Nishati: Makosa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Pili - Kifo cha Kiwanda cha kusafisha mafuta TIPPER

kipindi cha awamu ya pili kinalaumiwa kwa mambo mengi lakini je mambo yote yalitokea ndani ya miaka michache tuu? je haiwezekani kuwa walirithi matatizo? je, nyerere alistaafu kwa kuwa alichoka kutawala ?alikataa kugeuka jiwe? au kwa kuwa alishasoma alama za nyakati kuwa hali ya nchi haikuwa tena nzuri kwake?
vipi kuanzishwa kwa uchangiaji wa gharama za matibabu na huduma za afya kuanzia 1993, jee, ilitokana na ubovu wa sera za awamu ya pili au baada ya serikali kushindwa kumudu gharama kubwa za uendeshaji wa sekta ya afya? je mnaamini huo pia ulikuwa ni uamuzi mbovu wa serikali ya awamu ya pili
hivi nyerere angeendelea kutawala mpaka 1990, mapinduzi yasingetokea nchi hii?maana hata yeye kipindi chake cha mwisho alifail vibaya
 
jambo moja ambalo naamini ni kuwa marais wote wanne waliopata kupita nchi hii mpaka sasa, miaka yao mitano ya mwisho wamefail sana, si nyerere, mwinyi, mkapa na kikwete ambaye atavunja rekodi ya kuharibu kwa wote hao
 
yawezekana ikawa kweli tiper ilikufa wakati wa mwinyi, lakini yawezekana ilikuwa tayari imeshajichokea soo mwinyi akadondokewa na jumba bovu tu, kwani viwanda vingi vilivyokuwa vya umma vikabinafsishwa baadae je havikuyumba enzi ya mwalimu??? mbona pia utawala wa mwalimu unalaumiwa kwa kulea wezi wachache au wale waliokuwa wakiharibu hapa na kusogezwa kule kwa kisingizio kuwa hakuna wataalamu wengine? hili laweza kuwa sawa na mgonjwa aliyecheleweshwa kuletwa kituoni kisha akaja kufia mikononi mwa daktari na kuishia kumlaumu dr kwamba kasababisha kifo cha mgonjwa ilhali mgonjwa mwenyewe alikuwa dhoofu,
binafsi, naamini mashirika mengi ya umma yaliyumba kipindi cha mwisho cha utawala wa nyerere kutokana na sababu mbalimbali za ndani na za nje, na mind you, mashirika mengi yalitegemea ruzuku ya serikali lakini nyie nyote mwajua serikali haikuwa na pesa sxasa mashirika hayo yangejiendeshaje???
naomba nifundishwe na nielekezwe kwani nimepata kusikia kuwa kipindi mwinyi anaingia nchini(nikimquote warioba alipohojiwa itv kwenye dakika 45 ) kwamba wao walipokea nchi ikiwa haina hela kabisa na mfumuko wa bei ulikuwa 36%, lakini mpaka mwaka 1990 mfumuko ulipungua kufikia 18%, na yeye akajinasibu kuwa hayo kwao yalikuwa mafanikio makubwa katika serikali ya kipindi chake, sasa kwa kuwa mashirika mengi ya uma yalitegemea ruzuku yangeendeleaje???
unless tuelezwe vinginevyo kwamba mpaka 1985 , TIPER ilikuwa ikiendeshwa kwa ufanisi ila kuanzia 1986-its death ndo ilianza kuyumba nitaamini ni sababu ya mwinyi, vinginevyo mimi nitaamini nyerere na utawala wake walichangia kumchelewesha mgonjwa ila akaja fia mikononi mwa daktari, lawama iwe pande zote to be fair
Ndugu tuko kwenye uwaanda huu wa uchumi na biashara, na mimi to be honest you have a point.
Ni kweli Mzee Ruksa alirithi a skeletal economic situation toka kwa Mwalimu.
Na Mwalimu aliona the writting on the wall.
Hata hivyo mabadiliko ya kiuchumi yalikuwa whole sale.
Katika Mashirika yaliyokuwa yakizorota TIPER lilikuwa mojawapo.Lakini je tujiulize, hivi imagination zetu ziliishia na Mwalimu?
Kwa Mwalimu ilikuwa Mtanzania kwanza, mtu mwingine baadaye, iwe kiuchumi kiutamaduni au vinginevyo.
Kimsingi Mwalimu alipatia sana ile siasa ya kudhibiti njia kuu za uchumi-hili halina mjadala maana ni strategic.
Kwamba Mzee Ruksa aliachia njia hizo zichukuliwe , tena whole sale na kwa kuzivunjilia mbali ni dhambi tuanayolilipia hadi leo.
Sekta ya nishati haijatengemaa toka miaka ya mzee Ruksa, na imeingiliwa na wageni wenye strategic interests za kwao wenyewe na si za nchi.
Wanakuja watu wanasema gesi ndio mkombozi-lakini kwa biashara yao wkirudisha pesa zao wanatimka
Wengine wanakuja na vijenereta na capacuty charges -wakitutoa mahela wanatimka
Wa kuuza mitambo hewa -nao wakifanikiwa wanatimkia mbali.
Halimradi sekta ya nishati ni kichwa cha mwenda wazimu.
Kwani pamoja na matatizo yake baada ya Mwalimu tuliacha kufikiri?
Au leo ni 10% kwanza kabla ya mradi wowote wa nishati.
Nakukumbusha tu, ndugu yangu Matambo, kuwa nchi ya Zambia hakufanya upuuzi wa kuua kinu chao cha mafuta toka miaka hiyo, kimeboreshwa na wanaendelea kudhibiti nishati ya mafuta hadi leo, wakati sisi tulitupa jongoo na mti wake.
 
