Nishati: Makosa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Pili - Kifo cha Kiwanda cha kusafisha mafuta TIPPER | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nishati: Makosa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Pili - Kifo cha Kiwanda cha kusafisha mafuta TIPPER

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Majoja, Aug 5, 2011.

 1. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Serikali ya awamu ya pili ilifanya kitu ambacho mpaka kesho naona ni cha kijinga sana.

  Sijui kama ilikuwa ni shinikizo la wafanya biashara au ushauri wa World Bank, sijui.

  Wenzetu kama Zambia walitupilia mbali ushauri huo ambao ulitolewa kwa shinikizo la kuwafaishisha makampuni makubwa ya mafuta.

  Baada ya Uhuru serikali ya awamu ya kwanza iliamua kisahihi kabisa kujenga kinu cha kuchuja mafuta-crude oil.

  Kinu hicho-TIPER Refinery ya pale Kigamboni ilifanya kazi nzuri tu na kwa muda mrefu sana.
  Zambia wakaenda mbali zaidi wao wakajenga bomba la mafuta ya crude oil toka Dar es salaam hadi kwao-bomba hili hadi leo linafanya kazi.

  Mantiki ya refinery ya Kigamboni haihitaji akili kubwa sana kuielewa.

  Importation ya crude oil inafanyika ONCE(mara moja) na hivyo freight charges zinalipwa once.

  Baada ya kurefine hiyo crude oil unapata petrol za aina zote, Mafuta ya taa(kerosine),Mfuta ya Kulainisha(lubricating oil),diesel,IDO(Industrial Diesel Oil), na hata lami za aina tofauti kuanzia Bitumen 50/60, 60/70,80/100 na hata Gesi(Liquefied Petroleum Gas-LPG).

  Kwa wale ambao hawakumbuki au hawakuwepo miaka hiyo, hizi products tulizipata hapa hapa nchini.
  Leo ukitaka kuagiza product yoyote kati ya hizo unalipia freight(usafirishaji) kwa each individual product.

  Si jambo la kushangaza kuwa leo bei za mafuta nchi ni karibu sawa na bei za Burundi, Rwanda hata Zambia pamoja na kuwa wao wanapitisha products zote hapa hapa nchini.

  Ki ukweli bei zetu za mafuta na products zake zilitakiwa kuwa chini kama tusingekisambaratisha kiwanda cha TIPER pale Kigamboni.
   
 2. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Du wengi wameshasahau kuwa tulikuwa tunachuja mafuta tuliyonunua wenyewe.
  Na nakumbuka karibu TPDC ivunjwe ili kulinda biashara za wakubwa.
  Mzee Ruksa saa hizi kimyaaaaa!!!!!!
   
 3. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  Mzee ruksa hakuharibu haya mambo kwa bahati mbaya bali alibase zaidi kwenye 10%
   
 4. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kumbe basi ufisadi ndani ya wizara ya Nishati umeanza siku nyingi sana na tunayoyaona(ya akina Jairo) ni wajukuu!!
   
 5. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Hivi tukisema serikali ya awamu ya pili ILIHUJUMU uchumi na kutengeneza mazingira ya ufisadi unaoendelea sasa hivi katika wizara hiyo, tutakuwa tumekosea kweli?
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Tumefika pabaya sasa tukaongelee wapi wakubali kurudisha ile hali ya zamani tukubali tulikosea na sasa turudishe!
  Tunajifunza kwa makosa na sababu tumeona makosa yetu sasa nikujipanga upya tatizo lipo wapi! MAGAMBA JITAHIDINI BASI NCHI INAIBIKA NAMNA HII KWELI!
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Da mkuu ni kweli kabisaa na hii pipeline ya wazambia imepita kwetu na mpaka leo bado inafanya kazi vizuri tuu tena wanaunload toka kwenye Bandari yetu hapahapa, tunaweza kuanza upya tusiwe wachoyo inaweza isionyeshe impact sasa but walau hata vijana watu waje wafurahi!
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  utakuwa umepatia mkuu..ila kikubwa sio kuingizwa kwa hujumu uchumi nchi swala hapa kama waliona hilo kipindi hicho wanafanya nini sasa hivi ndo hapa sasa watz waleo wanahitaji mabadiliko kwenye hilo swala..
   
 9. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa vyovyote vile kupokea ushauri unao kufaidisha wewe mwenyewe na ukijua wazi kuwa Taifa kitapata hasara kwa kiwango tunachokiona leo ni UHUJUMU UCHUMI.
   
 10. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sijasikia popote hata kwa mipango tu , ya kufufua ile Refinery ya Kigamboni ili kuondokana na adha hii ya gharama kubwa ya nishati-mafuta.
  Kati ya vitu ambavyo Mzee Ruksa atalaaniwa na vizazi vijavyo ni kukubali ushauri usio na tija kwa nchi.
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Jiulize, utajiri wa Kikwete kaupata wapi?
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  leo asubuhi nimetoka kuwahabarisha watu kuhusu tipper wanashangaa tu, ndo hivyo nyerer aijenga hawa wahuni wanuza na kuharibu nchi!
   
 13. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Lisemwalo lipo!
   
 14. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli kila nikilifikiria suala la TIPER huwa najiuliza kama kweli tuna viongozi wenye uchungu na nchi hii.Mimi bado nafikiri kuivunja TIPER ni suala la kuhujumu uchumi na hamna namna nyingine ya kulielezea.
   
 15. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tiper iliacha kufanya kazi wakati wa utawala wa Mwalimu,Wataliani ambao walikuwa wabia waliomba kuongezewa shares ili kukarabati kiwanda ambacho mitambo ilikuwa imechakaa na wakakataliwa na baadae kujitoa kabisa.Uwezekano wa tiper kufanya kazi sasa haupo tena kutu imekula kila kitu labda kijengwe kingine. Tusipotoshe watu hapa kwakuwa wengi hawakuwepo muda huo.
   
