Nishati ya umeme chooni

Mnyenz

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
1,425
4,321
Habari zenu wakubwa kwa wadogo, bila kupoteza muda wala manjonjo naenda kwenye mada.

Kipindi fulani miaka ya nyuma nilikua nikisikia sana kwamba kuna namna ambayo mtu anaweza kupata nishati ya umeme kwa kuunganisha nyaya moja kwa moja kutoka chooni.

Habari hii niliisikia zama zile nakua nami niliamini(japo sikuwahi kushuhudia) ila nilisikia lilikua ni kosa kubwa sana kufanya utaalamu huo kwa kuwa ilikua ni hatari sana kwa usalama wa maisha na nyumba za wahusika kwani naskia umeme uliokua unazalishwa na chanzo hicho ulikua ni mkali sana( huenda tulikosa teknolojia ya kuupoza).

Sasa basi naona muda umeenda sana, tumekutana na mabadiliko mengi sana ya kiteknolojia na pia tumesomesha vijana(kama taifa)wengi sana katika sekta hiyo ya mambo ya umeme.

kwa mawazo yangu machache napendekeza wataalamu wetu wapewe jukumu la kujaribu kufuatilia aina hiyo ya nishati(umeme wa chooni) ili kama inawezekana basi tuitambulishe teknolojia hii kwa ulimwengu kwani kwa sasa naamini umeme huo(kama upo kweli) hautaweza kuwa tishio tena kwa maisha yetu kwani teknolojia imekua sana tunaweza kuupoza makali na ukafaa hasa maeneo ya vijijini ambapo hakufikiki kirahisi na nyaya za Tanesco.

UKIONA MTAANI KWENU HAKUNA MWENDAWAZIMU JICHUNGUZE SANA, YAWEZEKANA UKAWA NI WEWE.
 
Back
Top Bottom