Mkuu Uporoto1, you are PLAIN WRONG on this issue.
Peruse your facts to refresh your self.
TIPER ilikuwa inafanya kazi hadi 1991, licha ya kuwa na migogoro.1991 Rais alikuwa Mzee Ruksa na si Mwalimu.
Mwalimu alisimamia ujenzi wa kiwanda hiki kna kuki-commisiion mwaka 1969.
Please read your history well.
Naaambatanisha hii reference toka net.

Tiper Refinery - Simple Oil Refinery in Dar es Salaam, Dar es Salaam, Tanzania

::
Overview:: Refinery Units:: Contact Details:: General Information:: Related Organisations:: Contact Information

:: Update :: Upgrade
[
Overview
The Tanzanian and Italian Petroleum Refining Co Ltd (Tiper) refinery at Dar es Salaam, Tanzania was originally built between 1963 and 1966 and commissioned in 1969. It is a topping and reforming refinery with a nameplate distillation capacity of 875 ktonnes per annum (17,500 bpd) but is generally operating at approximately 60% of rated capacity. The refinery is a limited company incorporated in Tanzania under the parastatal Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC). The shareholders of the company are the Treasury of Tanzania (50%) and Agip (50%) who are also the refinery's operators.
Since 1991 the refinery has been undergoing rehabilitation and modernisation in order to increase its efficiency, safety standards and output. The rehabilitation is (was)intended to restore output to its nominal capacity despite a recommendation by the World Bank, strongly opposed by the Tanzanian government, that the refinery be closed. The Tanzanian government is of the opinion that the refinery is essential to the Tanzanian economy and are working to keep it operating.The upgrading programme also includes a revamp of the boiler and the installation of a new instrument panel. TPDC has also considered installing conversion units in order to boost the yield of white product.

(source and ref: mBendi.com)

Kiwanda kilikuwa scrapped during the second half ya awamu ya mzee Ruksa.
Be informed.
Mkuu miaka hiyo nilikuwa nafanya kazi katika kampuni ya mafuta HAMNA REHABILITATION iliyofanyika,kulikuwa na mpango huo na kweli vifaa vingi vililetwa lakini Grupo ENI kampuni mama ya Agip walikuwa wanataka kwa kugharamia ukarabati na serikali kutokuwa na hela za kuchangia basi waongezewe shares ili kufidia gharama na serikali ilikataa,kweli pia kwamba kulikuwa na shinikizo kutoka world bank kwamba mradi haukuwa na maslahi kwa muda huo kwakuwa mafuta yalikuwa rahisi.
Nakubaliana nawe kuwa tukiangalia sasa kweli haukuwa uamuzi mzuri kuwakatalia Agip kugharamia ukarabati na kuongezewa umiliki lakini world bank walionyesha muda huo kuwa mafuta yatakayosafishwa tiper yatakuwa ghali zaidi ya yale yanayokuja tayari kama petrol,diesel etc.
Pia elewa world bank muda huo ilikuwa na kauli ya mwisho kwenye mambo mengi ya nchi zinazoendelea zaidi ya sasa ambapo nguvu yao imepunguzwa.
 
Pia tuache kuwasikiliza hawa waliokuwa wanaongoza mashirika haya muda huo hawakuwa wazalendo PERIOD.Wengi walishiriki kuhujumu mashirika haya na sasa wanakaa na sisi kwenye mabaa na kulaumu na kiukweli wangestahili kuwa jela.
 
Nakuambia watanzania sasa tupate fundisho! Kwa kweli katika kuchagua marais inabidi tuwe makini sana, tusiangalie tu sura nzuri maana kama taabu tunayoipata sasa hivi ni fundisho tosha kabisa. Sera za chama kilichopo madarakani tayari ni failure tunaweza kuona hilo maana katika zaidi ya miaka 40 madarakani hakuna jambo la muhimu walilolifanya. Sasa tukiendelea na utaratibu huo ninauhakika tusitegemee mabadiliko yoyote dhidi ya haya tunayoyaona. Tubadilike sasa acheni mawazo mgando.
 
Ndugu tuko kwenye uwaanda huu wa uchumi na biashara, na mimi to be honest you have a point.
Ni kweli Mzee Ruksa alirithi a skeletal economic situation toka kwa Mwalimu.

Je aliboresha nini? zaidi ya kuuza na kuvunja misingi aliyaoacha Mwalimu?

Kwa Mwalimu ilikuwa Mtanzania kwanza, mtu mwingine baadaye, iwe kiuchumi kiutamaduni au vinginevyo.

Kimsingi Mwalimu alipatia sana ile siasa ya kudhibiti njia kuu za uchumi-hili halina mjadala maana ni strategic.

Kwamba Mzee Ruksa aliachia njia hizo zichukuliwe , tena whole sale na kwa kuzivunjilia mbali ni dhambi tuanayolilipia hadi leo.

Swadakta ndugu hilo halina ubishi kabisa

........ kuwa nchi ya Zambia hakufanya upuuzi wa kuua kinu chao cha mafuta toka miaka hiyo, kimeboreshwa na wanaendelea kudhibiti nishati ya mafuta hadi leo, wakati sisi tulitupa jongoo na mti wake.

Na ile LPG enzi hizo waliokuwa wakiichoma sasa wana soko la kuwauzia Wakenya....hebu angalia kwa wenzetu bomba linapita kwetu na leo Wakenya wanapita kwetu kwenda kununua hiyo LPG halafu leo tunalia na kuwalaumu Waarabu na Wahindi kwa biashara ya mafuta wakati ambapo sisi ndio tumewatengenezea njia ya kutukamua....
 
