Nishauri kati ya biashara ya nyama choma na barbershop nifanye ipi?

lup

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
2,514
2,732
Za asubuhi jamani..

Leo nimejikuta katika mawazo sana lipi la kuamua. Kuna pesa natarajia kuipata very soon... Sasa nawaza kufanya biashara ila nimeshidwa kuamua nimeona nipate mawazo kwanza kwa wadau..

Barbershop..
Nawaza kama ni barbershop nifungue yenye hadhi nzuri na ikibidi nichanganye na saloon ya like na maeneo nilipo Niko mwanza ila nafikilia kuweka mle mwanza moral. Yaani niifanye iwe inaweza kuingiliwa na watu wa hadhi zote.

Nyama Choma
Lakini pia kuna wazo linakuja kwa kasi la kuhusu kufungua nyama choma yenye vinywaji baridi kwani imani yangu hairuhusu pombe...

Kati ya biashara hizo tafadhali mnisaidie mawazo.
 
Fanya hivi nenda kajichanganye kwenye banda la nyama choma, jua nyama wananunua wapi, wananunua kiasi gani, wateja muhimu kina nani, siku zipi zinabiashara sana,hasara na faida then Fanya hivyo na hiyo nyingine then Fanya uchaguzi mwenyewe biashara sio ya kuchaguliwa na mtu hili ni angalizo usitake sisi tuseme ila chagua mwenyewe
 
Fanya ya babashop haina presha mwanzo ytakuw mgumu then baadae itasimama Mimi Nina babashop cha kufanya elewana na vinyozi wako kila kiti wakupe kiasi gani kwa siku ila nyama choma sikushauli life ya kuchoma sana nyama imepungua kwa sasa
Mkuu kama hautojari naomba nije inbox tuongee kidogo
 
Kama una sehemu nzuri fanya biashara ya nyama choma n ugali wa dona na ulezi,halafu weka reliable price...aisee utapata hela sana
Mkuu una uzoefu na hii biashara?
 
Mkuu una uzoefu na hii biashara?
Sina uzoefu ila nina jamaa hii biashara imemtoa yuko vizuri..kiasi kwamba sasa anifikiria kujenga mgahawa wa kisasa kila wilaya tanzania
 
  • Thanks
Reactions: lup
Kama unaweza kupata bar nzuri na kubwa hapo mjini,wewe unafungua jiko (mgahawa) hapo bar
 
  • Thanks
Reactions: lup
mk
Fanya ya babashop haina presha mwanzo ytakuw mgumu then baadae itasimama Mimi Nina babashop cha kufanya elewana na vinyozi wako kila kiti wakupe kiasi gani kwa siku ila nyama choma sikushauli life ya kuchoma sana nyama imepungua kwa sasa
mkuu nieleweshe kidogo hapa..je huyo kinyozi atakua anakulipa kwa mwezi,wiki au kwa siku au we unafanya vipi mkuu...?
 
sikushauri uweke pombe na nyama choma ila kinyozi iko poa ila kama ni mzur katika kunyoa.
 
  • Thanks
Reactions: lup
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom