Nishati: Makosa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Pili - Kifo cha Kiwanda cha kusafisha mafuta TIPPER

Sababu za kuanzishwa Tipper zilikuwa za kisiasa zaidi,kuliko kiuchumi.
Kibaya zaidi ubia wake na Agip ya Italy uligubikwa na ufisadi mkubwa mno na serikali kubebeshwa mzigo mkubwa sana.
Kama haitoshi mchango wa Tipper kiuchumi ulikuwa mdogo kwani refinery ilikuwa ndogo sana na yenye mitambo ya zamani chakavu.Asili mia kubwa ya mafuta yaliagizwa yakiwa yameishasafishwa kwani Tipper ilikuwa haina uwezo wa kusafisha mafuta ghafi
 
Sasa Kwa kubinafsisha, technology imebadilika?? Na mitambo mipya imewekwa?? Na kiwanda kimeongezwa ukubwa??? Au ndio huo Mzigo uliobebeshwa serikali kupitia huo mkatana Na agip ndio sasa tunabebeshwa kwenye hizo cost zingine Na kukosesha watu wetu kazi
 
Uzalendo wa usimamiaji rasilimali za nchi viwanda miundombinu ulikua dhaifu
Pia washsuri wa uchumi zama hizo walikua ziro
 
Sasa Kwa kubinafsisha, technology imebadilika?? Na mitambo mipya imewekwa?? Na kiwanda kimeongezwa ukubwa??? Au ndio huo Mzigo uliobebeshwa serikali kupitia huo mkatana Na agip ndio sasa tunabebeshwa kwenye hizo cost zingine Na kukosesha watu wetu kazi
Ilikuwa ni hasara tokea mwanzo,Tipper ilifunga uzalishaji wa mafuta miaka 17 iliopita,kwa sasa inatumika kama storage tu.
 
Sasa Kwa kubinafsisha, technology imebadilika?? Na mitambo mipya imewekwa?? Na kiwanda kimeongezwa ukubwa??? Au ndio huo Mzigo uliobebeshwa serikali kupitia huo mkatana Na agip ndio sasa tunabebeshwa kwenye hizo cost zingine Na kukosesha watu wetu kazi
Tipper haikubinafsishwa, Tipper ilikufa yenyewe kifo cha mende sababu mabadiliko ya uzalishaji nafuta kidunia, ambapo mafuta yaliyosafishwa yalizalishwa kwa wingi toka kwa wauzaji. Kuna msemo "If you can easly get milk why you raise a Cow?" Bomba LA Zambia halisafirishi mafuta ghafi, linasafirisha mafuta yaliyosafishwa hesabu za kiuchumi zililazimisha kama nchi kuagiza mafuta yaliyosafishwa kuliko kuagiza mafuta ghafi kisha kusafisha wenyewe.
 
Tipper haikubinafsishwa, Tipper ilikufa yenyewe kifo cha mende sababu mabadiliko ya uzalishaji nafuta kidunia, ambapo mafuta yaliyosafishwa yalizalishwa kwa wingi toka kwa wauzaji. Kuna msemo "If you can easly get milk why you raise a Cow?" Bomba LA Zambia halisafirishi mafuta ghafi, linasafirisha mafuta yaliyosafishwa hesabu za kiuchumi zililazimisha kama nchi kuagiza mafuta kuliko kusafisha wenyewe.
Mbona Kenya waliendelea kuwa nacho ???
 
Hatari sana.
 
Serikali ya awamu ya pili ilifanya kitu ambacho mpaka kesho naona ni cha kijinga sana.

Sijui kama ilikuwa ni shinikizo la wafanya biashara au ushauri wa World Bank, sijui.

Wenzetu kama Zambia walitupilia mbali ushauri huo ambao ulitolewa kwa shinikizo la kuwafaishisha makampuni makubwa ya mafuta.

Baada ya Uhuru serikali ya awamu ya kwanza iliamua kisahihi kabisa kujenga kinu cha kuchuja mafuta-crude oil.

Kinu hicho-TIPER Refinery ya pale Kigamboni ilifanya kazi nzuri tu na kwa muda mrefu sana.
Zambia wakaenda mbali zaidi wao wakajenga bomba la mafuta ya crude oil toka Dar es salaam hadi kwao-bomba hili hadi leo linafanya kazi.

Mantiki ya refinery ya Kigamboni haihitaji akili kubwa sana kuielewa.

Importation ya crude oil inafanyika ONCE(mara moja) na hivyo freight charges zinalipwa once.