Serikali ya awamu ya pili ilifanya kitu ambacho mpaka kesho naona ni cha kijinga sana.
Sijui kama ilikuwa ni shinikizo la wafanya biashara au ushauri wa World Bank, sijui.
Wenzetu kama Zambia walitupilia mbali ushauri huo ambao ulitolewa kwa shinikizo la kuwafaishisha makampuni makubwa ya mafuta.
Baada ya Uhuru serikali ya awamu ya kwanza iliamua kisahihi kabisa kujenga kinu cha kuchuja mafuta-crude oil.
Kinu hicho-TIPER Refinery ya pale Kigamboni ilifanya kazi nzuri tu na kwa muda mrefu sana.
Zambia wakaenda mbali zaidi wao wakajenga bomba la mafuta ya crude oil toka Dar es salaam hadi kwao-bomba hili hadi leo linafanya kazi.
Mantiki ya refinery ya Kigamboni haihitaji akili kubwa sana kuielewa.
Importation ya rude oil inafanyika ONCE(mara moja) na hivyo freight charges zinalipwa once.
Baada ya kurefine hiyo crude oil unapata petrol za aina zote, Mafuta ya taa(kerosine),Mfuta ya Kulainisha(lubricating oil),diesel,IDO(Industrial Diesel Oil), na hata lami za aina tofauti kuanzia Bitumen 50/60, 60/70,80/100 na hata Gesi(Liquefied Petroleum Gas-LPG).
Kwa wale ambao hawakumbuki au hawakuwepo miaka hiyo, hizi products tulizipata hapa hapa nchini.
Leo ukitaka kuagiza product yoyote kati ya hizo unalipia freight(usafirishaji) kwa each individual product.
Si jambo la kushangaza kuwa leo bei za mafuta nchi ni karibu sawa na bei za Burundi, Rwanda hata Zambia pamoja na kuwa wao wanapitisha products zote hapa hapa nchini.
Ki ukweli bei zetu za mafuta na products zake zilitakiwa kuwa chini kama tusingekisambaratisha kiwanda cha TIPER pale Kigamboni.
Uuzwaji wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha TIPER zilikuwa njama za awali kabisa katika serikali ya awamu ya pili iliyofanywa na wafanyabiashara waliokuwa maswahiba wakubwa sana na Rais wa awamu ya pili Mzee Mwinyi aliyekuwa akifahamika pia kama Bwana Ruksa. Hayati Baba wa Taifa alionekana wazi kukerwa na hali ilivyokuwa kiasi cha kukosoa hadharani maamuzi kadhaa ya serikali ile na mara kadhaa alikemea au kuyaponda maamuzi yaliyofanywa. Kwa mfano alisikika akionya hadharani kwamba ikulu si pango la walanguzi na wezi, na mara kadhaa alilalamikia maamuzi yaliyokuwa yakifanywa na chama alichokiasisi cha CCM kwamba waliacha misingi ya maana iliyoachwa na utawala wa awamu yake na kuzingatia makosa ya ovyo ovyo yaliyofanywa na awamu yake.
Kimsingi Nyerere aliona mbali. Aliujua umuhimu wa Tanzania kuwa na kiwanda chake cha kusafisha mafuta, na kwa hakika uzalishaji katika kiwanda hiki ulisaidia sana katika kudhibiti bei ya bidhaa za mafuta na kulingizia taifa kipato kikubwa. Alijua kwamba siku Tanzania itakapoanza uchimbaji wa mafuta ingefaidika na uwepo wa kiwanda hicho kwa vile haingekuwa lazima kuyasafirisha nje ili yakasafishwe, yarudishwe na tuuziwe tena kwa bei ya ulanguzi!
Madhara ya uuzwaji wa kiwanda kile yanasikika zaidi sasa na yatakuwa machungu zaidi pale tutakapoanza uchimbaji wa mafuta yetu kwani uchimbwaji huo kamwe hautatusaidia lolote katika kupunguza bei ya mafuta kwa watumiaji kwani bidhaa hiyo itaendelea kununuliwa na kwa bei ya kilanguzi toka nje mafuta yatakakokuwa yakisafishwa. Hali yetu haitakuwa tofauti na Nigeria ambako licha ya kuwa taifa linalozalisha mafuta mengi ulimwenguni bei yao ya mafuta yaliyosafishwa ni kubwa pengine kuzidi hata hii yetu kwani nao inawabidi kununua toka nje mafuta yaliyosafishwa. Ile ilikuwa hujuma ya muda mrefu iliyopangwa na mafisadi waliowatumia viongozi wetu waliokuwa na upeo mdogo wa kufikiri kwa kubembelezwa na rushwa ndogondogo.
Hujuma ile ndiyo mama wa matatizo ya upandaji wa bei wa ovyo ovyo wa mazao ya mafuta nchini, hujuma itakayoendelea kulisakama taifa letu kwa miango na hata karne kadhaa zijazo. Ni CCM ndiyo waliotufikisha hapa kwa kuziponda sera za kijamaa za awamu ya kwanza na kuingiza seera za kibepari zilizotuzalishia mafisadi papa waliosheheni ndani ya chama hilo bovu, chakavu, lenye uvundo wa rushwa, wizi, na ubakaji wa uchumi uliokithiri uliokifanya chama hicho kupoteza kabisa mwelekeo na mvuto mbele ya watanzania wanaozidi kuwa waelewa wa madhambi na uchafu ndani ya chama hiki kila kukicha. Suluhu ya matatizo haya ni kuing'oa CCM na mizizi yake yote na kuanza upya na chama ambacho hakitakuwa na fungamano na mikataba ya kijinga, mibovu, kiwendawazimu na kihayawani kama hii ya sasa iliyojikita katikati ya chama bovu hili linalotapatapa kujinusuru na uovu wake, chama lililosheheni watu waliovimbiwa ufisadi mithili ya panya waliokula chakula kilichowekwa sumu ya kuwamaliza. Haya shime watanzania tuing'oe CCM na kurudisha heshima ya taifa letu iliyouzwa kwa bei poa na CCM.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
Jamani basi tumalize hii ibada!
kama TIPER ilikuwa na faida kubwa kwa wnanchi , basi tuishikize serikali ifufue TIPER ili tuondokane na kuwa faidisha hawa walionufaika na kufa kwa TIPPER. CCM na VYama vya Upinzani ni lazima viweke kufufua TIPER katika Ajenda zao za uchaguzi la sivyo hatuwapi kura.

Nakumbuka mfanya biashara mmoja mwanzilishi wa Disco toto hapa Tanznaia miaka ya nyuma , aliwahi kupewa tenda ya kuleta mafuta nchini wakati TIPER na TPDC ziko na nguvu imara. Unajua hata wakati wa nyerere ikulu haikuhitaji ukuta. Ila wafanya biashar awakamrubuni mwinyi aweke ukuta natenda hiyo ghalama yake ilikuwa sio nzuri kuisimulia leo.

mawazili wakaanza kuingia mikataba kuuwa mashirika yaliokuwa yanategemea mali ghafi za nchi na ambayo yalikuwa yanaleta faida ya soko la ajira.

Wewe ona tuu mfano TAFICO. Tafico ilikuwa inatoa ajira nzuri kwa kuvua samaki wa kila aina katika bahari ya hindi. Lakini kwa nini mfanya biashara wa nje alipewa leseni ya kuvua samaki wetu wakati TAFICO ilikuwa ipo na inafanya vema? Sasa leo wafanya biashara hao hao wanaimport samaki wenye mionzi toka japan, je tungekuwa na TAFICO samaki hao wangekuja kweli hapa nchini?

Mashilika yote ya ujasusi ya assia na uarabuni yalikuwa na hongo za keleta bidhaa zao na kuhakikisha zile za viwanda vyetu vitengenezavyo bidhaa hizo vinakufa. Kwa nini national battery(matshushita) ilikufa? wakati National battery kilikuwa ni moja ya kiwanda kitoacho redio bora na kutoa ajira nyingi kwa watu,. Mjanja mmoa akaenda asia na kuingia mkataba wa nchi hizo kuleta raadio hapa nchini . Matokeo yake, National batery ikafa na wafanyakazi wote wake kutawanyika bila kazi.

