Nisihamishe au nihamishe familia na mke aache kazi?

MENISON

JF-Expert Member
Apr 26, 2013
726
622
Mimi ni mwajiriwa kampuni binafsi hapa Dar, na mke wangu yupo serikalini ngazi ya chini kabisa ya mshahara.

Nilifanya kazi yenye mshahara mkubwa miaka miwili iliyopita mikoani na nikafanikiwa kujenga nyumba tunayoishi na familia Dar.

Miaka hii miwili nilikuwa nadunduliza tu ila nimepata dili tena kama la zamani mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa mkataba wa miaka 3. Sasa nimeoa kuhamisha familia ndiyo naumia, maana hapo inabidi aache kazi anifuate, na kazi ya huko ni ya muda tu.

Na akihama kule atakuwa hana kazi.
Wadau waliowahi kukaa mbali na familia inawezekana kila baada ya mwezi au miwili kuicheki tu kwa miaka hiyo mitatu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mueleze mkeo hali halisi,then wewe nenda kapige kazi,maswala ya kuhama hama sio mazuri,kila baada ya muda flani wewe au yeye atakuja kukutembelea,hasa wewe kwa sababu huku ndio kuna familia.
 
muache mkeo aendelee na kazi na ataangalia na familia, we uende huko chuchu zone.
 
Mwache mkeo hapo kwako.
Au mkeo ni mzee wa kuruka mageti, unaogopa ukienda kanda ya ziwa atabaki anaruka mageti mpaka geti la 7.
 
acha familia nenda kapambane huku ukiwatembelea mara kwa mara.mbona issue ndogo hii mkuu 🚶🏿🚶🏿🚶🏿
 
Mi nakushauri kama unampenda mke wako nenda naye !! Kabisa ukimuacha

Ujue umekaribisha ufa ....yatakayokukuta utakuja kujuta
Kosa dogo litakukost

Wanawake ni watu wa kurubuniwa sana mimi yalinitokea km yako nikaacha mke ....mwaka wa tatu sasa imenibidi tu nitegane na mke wangu kwa kiwa alipata bwana mwingine kamjaza maeneno haambiliki kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
miaka 3 si kidogo na si mingi katika kutengana na familia yako.
ushauri, mwache shemeji na watoto wewe unafanya kuwafata pindi upatapo nafasi.
maana kuhamisha mji kuna maana kubwa sana,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom