Nishati na Madini wanarejea Bungeni Jumamosi hii: Tutegemee muujiza Gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nishati na Madini wanarejea Bungeni Jumamosi hii: Tutegemee muujiza Gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, Aug 11, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Nishati na Madini siku 21 zimekwisha

  Huku Jairo akisukumiwa Tuhuma nyingine jana kama njia na kamtego hivi kupoteza lengo na kuwasahaulisha Watanzania uozo katika Bajeti ya Awali ya Wizara hiyo iliyogonga mwamba mwezi uliopita, siku zao 21 zimekwisha na Jumamosi wanarejea tena Bungeni kuwasilisha Bajeti yao itakayosomwa kwa siku moja na kisha kuputishwa ama kutopitishwa.

  My Take:
  • Unafiki wa wabunge na makundi utaona yanavyofanya kazi Jumamosi.
  • Sina shaka semina zimeshapigwa vya kutosha kama ilivyookolewa Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi
  • Mie binafsi sitegemei muujiza wowote kesho wala jipya zaidi ya Bajeti kupita katikati ya Giza
  • Ahadi zitajaa zenye ladha saafi kama asali na wingi wa hoja za kinafiki kama mkia wa kondoo
  Yetu macho na masikio, sijui mnalitazamaje hili hapo Jumamosi

  ADIOS
   
 2. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Generator zinadaiwa kuwa zinaweza kusababisha ongezeko la Hewa ya Ukaa kutokana na kuwashwa kwa Wingi bila mpangilio, Thanks to maamuzi mazito ya Serikali kuwabana wamiliki wa mabohari ya Mafuta baada ya shinikizo zito la CDM
   
 3. s

  smz JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo bunge litafanya kazi Jumamosi??
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Naona katika hii bajeti haitakua na jipya zaidi zaidi hongo ndo itatumika zaidi ili ipite kwa upigajikura wao wakiwenda wazimu wa ndio au hapana makinda hakukosea kulifananisha bunge na kariakoo
   
 5. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Itakuwa muujiza kama watakuja na muujiza lakini knowing them business as usual will prevail
   
 6. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mie naungana na Mwanakijiji kutoa rai kuwa bila ya Wizara ya Nishati kutenga pesa za Stieglers gorge project hiyo bajeti isipitishwe!!!!! Tumechoka na umeme wa hadithi za megawati hatutaki tunataka a fixed solution na wapunguze matumizi ya serikali kulipia mradi huo.
   
 7. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Bunge tangu lini likafanya kazi Jumamosi? Mbona kama vile inataka kupitishwa kwa nguvu hii bajeti? Maana hakutakuwa na muda wa kutosha kuijadili. Na pia, siku hiyo kuna mechi ya Simba na Yanga na Ligi Kuu ya England inaanza...Si unawajua Watanzania ilivyo rahisi ku-divert attention yao?

  Tusubiri tuone! Ila hakutakuwa na jipya. Zitapigwa blah blah kisha wabunge wa magamba watagonga meza na bajeti itapita!
   
 8. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ligi Kuu ya England ndo chambo hapo, Simba na Yanga wanakipiga Jumatano ijayo Tarehe 17 August 2011.

  Kiukweli Jumamosi ni siku ambayo wabunge wengi huipenda kwenda Mnadani kula nyama na mvinyo, bila shaka hapa ni game la kuwafanya wajadili kwa kukosa umakini wakiwazia weekend, ila kama nilivyotahadharisha hapo juu tutayaona na kuyasikia mengi hapo kesho
   
 9. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Tatizo Mwanakijiji washamwona kama Adui hata awashauri jema lipi ni kama hawaoni licha ya Mdau huyu mwenye ufahamu mkubwa kuchukua muda mwingi kuchambua vitu vizito vyenye masilahi ya Umma.
   
 10. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  VOR mgao umepanda makali kama umegundua katika siku hizi mbili kuelekea Jumamosi
   
 11. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ni kanuni inatenguliwa tu kuruhusu muda huo kutumika kwa shughuli za kawaida za Bunge
   
 12. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mh. William Lukuvi katoa ufafanuzi tayari kanuni ya 28 kifungu kidogo cha 25 kwa kuwa Bunge haliwezi kukutana siku za Jumamosi Jumapili na siku za Sikukuu, kaomba Bunge kutengua Kanuni hiyo ili kuruhusu Hoja hiyo kujadiliwa siku ya Jumamosi kwa kuwaruhusu Wizara ya Nishati na Madini kuweza kutoa marekebisho yao katika kipengele cha MATUMIZI YA WIZARA na ni KIPENGELE cha UMEME tu.

  Mnyika anaomba muongozo kuhusu kutengua kanuni muda kuongezwa na kutoa nafasi ya kujadiliwa vema kwa Hoja hiyo ambayo inadaiwa kuwa haitarejewa Hotuba yote ila kipengele nilichokitaja hapo juu na hapatakuwa na maswali.

  Spika anasema muda utatosha kwa kuwa hatasoma tena Hotuba yote kama hofu ya Mnyika ilivyojitokeza
   
 13. Terrire

  Terrire Member

  #13
  Aug 12, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio hewa chafu peke yake pia ni "NOISE POLLUTION"
   
 14. Terrire

  Terrire Member

  #14
  Aug 12, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Masaki umeongea Point kamanda wangu.................. That's TZ
   
 15. Terrire

  Terrire Member

  #15
  Aug 12, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wangetaka ipite kiurahisi wangepanga tarehe ya jana Majembe ya CHADEMA yakiwa Arusha
   
 16. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Bajeti imepita, na marekebisho yanatia matumaini. Mlikuwa wapi sasa kuja na mikakati kama Hii

  Hongera Wizara na Wataalam mliofanya marekebisho haya
   
Loading...