Baada ya kurefine hiyo crude oil unapata petrol za aina zote, Mafuta ya taa(kerosine),Mfuta ya Kulainisha(lubricating oil),diesel,IDO(Industrial Diesel Oil), na hata lami za aina tofauti kuanzia Bitumen 50/60, 60/70,80/100 na hata Gesi(Liquefied Petroleum Gas-LPG).

Kwa wale ambao hawakumbuki au hawakuwepo miaka hiyo, hizi products tulizipata hapa hapa nchini.
Leo ukitaka kuagiza product yoyote kati ya hizo unalipia freight(usafirishaji) kwa each individual product.

Si jambo la kushangaza kuwa leo bei za mafuta nchi ni karibu sawa na bei za Burundi, Rwanda hata Zambia pamoja na kuwa wao wanapitisha products zote hapa hapa nchini.

Ki ukweli bei zetu za mafuta na products zake zilitakiwa kuwa chini kama tusingekisambaratisha kiwanda cha TIPER pale Kigamboni.
Ukifuatilia kwa makini utagundua kwamba TIPER kwa sasa hivi ina manufaa kuliko pale mwanzo. miaka ile TIPER ilikuwa ina uwezo wa kuzalisha asilimia 30tu ya mahitaji maana ilikuwa na uwezo wa kurefine tani laki 6(ambazo ni takribani lita milioni mia sita) tu mwaka na badae ziliongezeka mpaka kufikia tani 750,000 kwa ajili ya zambia na pia tujue kwamba haikuwa mali yetu 100% sisi tulikuwa na 50%. ukilinganisha na leo TIPER kama ghala inaweza kuhifadhi lita milioni 254 kwa wakati mmoja piga hesabu kama mafuta hayo ni ya mwezi mmoja kwa mwaka ni lita ngapi!?!?. na kwa sababu ilikuwa mali ya ubia, mbia mwingine aliuza asset na share zake akaja mwingine , naona hapo bado huwezi kujua mbia wako ataamua nini kesho. Sikatai kwamba Bretten woods walikuwa na mkono wao kuiscrap TIPER OG lakini kwa leo tukicheza karata zetu vizuri tukaiown TIPER 100% itakuwa na manufaa makubwa zaidi. NOOYA!!
 
Wadau naomba kuchangia katika mada hii kidogo.

(1) Umuhimu wa nchi kama Tanzania ambayo ina bandari (nyingi na nzuri) na ambayo pia inazungukwa na land-locked countries kuwa kiwanda cha kuchakata 'crude oil' ni mkubwa sana, na kuna faida nyingi sana, jana, leo na kesho.
(2) Awamu ya kwanza ya (Rest in peace, Baba wa Taifa) iliona umuhimu huu, ndio sababu TIPER ilijengwa.
(3) Matatizo ya TIPER yalianza pale ambapo, kwa kujua au kutokujua, SOURCE ya CRUDE ambayo kiwanda kilikuwa designed kuchakata ilibadilishwa, bila kuzingatia kwamba MTAMBO ulikuwa DESIGNED kwa specific CRUDE.
(4) Matokeo yake ni kwamba PRODUCTS ambazo zilikuwa zinatakiwa kwa wingi (DIESEL na PETROLI) zilikuwa kidogo, na mafuta mazito (HEAVY FUEL OIL) pamoja na LAMI zilikuwa nyingi. Kumbuka kwamba hizi HEAVY products ni za thamani ndogo wakati hizo lighter products (PETROLI na ndugu zake) ni za thamani kubwa - kwahiyo kiwanda kikawa kinaendeshwa kwa HASARA.
(5) USHAURI wa kitaalam uliotolewa kwa serikali (WORLD BANK Report, 1984) ni kutumia kiasi cha DOLA Mil. 10 hivi kurekebisha mitambo (REFINERY MODIFICATIONS); kinyume cha hapo, serikali ingelazimika kufunga mitambo baada ya muda si mrefu kutokana na HASARA.

YALIYOPITA SI NDWELE, TUGANGE YAJAYO

(1) Umuhimu wa CRUDE OIL REFINERY in TANZANIA bado upo.
(2) SEHEMU nzuri ya kujenga CRUDE OIL REFINERY Tanzania kwa sasa ni TANGA, ili kuweza kuchukua advantage ya CRUDE OIL kutoka UGANDA hapo baaadae.
(4) HATA bila kutumia CRUDE OIL kutoka UGANDA, bado kuna faida kubwa kujenga CRUDE OIL REFINERY Tanzania kwani kuna products nyingi sana zitatengenezwa locally.

Nawasilisha.
MJ
 
Back
Top Bottom