Tunayo mengi ya kulia , ila machozi sasa hayatoki!
 
Uuzwaji wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha TIPER zilikuwa njama za awali kabisa katika serikali ya awamu ya pili iliyofanywa na wafanyabiashara waliokuwa maswahiba wakubwa sana na Rais wa awamu ya pili Mzee Mwinyi aliyekuwa akifahamika pia kama Bwana Ruksa. Hayati Baba wa Taifa alionekana wazi kukerwa na hali ilivyokuwa kiasi cha kukosoa hadharani maamuzi kadhaa ya serikali ile na mara kadhaa alikemea au kuyaponda maamuzi yaliyofanywa. Kwa mfano alisikika akionya hadharani kwamba ikulu si pango la walanguzi na wezi, na mara kadhaa alilalamikia maamuzi yaliyokuwa yakifanywa na chama alichokiasisi cha CCM kwamba waliacha misingi ya maana iliyoachwa na utawala wa awamu yake na kuzingatia makosa ya ovyo ovyo yaliyofanywa na awamu yake.
Kimsingi Nyerere aliona mbali. Aliujua umuhimu wa Tanzania kuwa na kiwanda chake cha kusafisha mafuta, na kwa hakika uzalishaji katika kiwanda hiki ulisaidia sana katika kudhibiti bei ya bidhaa za mafuta na kulingizia taifa kipato kikubwa. Alijua kwamba siku Tanzania itakapoanza uchimbaji wa mafuta ingefaidika na uwepo wa kiwanda hicho kwa vile haingekuwa lazima kuyasafirisha nje ili yakasafishwe, yarudishwe na tuuziwe tena kwa bei ya ulanguzi!
Madhara ya uuzwaji wa kiwanda kile yanasikika zaidi sasa na yatakuwa machungu zaidi pale tutakapoanza uchimbaji wa mafuta yetu kwani uchimbwaji huo kamwe hautatusaidia lolote katika kupunguza bei ya mafuta kwa watumiaji kwani bidhaa hiyo itaendelea kununuliwa na kwa bei ya kilanguzi toka nje mafuta yatakakokuwa yakisafishwa. Hali yetu haitakuwa tofauti na Nigeria ambako licha ya kuwa taifa linalozalisha mafuta mengi ulimwenguni bei yao ya mafuta yaliyosafishwa ni kubwa pengine kuzidi hata hii yetu kwani nao inawabidi kununua toka nje mafuta yaliyosafishwa. Ile ilikuwa hujuma ya muda mrefu iliyopangwa na mafisadi waliowatumia viongozi wetu waliokuwa na upeo mdogo wa kufikiri kwa kubembelezwa na rushwa ndogondogo.
Hujuma ile ndiyo mama wa matatizo ya upandaji wa bei wa ovyo ovyo wa mazao ya mafuta nchini, hujuma itakayoendelea kulisakama taifa letu kwa miango na hata karne kadhaa zijazo. Ni CCM ndiyo waliotufikisha hapa kwa kuziponda sera za kijamaa za awamu ya kwanza na kuingiza seera za kibepari zilizotuzalishia mafisadi papa waliosheheni ndani ya chama hilo bovu, chakavu, lenye uvundo wa rushwa, wizi, na ubakaji wa uchumi uliokithiri uliokifanya chama hicho kupoteza kabisa mwelekeo na mvuto mbele ya watanzania wanaozidi kuwa waelewa wa madhambi na uchafu ndani ya chama hiki kila kukicha. Suluhu ya matatizo haya ni kuing'oa CCM na mizizi yake yote na kuanza upya na chama ambacho hakitakuwa na fungamano na mikataba ya kijinga, mibovu, kiwendawazimu na kihayawani kama hii ya sasa iliyojikita katikati ya chama bovu hili linalotapatapa kujinusuru na uovu wake, chama lililosheheni watu waliovimbiwa ufisadi mithili ya panya waliokula chakula kilichowekwa sumu ya kuwamaliza. Haya shime watanzania tuing'oe CCM na kurudisha heshima ya taifa letu iliyouzwa kwa bei poa na CCM.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

Lazima tukubaliane kuwa shina la matatizo ya leo katika nishati msingi wake ni maamuzi kama ya kuua kiwanda cha kuchuja mafuta ghafi-crude oil, cha TIPER Kigamboni.
Hakuna lugha rahisi zaidi ya kuelezea kuwa hii ilikuwa hujuma.
Matokeo ya maamuzi mabaya zaidi ya miaka 20 iliyopita leo ndio tunaanza kuona matokeo yake.
Si kwamba hatuna wasomi, la hasha , si kwamba hatuna watu wenye uchungu na nchi hii la hasha.
Kinachoonekana sasa ni ulafi uliopindukia wa baadhi ya viongozi hadi kupelekea kuona scenario ya yale yajayo.
Viongozi wa lioua TIPER hawakuwa na uwezo wa kuforecast hata miaka 20 mbele, hata kile walichopewa hakijawasaidia katika aibu hii Taifa inalolikumba.

