JF wote wanajua kila kitu ni sawa. JF wote ni washauri wa kuanzia siasa, uchumi, michezo nk, jf wengi wanajiweza, its ok, JF wote ni mapro kwa kila sector, thats good.
=======
Kwa kawaida, mtu anayependa kusaidia huanzia kwa watu wake wa karibu kwanza kabla ya kuja JF kutoa ushauri wa namna mambo yanavyopaswa kufanyika. Kama kweli mnayosema ni sahihi, leo natamani kuona mtu akisimama hapa na kusema amewahi kumsaidia ndugu au rafiki yake akafanikiwa kupitia njia anayoishauri.
Kinachoshangaza ni kuona baadhi ya watu wakija hapa kueleza matatizo ya magari yao ilhali hata gari hawana. Mtu anakwambia viwanja vyote bora vya kula bata, lakini nyumbani kwao hali ni ngumu kiasi kwamba hata mahitaji ya msingi hayapatikani kwa urahisi. Tuache misifa na kujionyesha kusikokuwa na uhalisia.
Wengine mpo mjini mkijifanya maisha yamekaa sawa, wakati familia zenu vijijini zinategemea vibarua vya mashambani ili kupata chakula cha siku. Wapo pia wanaotumia Wi-Fi za watu wengine na kujenga picha ya maisha ya kifahari mtandaoni, wakisimulia kuhusu magari na vitu ambavyo havipo katika maisha yao halisi. Acheni ulimbukeni; tuwe wakweli kuhusu hali zetu. Na kabla mtu hajahisi kuguswa, niseme wazi tu kwamba sijamtaja mtu yeyote.