 16. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tatizo letu ni moja miaka yote na tusipobadilika hamna kitakachoenda sawa,hatuna tamaduni ya kufanya service ya vitu vyetu vikishajengwa mabwawa ya umeme,viwanda,barabara,majengo na vitu vingine.Usafishaji wa mafuta ulikoma Tiper late 70's early 80's na matenki yaliendelea na kazi ya kuhifadhi refined pruducts kazi ambayo pia baada ya muda ilishindikana baada ya matenki kuanza kuvujisha kwa uchakavu.
   
 17. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu Uporoto1, you are PLAIN WRONG on this issue.
  Peruse your facts to refresh your self.
  TIPER ilikuwa inafanya kazi hadi 1991, licha ya kuwa na migogoro.1991 Rais alikuwa Mzee Ruksa na si Mwalimu.
  Mwalimu alisimamia ujenzi wa kiwanda hiki kna kuki-commisiion mwaka 1969.
  Please read your history well.
  Naaambatanisha hii reference toka net.

  Tiper Refinery - Simple Oil Refinery in Dar es Salaam, Dar es Salaam, Tanzania

  ::
  Overview:: Refinery Units:: Contact Details:: General Information:: Related Organisations:: Contact Information

  :: Update :: Upgrade
  [
  Overview
  The Tanzanian and Italian Petroleum Refining Co Ltd (Tiper) refinery at Dar es Salaam, Tanzania was originally built between 1963 and 1966 and commissioned in 1969. It is a topping and reforming refinery with a nameplate distillation capacity of 875 ktonnes per annum (17,500 bpd) but is generally operating at approximately 60% of rated capacity. The refinery is a limited company incorporated in Tanzania under the parastatal Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC). The shareholders of the company are the Treasury of Tanzania (50%) and Agip (50%) who are also the refinery's operators.
  Since 1991 the refinery has been undergoing rehabilitation and modernisation in order to increase its efficiency, safety standards and output. The rehabilitation is (was)intended to restore output to its nominal capacity despite a recommendation by the World Bank, strongly opposed by the Tanzanian government, that the refinery be closed. The Tanzanian government is of the opinion that the refinery is essential to the Tanzanian economy and are working to keep it operating.The upgrading programme also includes a revamp of the boiler and the installation of a new instrument panel. TPDC has also considered installing conversion units in order to boost the yield of white product.

  (source and ref: mBendi.com)

  Kiwanda kilikuwa scrapped during the second half ya awamu ya mzee Ruksa.
  Be informed.
   
 18. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Shibe mwana malevya!! Alijisau kwa short term gains za 10% na sasa joto ya jiwe ya kupata mafuta inamkumba hata yeye na vijukuu vyake. Na ikifikia vitukuu basi navyo vitalalamika kama tunavyolalamika sisi hapa hii leo baada ya mali na immunity yote kuwa imetoweka!!! These people are too short-sighted for their own good!!
   
 19. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Muhahahaha Tipper haijafa Enzi za Mwalimu lol Kuna Bosi Mmojawapo wa Tipper Miaka Hiyo ya 80s hadi 90s Paul Rweyemamu Tulikuwa Tunaishi nae Upanga Mtaa Mmoja Wacha Kuzusha na Kumwaga Povu Tipper Imededi Na Mwinyi...
   
 20. m

  matambo JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  yawezekana ikawa kweli tiper ilikufa wakati wa mwinyi, lakini yawezekana ilikuwa tayari imeshajichokea soo mwinyi akadondokewa na jumba bovu tu, kwani viwanda vingi vilivyokuwa vya umma vikabinafsishwa baadae je havikuyumba enzi ya mwalimu??? mbona pia utawala wa mwalimu unalaumiwa kwa kulea wezi wachache au wale waliokuwa wakiharibu hapa na kusogezwa kule kwa kisingizio kuwa hakuna wataalamu wengine? hili laweza kuwa sawa na mgonjwa aliyecheleweshwa kuletwa kituoni kisha akaja kufia mikononi mwa daktari na kuishia kumlaumu dr kwamba kasababisha kifo cha mgonjwa ilhali mgonjwa mwenyewe alikuwa dhoofu,
  binafsi, naamini mashirika mengi ya umma yaliyumba kipindi cha mwisho cha utawala wa nyerere kutokana na sababu mbalimbali za ndani na za nje, na mind you, mashirika mengi yalitegemea ruzuku ya serikali lakini nyie nyote mwajua serikali haikuwa na pesa sxasa mashirika hayo yangejiendeshaje???
  naomba nifundishwe na nielekezwe kwani nimepata kusikia kuwa kipindi mwinyi anaingia nchini(nikimquote warioba alipohojiwa itv kwenye dakika 45 ) kwamba wao walipokea nchi ikiwa haina hela kabisa na mfumuko wa bei ulikuwa 36%, lakini mpaka mwaka 1990 mfumuko ulipungua kufikia 18%, na yeye akajinasibu kuwa hayo kwao yalikuwa mafanikio makubwa katika serikali ya kipindi chake, sasa kwa kuwa mashirika mengi ya uma yalitegemea ruzuku yangeendeleaje???
  unless tuelezwe vinginevyo kwamba mpaka 1985 , TIPER ilikuwa ikiendeshwa kwa ufanisi ila kuanzia 1986-its death ndo ilianza kuyumba nitaamini ni sababu ya mwinyi, vinginevyo mimi nitaamini nyerere na utawala wake walichangia kumchelewesha mgonjwa ila akaja fia mikononi mwa daktari, lawama iwe pande zote to be fair
   
Loading...