Ndugu zangu uzalendo kwanza na TIPER irudi ili tudhibiti muelekeo wa nishati-mafuta.
 
kipindi cha awamu ya pili kinalaumiwa kwa mambo mengi lakini je mambo yote yalitokea ndani ya miaka michache tuu? je haiwezekani kuwa walirithi matatizo? je, nyerere alistaafu kwa kuwa alichoka kutawala ?alikataa kugeuka jiwe? au kwa kuwa alishasoma alama za nyakati kuwa hali ya nchi haikuwa tena nzuri kwake?
vipi kuanzishwa kwa uchangiaji wa gharama za matibabu na huduma za afya kuanzia 1993, jee, ilitokana na ubovu wa sera za awamu ya pili au baada ya serikali kushindwa kumudu gharama kubwa za uendeshaji wa sekta ya afya? je mnaamini huo pia ulikuwa ni uamuzi mbovu wa serikali ya awamu ya pili
hivi nyerere angeendelea kutawala mpaka 1990, mapinduzi yasingetokea nchi hii?maana hata yeye kipindi chake cha mwisho alifail vibaya
Mkuu tunapochagua serikali kwa uchaguzi mkuu hatuchagui ili itoe visingizio na kusingizia serikali zilizopita.
Tunazichagua ili ZITATUE matatizo yaliyopo nchini.
Hili la kusingizia serikali za nyuma ni kushindwa kazi na hatimaye kukatisha tamaa wale walio wachagua kuwaongoza.
Katika hili la TIPER serikali ya sasa iunde tume ya kurejesha mtambo wa refinery ili tuondokane na adha hii ya kujitakia.
Tunaamini hata Rais wa sasa si mtu mgeni sana na tatizo hili maana alikuwapo wizara ile ya Nishati wakati wa kufanya maamuzi ya kuua TIPER, matokeo yake anayapata live sasa akiwa Rais.
Aliyelitega bomu hili ndiye anajua namna ya kulitegua.
 
Wakuu kama hatua ya mwanzo kurudishwe utaratibu wa mafuta kuja kwa mkupuo(bulk) na hawa ma-depots wawe wholesalers tu na vituo kuwa retailers.Depots zote ziwe zinanunua mafuta kutoka kwa muagizaji mmoja ambaye watashindanishwa kwa open tender na mwenye bei ndogo analeta mwaka huo.Sasa hivi biashara imekuwa syndicate importer/depot/retailer inafanywa na mtu mmoja kwa mfano Engen analeta mafuta,anayahifadhi, ana vituo vya rejareja.
Hili la kujenga refinery mpya liwe midterm goal hamna kiwanda cha kufufua pale kwa wanaobisha nendeni mkaangalie kwa macho yenu.
 
Nakubaliana kabisa na hili.
Biashara hii imekuwa kama cartel ya watu fulani ambao wanaing'iniza serkali kwa faida yao.
Nafikiri serikali imetambua makosa yake na nimesikia kuwa utaratibu wa kuagiza mafuta in bulk karibu unarudishwa.
TIPER ILIUWAWA na watu hawa hawa wakisaidiwa na wanasiasa, ni vizuri tukawa strategic katika sula hili ili tusikamatike tena na adha inayoendelea sasa na serikali kukosa meno ya kuchukua hatua.Ujenzi wa Kiwanda cha refinery ya crude oil hauepukiki kama tuna taka maslahi ya nchi yatiliwe maanani.
 
hili linaonyesha matokeo ya tatizo moja na miaka 10 ijayo huenda tukashuhudia mambo yasiyoweza kuelezeka!
 
Ndugu zangu wana jamii forum, naomba mnisaidie majibu, ni sababu zipi zilipelekea kiwanda chetu cha kusafisha mafuta ghafi (CRUDE OIL) cha TANZANIA ITALIAN PETROLEUM REFINERY CO. LTD. (TIPER) kufa.

Jana nilikua najiuliza maswali mengi, inakuwaje sisi tulishindwa kuendesha kiwanda hicho, na wakati wenzetu wa Zambia wameweza kukiendesha kiwanda chao cha kusafisha mafuta.

Kwa mimi nilikua nikiwaza moja ya viwanda vinavyo ingiza pesa nyingi duniani ni viwanda vya mafuta, maana nishati ya mafuta inahitajika sana duniani. Sasa basi kwanini serikali isikifufue kiwanda hicho??

Kama serikali ikifufua kiwanda cha cha kusafisha mafuta cha TIPER mimi naona itapata faida kubwa sana. Kwasababu Kiwanda kitazalisha mafuta ya petroli, diesel, mafuta ya ndege, mafuta ya taa, LPG, mafuta ya injini, grisi na rami, ambayo kwakweli yanahitajika sana sokoni.

Lakini pia kuna bidhaa zingine pia ambazo zingetoka hapo tungezitumia kwenye viwanda vya kutengeneza matairi, nguo, mbolea, plastiki, madawa ya binadamu, na kemikali za viwandani.

Kwa kweli serikali ingejitahidi sana ifufue kiwanda cha kusafisha mafuta, kitawezesha pia teknolojia yetu ikue kwa kasi sana.
 
Uuzwaji wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha TIPER zilikuwa njama za awali kabisa katika serikali ya awamu ya pili iliyofanywa na wafanyabiashara waliokuwa maswahiba wakubwa sana na Rais wa awamu ya pili Mzee Mwinyi aliyekuwa akifahamika pia kama Bwana Ruksa. Hayati Baba wa Taifa alionekana wazi kukerwa na hali ilivyokuwa kiasi cha kukosoa hadharani maamuzi kadhaa ya serikali ile na mara kadhaa alikemea au kuyaponda maamuzi yaliyofanywa. Kwa mfano alisikika akionya hadharani kwamba ikulu si pango la walanguzi na wezi, na mara kadhaa alilalamikia maamuzi yaliyokuwa yakifanywa na chama alichokiasisi cha CCM kwamba waliacha misingi ya maana iliyoachwa na utawala wa awamu yake na kuzingatia makosa ya ovyo ovyo yaliyofanywa na awamu yake.
Kimsingi Nyerere aliona mbali. Aliujua umuhimu wa Tanzania kuwa na kiwanda chake cha kusafisha mafuta, na kwa hakika uzalishaji katika kiwanda hiki ulisaidia sana katika kudhibiti bei ya bidhaa za mafuta na kulingizia taifa kipato kikubwa. Alijua kwamba siku Tanzania itakapoanza uchimbaji wa mafuta ingefaidika na uwepo wa kiwanda hicho kwa vile haingekuwa lazima kuyasafirisha nje ili yakasafishwe, yarudishwe na tuuziwe tena kwa bei ya ulanguzi!
Madhara ya uuzwaji wa kiwanda kile yanasikika zaidi sasa na yatakuwa machungu zaidi pale tutakapoanza uchimbaji wa mafuta yetu kwani uchimbwaji huo kamwe hautatusaidia lolote katika kupunguza bei ya mafuta kwa watumiaji kwani bidhaa hiyo itaendelea kununuliwa na kwa bei ya kilanguzi toka nje mafuta yatakakokuwa yakisafishwa. Hali yetu haitakuwa tofauti na Nigeria ambako licha ya kuwa taifa linalozalisha mafuta mengi ulimwenguni bei yao ya mafuta yaliyosafishwa ni kubwa pengine kuzidi hata hii yetu kwani nao inawabidi kununua toka nje mafuta yaliyosafishwa. Ile ilikuwa hujuma ya muda mrefu iliyopangwa na mafisadi waliowatumia viongozi wetu waliokuwa na upeo mdogo wa kufikiri kwa kubembelezwa na rushwa ndogondogo.
Hujuma ile ndiyo mama wa matatizo ya upandaji wa bei wa ovyo ovyo wa mazao ya mafuta nchini, hujuma itakayoendelea kulisakama taifa letu kwa miango na hata karne kadhaa zijazo. Ni CCM ndiyo waliotufikisha hapa kwa kuziponda sera za kijamaa za awamu ya kwanza na kuingiza seera za kibepari zilizotuzalishia mafisadi papa waliosheheni ndani ya chama hilo bovu, chakavu, lenye uvundo wa rushwa, wizi, na ubakaji wa uchumi uliokithiri uliokifanya chama hicho kupoteza kabisa mwelekeo na mvuto mbele ya watanzania wanaozidi kuwa waelewa wa madhambi na uchafu ndani ya chama hiki kila kukicha. Suluhu ya matatizo haya ni kuing'oa CCM na mizizi yake yote na kuanza upya na chama ambacho hakitakuwa na fungamano na mikataba ya kijinga, mibovu, kiwendawazimu na kihayawani kama hii ya sasa iliyojikita katikati ya chama bovu hili linalotapatapa kujinusuru na uovu wake, chama lililosheheni watu waliovimbiwa ufisadi mithili ya panya waliokula chakula kilichowekwa sumu ya kuwamaliza. Haya shime watanzania tuing'oe CCM na kurudisha heshima ya taifa letu iliyouzwa kwa bei poa na CCM.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
Uganda itasafirisha crude oil kupitia Tanga, kama hatuwezi kureabilitate Tiper Kigamboni basi tujenge refinnery mpya Tanga.
Tutanunua crude ya Ug kwa mkataba mzuri tujikwamue kupata mafuta ya bei nafuu na kuuza ziada nje.
 
