Mkata-tamaa
Senior Member
- Nov 21, 2018
- 180
- 312
Picha: Nissan Dualis
Wakuu nianze kwa kuwasalimu na kuendelea kukumbushana pia kuhusu namna ya kujikinga na hili gonjwa la sasa.. Corona
Naomba nije kwenye topic kuu sasa.
Nimekuwa nikitamani sana kumiliki gari lililo juu juu (wenyewe wanaita SUV), kutokana na mazingira niliyopo, gari la chini linaumia sana.
Nimejipanga nimepata 15Mil, kuna mdau akanishauri kwa bajeti yangu gari la juu juu ninaloweza kupata ni ilo gari tajwa Nissan dualis
Sasa nimekuja kwenu wataalam kuomba ushauri pia kabla sijafanya maamuzi ya kununua ilo gari
- Ni kweli naweza kupata nissan dualis kwa bajeti ya 15Mil?
- Vipi kuhusu vipuri vyake?
- Uimara wake upoje?
- Shida na matatizo ya hili gari ni yapi?
- 15km kwa lita moja, fuel consumption ni kweli?
- Kuna SUV yoyote ninayoweza kupata kwa bajeti ya 15Mil?
- Kuna model ngapi za hili gari?
Nakadhalika nakadhalika, naamini kupitia JF, nitapata mawazo na ushauri mzuri kabla ya kufanya maamuzi
Nilichokifanya mpaka sasa nimegoogle tu nikaliona muonekano wake na likanivutia pia kimuonekano
Natanguliza shukrani zangu kwenu wakuu
Sent using Jamii Forums mobile app