Ngisibara
JF-Expert Member
- Jan 2, 2009
- 3,301
- 2,076
Wana JF naomba kuelimishwa kidogo kuhusu bei ya magari katika mtandao wa Tradecar view kabla sijamnunulia dada/shemeji yenu, katika pitapita yangu ndani ya mtandao kuna kitu kimenishangaza sana kwani nimegundua gari nyingi za Nissan Ad Van ni bei chini sana tena kama ya mwaka 2005 ina uzwa kwa US$ 447 (FOB price) na baada ya kuunganisha mahesabu yote ya Inspection fee, Insuarance na fleight charges nikapata CIF US$ 1847, nikatumia GariYangu.com kukokotoa mahesabu ya TRA ili kujua gharama halisi mpaka kulitoa nikawa nimepata US$ 3.222 ambayo ni sawa na Tsh 4,188,285.00, kiujumla bei hiyo ni chini ya bei ya pikipiki inayouzwa ndani ya mtandao huo kwa US$112, sasa nabaki kujiuliza kulikoni? kunanini ndani yake kwani ukiiangalia inavutia na engine inaonekana sio complicated kama BMW, Ningependa kumchukulia BMW lakini naogopa kwani nasikia Dar hawana mafundi na hata wangekuwapo hawana computerised diagnostic equipment kwa gari kama hizo, tafadhali wakuu mnipe mwanga kwa hilo