Mkuu miaka hiyo nilikuwa nafanya kazi katika kampuni ya mafuta HAMNA REHABILITATION iliyofanyika,kulikuwa na mpango huo na kweli vifaa vingi vililetwa lakini Grupo ENI kampuni mama ya Agip walikuwa wanataka kwa kugharamia ukarabati na serikali kutokuwa na hela za kuchangia basi waongezewe shares ili kufidia gharama na serikali ilikataa,kweli pia kwamba kulikuwa na shinikizo kutoka world bank kwamba mradi haukuwa na maslahi kwa muda huo kwakuwa mafuta yalikuwa rahisi.
Nakubaliana nawe kuwa tukiangalia sasa kweli haukuwa uamuzi mzuri kuwakatalia Agip kugharamia ukarabati na kuongezewa umiliki lakini world bank walionyesha muda huo kuwa mafuta yatakayosafishwa tiper yatakuwa ghali zaidi ya yale yanayokuja tayari kama petrol,diesel etc.
Pia elewa world bank muda huo ilikuwa na kauli ya mwisho kwenye mambo mengi ya nchi zinazoendelea zaidi ya sasa ambapo nguvu yao imepunguzwa.

Enzi hizo pia World Bank ilijaa wapiga dili! Ni ajabu sana kwa nchi zetu zinazoendelea hasa kipindi hicho tuliamini kabisa kwamba hao World Bank ni kama Malaika na wanachoshauri kiko sahihi kabisa. Kumbe wale maofisa, hasa country desk officers wengine wanapiga dili na makampuni makubwa halafu wanakuja kushauri kwa manufaa ya hayo makampuni! Nakwambia hizi nchi zetu hizi zimechezewa kwelikweli!
 
Sijasikia popote hata kwa mipango tu , ya kufufua ile Refinery ya Kigamboni ili kuondokana na adha hii ya gharama kubwa ya nishati-mafuta.
Kati ya vitu ambavyo Mzee Ruksa atalaaniwa na vizazi vijavyo ni kukubali ushauri usio na tija kwa nchi.
Mzee wa viwanda achukue hili la kufufua refinnery ya Tiper.
Tutapata rami bitumen kwa urahisi na crude ya Ug itakuta tuko tayari kwa kazi!!
 
yawezekana ikawa kweli tiper ilikufa wakati wa mwinyi, lakini yawezekana ilikuwa tayari imeshajichokea soo mwinyi akadondokewa na jumba bovu tu, kwani viwanda vingi vilivyokuwa vya umma vikabinafsishwa baadae je havikuyumba enzi ya mwalimu??? mbona pia utawala wa mwalimu unalaumiwa kwa kulea wezi wachache au wale waliokuwa wakiharibu hapa na kusogezwa kule kwa kisingizio kuwa hakuna wataalamu wengine? hili laweza kuwa sawa na mgonjwa aliyecheleweshwa kuletwa kituoni kisha akaja kufia mikononi mwa daktari na kuishia kumlaumu dr kwamba kasababisha kifo cha mgonjwa ilhali mgonjwa mwenyewe alikuwa dhoofu,
binafsi, naamini mashirika mengi ya umma yaliyumba kipindi cha mwisho cha utawala wa nyerere kutokana na sababu mbalimbali za ndani na za nje, na mind you, mashirika mengi yalitegemea ruzuku ya serikali lakini nyie nyote mwajua serikali haikuwa na pesa sxasa mashirika hayo yangejiendeshaje???
naomba nifundishwe na nielekezwe kwani nimepata kusikia kuwa kipindi mwinyi anaingia nchini(nikimquote warioba alipohojiwa itv kwenye dakika 45 ) kwamba wao walipokea nchi ikiwa haina hela kabisa na mfumuko wa bei ulikuwa 36%, lakini mpaka mwaka 1990 mfumuko ulipungua kufikia 18%, na yeye akajinasibu kuwa hayo kwao yalikuwa mafanikio makubwa katika serikali ya kipindi chake, sasa kwa kuwa mashirika mengi ya uma yalitegemea ruzuku yangeendeleaje???
unless tuelezwe vinginevyo kwamba mpaka 1985 , TIPER ilikuwa ikiendeshwa kwa ufanisi ila kuanzia 1986-its death ndo ilianza kuyumba nitaamini ni sababu ya mwinyi, vinginevyo mimi nitaamini nyerere na utawala wake walichangia kumchelewesha mgonjwa ila akaja fia mikononi mwa daktari, lawama iwe pande zote to be fair
Mashirika mengi yalikufa au kubinafishwa kipindi cha pili.
Hakukuwa na good strategy za kufufua uchumi.
Matokeo yake viwanda na mashirika yakauzwa na kufa!!
Economical reform ilikuwa zero!!
 
Back
Top Bottom