Nishauri Kwa nini Nirudi Kuishi Tanzania?

Kipanga

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
677
0
Mama,

Hizi zako ni dalili za ulimbukeni kama utaogopa kurudi kwenu eti kwa sababu kuna hali duni ya maisha, uchawi na mengine nadhani nina wasi wasi na uwezo wako wa kufikiri.. Huko unakong'ang'ania kukaa ukiamini ndio kuna mambo matamu ni kwamba wenye nchi walikaza buti wakaweka hayo mambo mazuri. Lazima walikumbana na hali ngumu kufika hapo walipo sasa nyie mnaotaka sisi tuwashauri kwa nini mrudi Tz eti mnaogopa ufisadi ni wafinyu wa busara na mitazamo pamoja na ma-degree yenu.

Mnapenda vitu ready made??? Kutoka jasho hamtaki kwani nyoka akiingia ndani ya nyumba yako unafanyaje?? Unahama nyumba kwenda kwa jirani???? au unamtafuta mpaka umtoe??? vijana ndio matatizo ya kukariri mambo.. Rudini tupambane hapa hapa kwetu hata kama nyie hamtafaidi vizazi vyenu vitanufaika tu hata huko mliko hayo mambo mazuri mnayoona waliweka watu siku nyingi sana si ajabu hata hicho kizazi kilipita....Mmeniboa sana!!!
 
Mama

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
2,849
0
Mama,

Hizi zako ni dalili za ulimbukeni kama utaogopa kurudi kwenu eti kwa sababu kuna hali duni ya maisha, uchawi na mengine nadhani nina wasi wasi na uwezo wako wa kufikiri.. Huko unakong'ang'ania kukaa ukiamini ndio kuna mambo matamu ni kwamba wenye nchi walikaza buti wakaweka hayo mambo mazuri. Lazima walikumbana na hali ngumu kufika hapo walipo sasa nyie mnaotaka sisi tuwashauri kwa nini mrudi Tz eti mnaogopa ufisadi ni wafinyu wa busara na mitazamo pamoja na ma-degree yenu.

Mnapenda vitu ready made??? Kutoka jasho hamtaki kwani nyoka akiingia ndani ya nyumba yako unafanyaje?? Unahama nyumba kwenda kwa jirani???? au unamtafuta mpaka umtoe??? vijana ndio matatizo ya kukariri mambo.. Rudini tupambane hapa hapa kwetu hata kama nyie hamtafaidi vizazi vyenu vitanufaika tu hata huko mliko hayo mambo mazuri mnayoona waliweka watu siku nyingi sana si ajabu hata hicho kizazi kilipita....Mmeniboa sana!!!Pole kwa kukuboa na ufinyu wangu wa busara, lakini maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua. Kurudi nyumbani kupambana mapambano yasiyo kwisha na jasho kutoka kwa miaka 48 (ya uhuru) na hali inazidi kuwa mbaya kila siku? yaani kila siku ni kulalamika kwa kukata tamaa, ni afadhali kulalamika wakati matumaini yanaonekana. Sio kwamba sitaki kurudi nyumbani per se, bali niko kwenye enigma kuhusu hali ya hapo nyumbani! especially ya kisiasa na kiuchumi.
 
Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,338
2,000
kama maisha ni popote, basi afadhali kuishi nchi nyingine zaidi ya Tanzania. Kila sehemu ina matatizo yake, lakini matatizo huko nyumbani mweee yamezidi. Mentality yangu ya kurudi nyumbani inazidi kupotezwa na hayo mambo ya ufisadi, uchawi, hali duni ya maisha ya wastani ya mtanzania, why?

sitaki juaribu kurudi nyumbani, nataka niwe na yes au no, yaani nirudi au nisirudi, maisha nimeshayajaribu sana na umri umeshakwenda. What I need now is just to make a decision wapi nijikite kimaisha.

Pole sana ndugu yangu, unanikumbusha kuna wakati naanza kuona ndoa za waafrika nikaapa sitaolewa na mtanzania, kwani ni wapuuzi wote.
lakini hata wewe unajua si kweli kuwa unaweza kugeneralize such a big issue kuwa either black or white.
Najua kuwa unajua kuwa si tanzania yote ambayo inajihusisha na uchawi, siasa, ufisadi na hali duni..
ndo sababu nikakuambia, jifunze, panua mawazo yako,
hio nchi utakayoenda unasoma tabloids zake? mambo ya ajabu yanayotokea huko wewe yanakuathiri mojakwamoja? basi na huku tz pia ni hivyo.
mfano mimi sijawahi hata kupata uthibitisho wa uchawi hadi leo hii, nasoma tu na kusikia kama wewe.
 
