Nisome Degree nyingine?

Kikomelo

Senior Member
Sep 12, 2011
106
57
Mimi ni kijana mwenye miaka 29, nina Advanced Diploma in Accountancy toka IFM yenye GPA ya 4.2, nina CPA na MBA. Ninapenda sana kufundisha vyuo lakini nimekuwa nikikutana na ugumu kutokana na kuwa na Advanced Diploma. Nimekuwa nikifikiri kwa muda sasa kuwa nisome Open univestity degree ya Accounting ili nipate 1st class na kuingia kwenye game la kufundisha vyuo vikuu! je wadau mnanishaurije?
 
Muombe Mungu kwanza akupe ushauri mzuri. Kama umemuomba basi yawezekana ni kupitia hii thread waweza kupata ushauri mzuri ingawa Shetani anaweza kujipenyeza pia. Nakushauri kuwa;

1. Sio lazima ufundishe, yawezekana Mungu hajakupangia hilo na wewe umezuia blessings nyingi kutoka kwake kwa kung'ang'ania kufundisha.
2. Subiri nafasi zikitoka za kufundisha hapo IFM utakubaliwa
3. Kama huna kazi, nenda kaipeleke CV yako Deloitte, KPMG, PWC au E&Y lazima watakuita na kama huna uzoefu mkubwa wa kazi kubwa, accept kuanza ktk level ya chini then after time utakuwa na experience itakayokupa 'kiburi' cha kubargain kwenye blue-chip companies. Waweza pia kuipeleka kwenye mabenki watakuchukua. Belittle yourself ili baada ya muda ulie kivulini.
 
Ya ni kweli kwa elimu yako si lazima ufundishe vyuo lafu by the way umeona nini kwenye kufundisha vyuo maana kama masilahi si kama unavyodhani utakubali kuishi kwa mshahara tu katika maisha yako?Tupo humu but tunaona kuwa we need to struggle a lot
 
Kwani lazima ufundishe?.CPA yako ni mwaka gani? maana hizo ni professional za kukuwezesha hata wewe kuajiri na kujiajiri pia wewe mwenyewe .Muhimu ni kufanya networking na watu wengine.Elimu yako nzuri siyo ya kutembea na kusaga sole na bahasha yakaki.Pay ya tutor ni chini gross siamini kama inazidi 2m and is not a deal at all. find networks man
 
Kwani lazima ufundishe?.CPA yako ni mwaka gani? maana hizo ni professional za kukuwezesha hata wewe kuajiri na kujiajiri pia wewe mwenyewe .Muhimu ni kufanya networking na watu wengine.Elimu yako nzuri siyo ya kutembea na kusaga sole na bahasha yakaki.Pay ya tutor ni chini gross siamini kama inazidi 2m and is not a deal at all. find networks man

Asante sana ndugu kwa ushauri, CPA yangu ni ya mwaka 2010 December. Najaribu kufanya networking lakini bado kuna ka ugumu ndugu yangu!
 
pole yaan hata ww unahangaika na cpa mkononi hii serikali inatufanya mbaya wangetoa hata mikopo ya kuanzia biashara tunapokuwa kitaa.
 
kwa elimu yako ndugu nakushauri ;usiwe kimya wakati unakitu mkononi cha kukusaidia ,ebu jichanganye vizuru ndgu yangu.
 
unajua kuna mambo ukisikia/ukiona unashangaa, mi kuna jamaa nime graduate nae mwaka 2007 Bsc yy alipata GPA 2.6(gentleman), 2008 akaanza degree nyingine ya economics open Univ akamaliza 2010 na GPA 4.2, akaomba kazi ya TA open akapata wakamtupa huko mikoa ya kati mpaka sasa hiv anachapa kazi sie bado tunamaliza sole ofice kwa ofice kusaka vibarua.
ww anagalia nn moyo wako unataka fanya, hope utafanikiwa,
wish u all the best
 
Fuata moyo wako unataka nini. Kama ni kweli unataka ualimu unaweza ukatumia adv diploma yako kuomba postgraduate diploma. Ukimaliza unafanya masters. Utakuwa na uwezo wa kuwa assistant lecturer.

Ikiwa ile MBA ulikuwa unamaanisha Masters in Business Administration basi unaweza kuitumia kuomba kufundisha vyuo vikuu.

Nakuhakikishia ukiwa na masters na hiyo CPA mambo yako hayatakuwa mabaya.
 
Hii nchi yangu jamani....kuna watu wengi wana kisomo nao bado wanaangaika kupata kazi za kuwatoa kimaisha. vilevile kuna fani nyingine huwezi kujiajiri lakini ya kwako waweza labda kigumu is how to start business. tuombe Mungu atuondolee giza hili la ukosefu wa ajira
 
Nakusaidia pia peleka CV yako pale NBAA muone mtu mmoja anaitwa Juma Mtema mara nyingi ananetwork na waajiri wasiotaka longolongo za magazeti.NBAA inaratibu na kuwapa jina na pengine wao wanashiriki kwenye interview basi.Check with him immediately through 0715928074.
 
Nakusaidia pia peleka CV yako pale NBAA muone mtu mmoja anaitwa Juma Mtema mara nyingi ananetwork na waajiri wasiotaka longolongo za magazeti.NBAA inaratibu na kuwapa jina na pengine wao wanashiriki kwenye interview basi.Check with him immediately through 0715928074.

dah mdau hii meseji yako kusema kweli imenigusa sana kaka ...mbarikiwe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom