Nishauri kampuni nzuri ya bima

kibebi

Senior Member
Feb 22, 2013
108
247
Heri ya mwaka mpya 2017,

Wana JF, wakati wa kukata bima ya gari umefika ila niko njia panda kuhusu kampuni ya bima ambayo haitanipa wakati mgumu kama ikitokea nimepata matatizo. Nilikuwa mteja wa jubilee ila sijavutiwa na huduma zao.
Ninaomba wenye uzoefu na kampuni zingine wanisaidie mawazo.
ni bima comprehensive.

Asanteni

kbb
 
Mkuu wewe unataka Third party au comprehensive? Nijibu kwanza hapo harafu nikushauri company ya kukata!!!
 
Comprehensive
Kwa upande wangu huwa natumia company ya Reliance insurance company Ltd wako vizuri japo sijawahi kupata shida ila nilishawishika baada ya watu wangu wa karibu niliona wakihudumiwa vizur pindi wapatapo matatizo huu mwaka wa 6 niko nao, kama uko dar nenda UN Road, upanga reliance House kama ni mwanza neenda uhuru Street ukisimama hapo garden/kemondo bango lao liko hapo hapo waga linaonekana kirahisi zaidi unapotokea barabara ya airport.
 
Zingatia ushauri unaopewa humu na iepuke kampuni ya Zanzibar Insurance. Hawa jamaa waswahili sanaaa.
 
Back
Top Bottom