Uchawi unaweza kuwa minor issue, ila pale viongozi wako wanapojihusisha na mambo kinyume na maadili ya uongozi halafu hawawajibishwi hata kidogo zaidi ya issues kuzimwa kisiasa inatia uchungu sana. Kubwa zaidi ni hilo la ufisadi, najua hata nikirudi nyumbani sitaweza kuleta mabadiliko au hata kuingia kwenye hiyo system ya kuleta mabadiliko (nchi ina wenyewe hiyo).

Nilipo mambo ya ufisadi pia yapo, lkn at least most of people wanaishi standard life, tajiri na maskini wote wana umeme, maji, wana access na quality education and quality health services. Ninashop duka wanaloshop matajiri. Tunalozidiana ni starehe tu, ila basic services wote tunapata.
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
7,416
2,000
Mtanganyika, Heshima mbele,

Kwa mtazamo wangu, jina lako pekee lina nituma nikushauri urudi kuishi Tanganyika, you see how it sounds sweet!!!!. Jingine ni kwamba nimekuwa nasoma threads zako hapa JF na zinanionyesha una uchungu sana na hii nchi. Regardless kama huko uliko unakula mkate na siagi au na peanut butter Nyumbani ni nyumbani tu.

Sidhani kama unaichukia Tanzania kwa mantiki kwamba ni mbaya, ila unauchukia UNAFIKI, WIZI, UFISADI, POROJO, KIBURI CHA TULIOWAPA MADARAKA,na matendo mengi machafu wanayo yafanya viongozi walioko madarakani. But mind you brother, they are not there to stay, wataondoka, tunaamini iko siku watakuja viongozi wazuri wenye uchungu na Tanzania yetu nzuri, and we will flourish.

Kuna msemo unasema fimbo ya mbali haiui snake brother, hivyo ni vyema uje tushirikiane kuwaambia hawa Mafisadi kwamba sasa BAAASIII!! We need changes. Nadhani utakubaliana nami nisema HABARI NDIYO HIYOOO!!.

Usitufanye tuseme Mtanganyika anataka kutuachia haya mapambano sisi wenyewe. UNITED WE SHALL STRIVE. Tusilale mpaka kieleweke.
Karibu Tanzania Man!!!
 
Mama???

Usiwavunje moyo wanao, Kwenye mapambano sio lazima wote wawe frontline, Kwa wewe kupiga kelele ni mojawapo ya kelele za mapambano ambayo yataleta mabadiliko. Huhitaji kuwa Makamba Au Jk. ili kuwa badilisha hawa mafisi maji. Hata Nyerere hakushika bunduki lakini Idd Amin alimuogopa na akakimbia nchi kuonyesha ameshindwa na Nyerere. Hii ya NYERERE pia iliwapa ARI wapiganaji wetu hata ushindi ukawa ushindi mkweli. MAMA, pls do not stop piga kelele!!! Kemea ujinga, laani Ufisadi, Ombea Taifa kwa Mungu, tutapata viongozi commited na wenye uchungu na hili Taifa. Huu unatosha kabisa kuwa mchango mkuu kuliko hata kuingia kwenye system. Naogopa ukiingia kwenye system ukikutana na hawa MAFISI MAJI watakufundisha ufisadi. Let us eradicate them first, then uingie na watu safi.
 
MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,104
2,000
kwenu ni kwenu labda uwe mtumwa! Usiporekebisha kwenu nani arekebishe?

Mimi kusema ukweli tangu nimefika hapa takribani miaka 6-7 iliyopita na napata huduma nzuri ya kimaisha tena nzuri sana angalia intenet chumbani ,kila kona nikipita naweza kuifikia,maji ,elimu ,maradhi na mengine mengi LAKINI LAKINI Hata siku moja sijawahi kufurahia maisha yani ku feel kama niwapo nyumbani Tz ,yani hua siku zote nahisi namiss kitu.

Lakini hata hivyo Mtu huwezi kurudi kichwa kichwa eti unaenda kupambana mimi bado nafikiri mapambano yaliyo natija ni yale ambayo utawezesha ndugu na jamii kwenda shule hii mie ndio nafikiri ni strategies nzuri kuliko zote,kivipi kurudi bila misingi sitahiki madhara yake ni makubwa .

