Nisome nini ili niwe miongoni mwa "white hackers" hatari duniani kwenye suala la computer na mitandao kiujumla?

Habarini wakuu. Mimi ni kijana "age below 35".Napenda sana siku zijazo nije kuwa miongoni mwa watu wenye uwezo mkubwa wa kuamrisha internet kufanya kile ninachotaka. Hizi 'Search engines' zote kuanzia google hadi yahoo nizikosoe kwa namna moja ama nyingine.Hizi facebook,whatsap,instagram,tweeter etc nizivuruge kwa kuongeza vitu unique au nizikosoe kwa namna moja ama nyingine.Nisome course ipi ili nifanye hayo yote?.

NB:Mimi ni msomi wa kawaida tu(First degree holder).Bachelor of science with education "Chemistry+Biology".

Natanguliza shukrani.
SOMA + TUTORIAL + PRACTICE + COMMITMENT
 
Google Kuna materials kibao kuhusu hacking. Ukiweza inalipa Sana ukifanya kazi as systems security analyst. Bidii yako tu Mkuu ya kusoma na kupractise.
Nashukuru mkuu. Ahsante sana kwa ushauri wako.
 
Kwa namna ulivyoandika hupaswi kuungwa mkono maana unataka kuvuruga mipango ya watu

Kuna dalili nimeiona wazi kua testing yako ya kwanza utaielekezea jf, jambo ambalo hatuko tayari kuliruhusu litokee
Siwezi kuisaliti Jamiiforums.Bali nitakuwa najitahidi kuiboresha kwa kuondoa loopholes zilizopo.Nipe hizo mbinu mkuu.
 
Kuwa hacker mzuri hauitaji usome hata... ni kitu ambacho kinakuwa ndani ya damu.. hacker wengi wa kusomea ni watupu sanaaaaa
Lazima usome hilo halikwepeki,yaani sawa uwe na talent ya mpira alafu husifanye mazoezi,tunadanganyana kusoma hakukwepeki.Tena hizi field za IT kila siku zinabadilika,lazima usome kila siku uendane na mabadiliko .
 
Yatakusaidia nini hayo mambo?
Kwanza ni burudani kujua hizi ishu.Pili ni chanzo cha kutatua matatizo mbalimbali katika jamii.Na mwisho ni kwamba nitapata pesa nyingi.
 
Kwanza ni burudani kujua hizi ishu.Pili ni chanzo cha kutatua matatizo mbalimbali katika jamii.Na mwisho ni kwamba nitapata pesa nyingi.
Safari ndefu wenzetu wazungu wanaanzaga mapema,inabidi uwe na basic za Networking,Database,Linux,Website na programming.

Shughuli pevu lazima upractice SANA TENA SANA.

Ila na kwambia kuna kupenda na kuweza,unaweza ukapenda udaktari lkn biology inakukataa,so fanya unachoweza.
 
Kafanye kuzi chunguza kwanza system au mfomu unaotaka ku hack, uelewe namna unavyo fanya kazi in and out.. hapo unakuwa umemaliza kazi.. huwezi kupotea njia unayo pita kila siku, sana sana utagundua chocho za kukufikisha mapema ( hacking )
Point noted. Kwahiyo kozi ipi unashauri nianze nayo kwa haya malengo yangu?
 
Nenda Turkey huko, kuna madogo watakusaidia kukufundisha..

kuna hacker walitaka kusepa na account ya Twitter ya Trump

kuna m Turkey alisepa na account ya Twitter ya samatta
Duuh, huko ni ngumu kwenda. Hata jinsi ya kuwasiliana na hao madogo wa turkey bado itakuwa ngumu. Nahitaji mbinu zitakazonisaidia kulingana na mazingira niliyopo (Tanzania)
 
Habarini wakuu. Mimi ni kijana "age below 35".Napenda sana siku zijazo nije kuwa miongoni mwa watu wenye uwezo mkubwa wa kuamrisha internet kufanya kile ninachotaka. Hizi 'Search engines' zote kuanzia google hadi yahoo nizikosoe kwa namna moja ama nyingine.Hizi facebook,whatsap,instagram,tweeter etc nizivuruge kwa kuongeza vitu unique au nizikosoe kwa namna moja ama nyingine.Nisome course ipi ili nifanye hayo yote?.

NB:Mimi ni msomi wa kawaida tu(First degree holder).Bachelor of science with education "Chemistry+Biology".

Natanguliza shukrani.
Mkuu unajua magimbi yanatumia muda gani kuanzia kulima hadi kuvuna?
 
Safari ndefu wenzetu wazungu wanaanzaga mapema,inabidi uwe na basic za Networking,Database,Linux,Website na programming.

Shughuli pevu lazima upractice SANA TENA SANA.

Ila na kwambia kuna kupenda na kuweza,unaweza ukapenda udaktari lkn biology inakukataa,so fanya unachoweza.
Naamini nitaweza.Nia ninayo,uwezo wa kupiga msuli ninao na sababu ya kufanya hivyo ninayo pia."Mungu nisaidie"
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom