizotaja hapo.
Hili halimaanishi kuwa magari mengine ni ya hovyo sana (ingawa yapo ya hivyo) ila inategemea na mnunuzi anataka nini kwenye gari
 
Sasa mimi ni mpenzi mkubwa wa Nissan, tema Murano. Ninaimiliki ila imenitesa sana sio kidogo ila imekuja kutulia hadi nashangaa.
Ipo hv, nilipoinunua hii gari sikupata shida. Siku moja nikampa fundi anifanyie service ya oil ya gear box na Engine. Fundi akanunua oil ya Puma(manjis Arusha) badala ya Matic J(Murano inatumia matic). Akaweka hiyo oil na mimi sikujua. Baada ya kama mwezi mmoja tu gia ya rivers ikaanza kuwa haikubali gari ikipata moto. Yani ilianza kelele hapo. Mimi sikujua shida ni nini. Gari ilinisumbua sana kama miezi 4-6 nateseka tu. Mara ikaanza kuwa inazima tu yenyewe, mara inaua coil, mara betri inakufa kwa muda mfupi. Nimetembeza karibu garage zote Arusha, niliwasiliana na mafundi wa dar nao vilaza tu. Diagnosis machine nazo zinataja codes ambazo hata uki Google inaeleza vingine. Nikibadilisha control box, coil zote, pulgs zote bila muafaka. Hadi pump ya mafuta niliweka mpya ila gari hamna kitu. Nilitokea kuichukia sana. Nilibadili hadi camshaft sensor, crankshaft sensor, oxygen sensor ila bado hamna kitu.
Katika kutafuta msaada nikakutana na fundi mmoja akaniambia hii gari imeua sensor kwenye gia box na imewekwa oil ambayo sio yake. Akaniambia tatizo hapo ni gear box tu hmhamna kingine, nilishindwa kumuamini ila mwisho wa siku ilibidi nimuamini. Akaniambia nimpe hizo sensor zote coil na vifaa vya zamani avirudishie vyote halafu tuagize gear box nyingine(alinishauri kuwa gear box haifai kutengeneza) wakuu nialiagiza gear box, akafunga, akarudisha vile vifaa vyake vya zamani vyote. Hadi lei gari imetulia na sikuamini kama ni ile Murano iliyokuwa inawasha taa zote ukianzia na check engine.
Conclusion ni kuwa magari ya Nissan sio mabaya bali mafundi wetu elimu chenga. Na bei za vifaa mafundi ndio wanapandisha.
Nissan murano ni gari comfortable sana na ni nzuri ukiitunza na kuipa vitu vyake original
Nimepata jibu ya Tatizo la Murano yangu nimepaki mwaka wa 2 sasa
 
Kwa kifupi tu hakuna gari (kwa ujumla wake) inaweza shindana na TOYOTA kwenye suala la reliability. TOYOTA hawatengenezi magari sophisticated, luxury au yenye usalama zaidi kuliko wengine ila wanatengeneza magari yenye mifumo inayoweza kudumu na kuaminika kuliko wengine (in most cases/kwenye segment karibia zote. Kwa mfano Rav 4 matoleo karibia yote yana mauzo mazuri Ulaya na marekani kwa sababu nilizotaja hapo.
Hili halimaanishi kuwa magari mengine ni ya hovyo sana (ingawa yapo ya hivyo) ila inategemea na mnunuzi anataka nini kwenye gari
Hii comment ina akili sana. Moja ya comment bora nilizowahi kusoma jukwaa zima la magari.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Too much theory. Kama naona soli ya kiatu ilivyolika upande mmoja.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Hata mimi hizo theory zao zinanichekeshaga sana.
Eti wanakwambia usijenge nyumba ya kuishi ni liability wakati huo yeye anatakiwa kila mwezi alipe kodi sasa hawaoni kuwa hiyo kodi wanayolipa kila mwezi pia ni liability.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Maisha yenyewe ni liability.

Unatumia gharama nyingi kuishi sijui kula, kodi, mavazi, makazi, malazi etc lakini mwisho wa siku unakufa!

Sometimes naonaga ni lack of common sense tu.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Maisha yenyewe ni liability.

Unatumia gharama nyingi kuishi sijui kula, kodi, mavazi, makazi, malazi etc lakini mwisho wa siku unakufa!

Sometimes naonaga ni lack of common sense tu.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Kukariri notsi za darasani bila kutumia actual life common sense ni stupidity haijalishi umesoma degrees ngapi

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Vipi haka kagari toyota auris naomba kuliizia price, mantainance na fuel consumption yake ipo vipi. Je kati ya hii AURIS na IST ipi ipo vizuri? Hii auris nitokea kuilewa zaidi. Kwenu wataala
 
Back
Top Bottom