Hata hivyo mapambano ya mikuki na upande wa pili una B52 hayo sio mapambano ,hapa namaanisha kua watu walio nje kurudi ni vizuri kama tu wameshavuna chochote ambacho wakirudi kitawafanya wawekeze na sio kurudi tena kugombania ajira na walioko huko eti na tena wakijifanya kupambana kwa mikuki na mtu aliye na B52.

Hapa nasema hivi mimi siwezi kutoka hapa nikaenda nikajiriwa na wizara fulani harafu nikaendesha mapambano ya kupambana na waziri wangu ama Rais ,sanasana kitakachotokea ni ule mchezo wa watoto wasichana wa kamba .
 
Yo Yo

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,216
0
Aisee Mtanganyika,
Swali lako liansumbua wengi sana kifupi mkuu usije bongo kichwa kichwa kabisa hata ukija na $ Mil zitaliwa an wajanja mpaka utakuwa chizi.Kuna jamaa alikaa majuu miaak mingi an maisha yake yalikuwa mazuri tu akathubutu kurudi bongo na vijisenti vyake,sasa hivi ninavyoongea kashaenda ubalozini kuomba visa mara kibao anatoswa anataka kukimbia nchi.Kifupi kachoka.

Unaweza kuwa huko huko an nchi ukaijenga haya ya fimbo ya mbali.....hayana mantiki kipindindi hiki cha Globalization dunia imekuwa kijiji,njoo usalimie tena usikae sana(2weeks zinatosha) acha vijisenti rudi kapambane huko ulipo.
 
Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,749
2,000
...nimebahatika kujenga katika 'kisiwa' kidogo pembezoni ya jiji la dar es salaam kinaitwa Kigamboni, na haya ndiyo yaliyonisibu 'nilipokwenda' nyumbani kujaribu upepo!;

Usafiri; Kutoka ng'ambo moja ya kivuko kwenda upande wa pili ni safari inayochukua masaa hata manne kwa pantoni, (hii ni pamoja na muda wa kusubiri). Pantoni yenyewe mara kwa mara ilikuwa inakongoloka mlango wa kutokea magari, hivyo ilikuwa inabidi ku reverse gari wakati wa kutoka!

Mara nyingi foleni ya kutoka 'kisiwani' ilikuwa inaongezeka kutokana na 'wale watukufu' pale getini kuruhusu gari za washikaji zao, na wengineo wanaotoa kitu kidogo na hivyo kuruhusiwa kupitisha magari kwenye mlango wa dharura achilia mbali magari ya STG, na jeshi ambayo ni mengi mno yanayopitia hapo, hasa peak hours!

Alternative nyingine kuepuka kero hiyo ya 'kivuko' ni kuzungukia Kongowe, ambako nako raha yake inaishia pale mbagala, kuna foleni za dala dala, na msongamano wa magari ambayo nayo yanakimbia foleni ya kivuko, na wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo.

Foleni nyingine ya 'kufa mtu' utaikuta pale wachina wanapojenga barabara ya kilwa, maeneo ya sabasaba mpaka mtoni kwa aziz Ali. Ukijifanya hamnazo kuwasha kiyoyozi sana sana utajikuta 'wese' likuishia kwenye hiyo foleni.

Hiyo cocktail ya Juakali, Joto Vumbi na dala dala inakufanya ujiulize mara mbili mbili kama una ubavu kupambana na road rage ya madereva wenzio!

Umeme nao; ...njia peke ya kupata umeme hapo maeneo ya 'kisiwani' nilipojenga ni kuchangishana na wananchi -'wanakijiji' -wenzangu kiasi cha Milioni 9.5 kufanikisha kuvuta nguzo, nyaya pamoja na usajili wa umeme, otherwise kwa ufinyu wa bajeti zao (wanakijiji wenzangu), ndio nastahmili tu na 1st aid box toka china, kifaa kinachoitwa Inveter kuzalishia umeme. Labda mwaka 2010 Mbunge akija kupiga debe la kuombea kura naye tumbane atuongezee nguzo!!!

Kinyume na hapo, Bongo ni pesa yako tu, ukiwa na kisomo na ukapata ajira nzuri, au mradi unaokuingizia 'vijisenti' kila siku, maisha ni bora kuliko ulaya na marekani, kwani mpaka sasa, Tanzania unaweza ukajipatia vitu kama ardhi kwa bei nzuri tu, na ukafanya investments za kutosha.

Kwahiyo, wale walioondoka siku nyingi, licha ya kero za hapa na pale, (achana na hizo kubwa kubwa za mafisadi) hali nyumbani Tanzania si mbaya kama uisomavyo kwenye internet...hata ukitembea mjini, vijana kwa wazee wengi 'waliokubaliana na maisha' utawakuta na tabasamu pana tu usoni, hata kama uwezo wao ni window shopping maeneo ya mlimani city!

Hayo ni maoni yangu, toka jijini Dar es Salaam.
 
Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,324
0
Ninaweza mshauri kaka yangu Mtanganyika na wengine, ni vema mrudi Home ili mtufundishe sense ya kuwajibika. Bahati Mbaya nchi yetu imeoza kila eneo na inahitaji wapambanaji ambao watasaidia kwa namna moja au ingine kuboresha Hali iliyopo.

Mfano kama wewe ni Dr. na ukabahatika kuwa Dr. Mkuu wa Amana au yoyote alau utakuwa na uwezo kubadilisha nature ya utendaji wa taasis japo moja ya serikali.
 
Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,338
2,000
kama walivyosema wengi hapo juu, simamia maneno yako, yatekelezeke.uungwana ni vitendo.
 
Kimweri

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
3,999
2,000
wale ambao wanafikiria kurudi tanzania baada ya kuishi nje ya nchi ni kazi rahisi basi hawajawahi ishi majuu!!
kama wanafikiria kuja kijisemina cha wiki 2 au mwezi mmoa nako ni kuishi majuu basi u are wrong!!its not that simple 2 judge.
bahati nzuri wengi wanaoishi abroad wameshawahi ishi tanzania(kwa kuzaliwa,wengine wamesomea tz)
ukweli mchungu ni kuwa life is way easier abroad,naongelea LIFE integrity.being who you really are,affording what you deserve na infinite opportunities.
life abroad can be hard,BUT its always in a positive way, i.e overcoming hardships mostly provides rewards.
kuishi tanzania sio tatizo, ila ukiondoa factor ya familia,ndugu na uzalendo.there is absolutely NO other reason.
kwa wasioamini samahani sina nguvu za kuwaaminisha.ila ndio painful truth.if only life was fair!!
 
Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,338
2,000
Kimweri, nakubaliana na wewe kabisa, ila watu wanatofautiana katika priorities.
je uazalendo na upendo wa ndugu ni muhimu kuliko kipato, huduma unazopata huko binafsi?
kwa vijana ni muhimu wajifunze kwa kuzunguka dunia nzima kila wanapopata nafasi.
baadae wanaweza jichagulia mahali pa kutulia kulingana na mahitaji yao.
mara nyingi wengi wanapenda kurudi nyumbani.
Home is where the heart is.
kama tanzania mtu hana mapenzi na tanzania hakuna haja ya kurudi.
in many cases hakuna mtu wa kumiss mwenzie, hakuna uwapendao kwa nini urudi?
lakini hata kama unamiss nyumbani na huna cha kuwapa, bora ubaki uliko uhangaike, ukienda TZ umejiandaa kimaisha.
 
PlanckScale

JF-Expert Member
Sep 28, 2008
550
250
My personal experience has been quite the opposite:
I lived in New York City for 15 years, and I had a great job for the last 9 years of my stay. Growing up in Dar es Salaam during the 1980's, we had great times, parties, disco, Hellenic Club, Italian Club, Gymkhana, you name it – we did it all. Life was good back then. Therefore, going to New York City was like going to Mecca. The city had\has everything you can imagine; clubs, book stores that stay open through out the night, tennis courts that have lights at night, music stores (god, I used to spend countless hours searching for oldschools!), great food from allover the world, the people, the freedom of expression. You also have access to good education, great proffesional environment, and the assurance of emergency services, (bongo ukigongwa kasheshe :( ). But, despite all that, it was an empty life. I never felt complete in America. It always felt like I was in transit – from somewhere...going somewhere…

Yes, ndugu na uzalendo played a role (tulinyweshwa maji ya bendera huko JKT :) ), but now that I am reflecting on it, it was probably a combination of all things that make a person complete, and being among "your people" is a critical part of it. The friendships I had in the US were at a superficial level. There were not historical and cultural links to associate with, which leaves one feelling empty inside - "Yeah what's up, how is the weather, the knicks ain't gonna make it this season...". That was it. No depth. We had to comeback. And after a long preparation, when the time came, we were ready...We came back.

