Nishaurini: Nilipata division 3 kidato cha nne, nataka kurudia mtihani

Panda2

Member
Jul 4, 2016
7
2
Nimemaliza kidato cha nne mwaka jana na nikapata div3 ya 24, sinafanikiwa kuchaguliwa form5 na nimebaki njia panda juu ya hatima yangu. Nataka nirudie masomo niliyopata D na F mwakani kwani nina uwezo wa kufanya vizuri lakini tatizo nalazimishwa niende Veta. Je kupi bora??
 
nimemaliza kidato cha nne mwaka jana na nikapata div3 ya 24,sinafanikiwa kuchaguliwa form5 na nimebaki njia panda juu ya hatima yangu,,nataka nirudie masomo nliyopata D na F mwakani kwani nna uwezo wa kufanya vizuri,,,lakini tatizo nalazimishwa niende Veta,,je kupi bora??
Ndiyo ilivyo ukishindwa kujituma lazima utatumwa tu, sasa subiri huyo anayekulazimisha akufanye mtumwa wake maana hakuna namna
 
kwani nilazima usome shule za serikali?kama ni kidato cha 5 hata taasisi ya elimu ya watu wazima soma na ukafanye mtihani wa kidato cha sita ukiwa MTAHINIWA WA KUJITEGEMEA
 
Soma private candidate acha kubebeshwa mzigo ambao wewe unaona haupo akilini. Kulisiti sio mchezo na sikushauri utajuta. Uko mkoa gani kwanza maana huenda tunakupa ushauri kumbe huko uliko haya mambo ya private candidate huyajui. Hivyo mtoa mada rudi useme wapi umetokea bila shaka humu ndani tupo watu wa mikoa na wilaya mbalimbali
 
nenda Veta ila chagua fani zenye soko ktk ajira. fanya tafiti juu ya fani ukasome kwa bidii utatoka tu kimaisha. jiamini na umtegemee Mungu
 
maisha si Advance level tuu, kasome certificate up to bachelor ya course unayoipenda na yenye soko kwa sasa
 
SOMA VETA MIAKA 3 ILA CHAGUA FANI NZURI NA UNAYOUPENDA AMBAYO BADAE UTASOMEA SHAHADA YAKE.
WAKATI UNASOMA VETA HAKIKISHA UNARUDIA NW MASOMO YAKO YA FORM IV HATA KWA TUITION..UTAFANYA MTIHANI KAMA PC,
UKIFAULU UNAANZA KUSOMA MASOMO YA ADVANCE KWA TUITION PIA,, WAKATI HUO USHAMALIZA VETA TAYARI UNA UJUZI WAKO TENA HUENDA UKAWA AJIRA KABISA AU UMEJIAJIRI.
BAADAE UTAFANYA MTIHANI WA VI KAMA PC,, UKIFAULU TAYARI UNAENDA CHUO KUSOMA SHAHADA..(HAYA YANAWEZEKANA KAMA UNA NIA)
SASA UKIGOMA KWENDA VETA HUYO ANAYEKUSUPPORT ANAWEZA ASKUPE USHIRIKIANO.
PIA VYUO VYA VETA VIMEBIRESHWA SANA SIKU HIZI.
FANI ZIPO NYINGI NZURI.
NAKUTAKIA KILA LA HERI.
 
Back
Top Bottom