It is true, TZ kuna matatizo ya maji, umeme, foleni zamagari, watoa huduma wazembe, ufisadi, na kadhalika. Lakini vyote hivyo tisa mwanangu. Ukijiandaa kurudi na kuweka mambo sawa...BONGO POA. Basically, I went there not to stay, but prepare myself to come back and LIVE!
 
Nikifufukammekwisha

JF-Expert Member
Aug 17, 2007
260
0
Mtanganyika, Do you really believe you have no reason to come back home? Do you really believe Tanzania is a wrong place for you in all walks of life? So you are convinced that you can not change the situation and you have nothing to contribute? So you feel that you have nothing to loose and you can live wherever you are peacefully and let whatever is happening there continue? Therefore you wish you were not born Tanzanian. Kama ni hivyo, don't come back, endelea kubeba ma-box. But Idon't want to believe umefikia hatua hiyo and perhaps thats why you call yourself Mtanganyika. Hebu acha mentality ya kitumwa hiyo! Tanzania is still one of the best places kuzidi hata huko mliko, nakushauri tu malizia mipango yako urudi home, our beautiful land!

Kwahiyo ndugu Scorpion unataka niambia kwamba it is possible for individuals like you and me ku-make changes in the existing situation hapa nyumbani bongo? na una-encourage watu wengine kuja kutusaidia ku-make hizo changes?

I believe in a lawless society like ours it is not easy to accomplish your dreams of changing the country to the better... Angalia mkulu mkubwa kabisa wa nchi, kapewa orodha ya mafisadi ambao in the first place hakupaswa kupewa hiyo orodha kwa kua anawafahamu.. What has he done as of late? Je, kwa kutumia uamiri jeshi wake mkuu tuliomkabidhi pale alipoapishwa kutuongoza, je kawaweka hawa watu into custody? Je, Nyerere angetumia the same approach anayotumia huyu jamaa? Kwa hiyo vilevile unataka kuniambia kwamba pamoja na mkulu mkubwa kabisa kutuchezea akili zetu bado it is possible for individuals ku-struggle ku-make change na kuwa succesful? To me I think it is a WASTE OF TIME AND RESOURCES...........
 
Nikifufukammekwisha

JF-Expert Member
Aug 17, 2007
260
0
...nimebahatika kujenga katika 'kisiwa' kidogo pembezoni ya jiji la dar es salaam kinaitwa Kigamboni, na haya ndiyo yaliyonisibu 'nilipokwenda' nyumbani kujaribu upepo!;

Usafiri; Kutoka ng'ambo moja ya kivuko kwenda upande wa pili ni safari inayochukua masaa hata manne kwa pantoni, (hii ni pamoja na muda wa kusubiri). Pantoni yenyewe mara kwa mara ilikuwa inakongoloka mlango wa kutokea magari, hivyo ilikuwa inabidi ku reverse gari wakati wa kutoka!

Mara nyingi foleni ya kutoka 'kisiwani' ilikuwa inaongezeka kutokana na 'wale watukufu' pale getini kuruhusu gari za washikaji zao, na wengineo wanaotoa kitu kidogo na hivyo kuruhusiwa kupitisha magari kwenye mlango wa dharura achilia mbali magari ya STG, na jeshi ambayo ni mengi mno yanayopitia hapo, hasa peak hours!

Alternative nyingine kuepuka kero hiyo ya 'kivuko' ni kuzungukia Kongowe, ambako nako raha yake inaishia pale mbagala, kuna foleni za dala dala, na msongamano wa magari ambayo nayo yanakimbia foleni ya kivuko, na wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo.

Foleni nyingine ya 'kufa mtu' utaikuta pale wachina wanapojenga barabara ya kilwa, maeneo ya sabasaba mpaka mtoni kwa aziz Ali. Ukijifanya hamnazo kuwasha kiyoyozi sana sana utajikuta 'wese' likuishia kwenye hiyo foleni.

Hiyo cocktail ya Juakali, Joto Vumbi na dala dala inakufanya ujiulize mara mbili mbili kama una ubavu kupambana na road rage ya madereva wenzio!

Umeme nao; ...njia peke ya kupata umeme hapo maeneo ya 'kisiwani' nilipojenga ni kuchangishana na wananchi -'wanakijiji' -wenzangu kiasi cha Milioni 9.5 kufanikisha kuvuta nguzo, nyaya pamoja na usajili wa umeme, otherwise kwa ufinyu wa bajeti zao (wanakijiji wenzangu), ndio nastahmili tu na 1st aid box toka china, kifaa kinachoitwa Inveter kuzalishia umeme. Labda mwaka 2010 Mbunge akija kupiga debe la kuombea kura naye tumbane atuongezee nguzo!!!

Kinyume na hapo, Bongo ni pesa yako tu, ukiwa na kisomo na ukapata ajira nzuri, au mradi unaokuingizia 'vijisenti' kila siku, maisha ni bora kuliko ulaya na marekani, kwani mpaka sasa, Tanzania unaweza ukajipatia vitu kama ardhi kwa bei nzuri tu, na ukafanya investments za kutosha.

Kwahiyo, wale walioondoka siku nyingi, licha ya kero za hapa na pale, (achana na hizo kubwa kubwa za mafisadi) hali nyumbani Tanzania si mbaya kama uisomavyo kwenye internet...hata ukitembea mjini, vijana kwa wazee wengi 'waliokubaliana na maisha' utawakuta na tabasamu pana tu usoni, hata kama uwezo wao ni window shopping maeneo ya mlimani city!

Hayo ni maoni yangu, toka jijini Dar es Salaam.

Ndugu yangu Mbu,

Hii kadamnasi uliyoizungumzia kwenye maelezo yako, ina-occupy asimilia ngapi ya Watanzania? Na je, hao uliowazungumzia je ndugu zao wa karibu wanaoishi hapo hapo Dar ama vijijini kama kule Dar-Pori Ruvuma je nao wana uwezo wa kuchanga izo milioni 9 na kuvuta umeme?

I strongly believe that Tanzania yetu bwana tatizo kubwa ni sisi wenyewe kutokujua what we deserve. Tunalipa kodi nyingi sana kwa serikali in terms of VAT, stamp duties, makato kwenye mishahara, kodi kwenye petroli ama dizeli nk.. BUT, the government haifanyi kazi inayopaswa kufanya kwa kuwekeza kwenye HUDUMA MUHIMU in terms of mahospitali, mashule yenye quality ya kueleweka (sio mabanda), mabarabara.. Badala yake Serikali yetu inawekeza kwenye mambo ya ki-luxury wakati raia wake ni masikini, kama vile kuongeza idadi ya semina zisizo na mpango wowote, ununuzi wa ma-VX, ujenzi wa bunge jipya, ununuzi wa very advanced radar tusiyokuwa na equipment/teknolojia ya kuitumia na kadhalika.
 
Nikifufukammekwisha

JF-Expert Member
Aug 17, 2007
260
0
Mtanganyika, Heshima mbele,

Kwa mtazamo wangu, jina lako pekee lina nituma nikushauri urudi kuishi Tanganyika, you see how it sounds sweet!!!!. Jingine ni kwamba nimekuwa nasoma threads zako hapa JF na zinanionyesha una uchungu sana na hii nchi. Regardless kama huko uliko unakula mkate na siagi au na peanut butter Nyumbani ni nyumbani tu.

Sidhani kama unaichukia Tanzania kwa mantiki kwamba ni mbaya, ila unauchukia UNAFIKI, WIZI, UFISADI, POROJO, KIBURI CHA TULIOWAPA MADARAKA,na matendo mengi machafu wanayo yafanya viongozi walioko madarakani. But mind you brother, they are not there to stay, wataondoka, tunaamini iko siku watakuja viongozi wazuri wenye uchungu na Tanzania yetu nzuri, and we will flourish.

Kuna msemo unasema fimbo ya mbali haiui snake brother, hivyo ni vyema uje tushirikiane kuwaambia hawa Mafisadi kwamba sasa BAAASIII!! We need changes. Nadhani utakubaliana nami nisema HABARI NDIYO HIYOOO!!.

Usitufanye tuseme Mtanganyika anataka kutuachia haya mapambano sisi wenyewe. UNITED WE SHALL STRIVE. Tusilale mpaka kieleweke.
Karibu Tanzania Man!!!

Hao mafisadi wataondokaje wakati wanarithishana kwenye utawala? Umeangalia kikao cha vijana wa CCM kwenye blog ya Michuzi? Unafikiri mtoto anaweza kuja mkamata baba ake baadaye kwamba alikua mwizi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom